jozee jose
Member
- Sep 22, 2022
- 52
- 120
Tangu January Hadi katikati ya mwezi huu( April) tumekuwa tukisikia na kushuhudia mvua kubwa zikinyesha Kwa baadhi ya mikoa nchini Tanzania.
Kwa mtazamo wangu haya ni matokeo ya ubinafsi wetu juu ya mazingira yanayotuzunguka.
Wiki Moja iliyopita niliongea na mdau mmoja ambaye Yuko mkoani Mbeya alielezea janga la maporomoko ya matope(mud flow) kuwa ni jambo ambalo halikuwahi kuwepo kabla pia amesema mvua zimekiwa kubwa mno hajawahi kuziona tangu 1999, Akaeleza sababu kuu ya maporomoko ya matope kutoka mlima kawetere ni ukataji wa miti ovyo, Kwenye hili alitia mkazo kuwa hakuna Sheria Wala hatua madhubuti ambazo anasimamia katika kuyatunza mazingira hayo.
Athari zilizotokea ni kama watu wamekosa makazi, miundo mbinu kama Barabara na mitaro imeharibika pamoja na mazao ya kilimo kama mahindi na maharagwe.
Ni nini tukitarajie baada ya mvua hizi?
Kuongezeka Kwa uhitaji hasa Kwa bidhaa ya chakula hili litapelekea vitu kupanda bei na ugumu wa maisha kuongezeka. Sasa ni nani alaumiwe?