Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,232
- 3,334
Nimekuwa nikisafiri kwenda nchini Kenya mara kwa mara kwa shughuli zangu binafsi. Katika safari hizo, nimepata fursa ya kufuatilia vyombo mbalimbali vya habari, hususan televisheni na redio, na kufanya ulinganisho na hali ilivyo hapa Tanzania.
Jambo moja kubwa nililolibaini ni kwamba, nchini Kenya, hususan nyakati za asubuhi, vyombo vingi vya habari vinatoa nafasi kubwa kwa mijadala ya kitaifa inayohusu maendeleo ya nchi, uchumi, siasa, uwajibikaji wa viongozi, sera za serikali na changamoto zinazowakabili wananchi. Mara nyingi mijadala hiyo huwa mizito, yenye hoja na mitazamo tofauti, na huwapa wananchi fursa ya kuelewa masuala muhimu yanayoathiri maisha yao ya kila siku.
Lakini nikigeukia upande wa Tanzania, ninabaini tofauti kubwa. Kwa sasa, ukifungua redio nyingi asubuhi au jioni, sehemu kubwa ya mijadala inahusu mpira wa miguu. Ni mpira asubuhi, mpira mchana na mpira jioni! Wakati mwingine mijadala hiyo inakuwa mingi kiasi cha kufunika kabisa masuala mengine muhimu ya kitaifa.
Sina tatizo na michezo, wala sipingi umuhimu wa mpira wa miguu katika jamii. Michezo ni sehemu muhimu ya burudani, afya na uchumi. Lakini je, ni sahihi kwa vyombo vya habari kutumia muda mwingi kujadili mpira huku masuala yanayogusa maendeleo ya wananchi yakipewa nafasi ndogo?
Nakumbuka miaka ya nyuma, tulikuwa tukifungua redio au televisheni asubuhi na kukutana na mijadala yenye kujenga uelewa wa wananchi kuhusu kilimo, uchumi, elimu, afya, utawala bora, ajira, biashara na mustakabali wa taifa letu.
Leo hii, mijadala ya aina hiyo inaonekana kupungua kwa kiasi kikubwa katika baadhi ya vyombo vya habari.
Tunapaswa kujiuliza: Je, mabadiliko haya yamesababishwa na mahitaji ya wasikilizaji na watazamaji? Je, ni ushindani wa kibiashara na kutafuta matangazo? Au tumefikia mahali ambapo vyombo vya habari vinaona ni rahisi zaidi kujadili michezo kuliko kuendesha mijadala ya kina kuhusu masuala ya maendeleo na uwajibikaji?
Swali langu kwa wadau wa habari na Watanzania kwa ujumla ni hili: Tumefikaje hapa, na nini kifanyike ili kurejesha mijadala yenye tija kuhusu maendeleo ya taifa letu katika vyombo vya habari?