Tumekutana kwenye mwamvuli!

Tumekutana kwenye mwamvuli!

jouneGwalu

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
2,687
Reaction score
1,782
Maisha yanaendelea kama tunavyojua dar yetu tena, kamvua kananyesha mdogo mdogo kipindi hiki,
trii triii..... napokea simu, mshkaji wangu ananiambia kuna dili posta so niwahi mda huo mapema tu kama saa sita ya mchana, natoka uswazi kidogo na vimanyunyu natembea hapa na pale mvua inazidi, kurudi nyuma mwiko so sababu hadi kituoni sio mbali nkasema nikimbie tu fasta nikajibanze palepale wakati nasubiria daladala,
Oh ona mambo yetu bongo sasa nakuta pale kituoni maji yamejaa ile mbaya huwezi hata kusimama, kwa pembeni kunajamaa anakibanda chake ila nacho raia wamejaa kila mtu anakimbia mvua.... nikadata, mvua inakomaa
Mungu saidia nataka nivuke barabara niende kwenye maduka ya ng'ambo, nika-stuck kwa kiherehere cha macho whaoooooo nini hiki.....??
Mashosti wawili wapo na miamvuli yao, wanakuja hapo kwangu pembeni ya kibanda..... alhamdulilah, bila kukalibishwa nikadandia mwamvuli wa shosti mmoja, poozi yote imeniisha nimelowa kiasi flani, jasho kwa kukimbia, natoa kitambaa najifuta futa huku nahema...., "pole, pole sana" mtu ananiambia, oh kumbe ni mwenye mwamvuli bwana, hata sula sijamuangalia kumbe sasa kwa kusikia hiyo sauti ndio nikatulia nimuangalie tusalimiane, dooooo jamani Mungu huyu kaumba, tumuache tu aitwe Mungu kwa utukufu wa viumbe vyake.
Ni mtoto mzuri, naomba niishie hapo tu kwa sifa na vidume wenzangu wote muelewe kuwa huyo mtoto ni mzuri bwana. Tukabadilishana maongezi kuhusiana na hali ya hewa ya mvua na shida ya usafiri dar. Siwezi kumsemea ila kuna namna alikuwa ananiangalia hadi kama nikawa na-blush hivi, the same way na yeye nikijaribu kumkazia macho straight kwenye macho yake hivi... wanasema hisia zinaongea?? ofcz siku-develop kitu chochote personal, just zikabaki hisia ndani yangu tu. Mmmmmhh bwana wee hadi tukawa tumemsahau yule shosti mwingine kama wapo wote! Baada ya kama dakika 10 hivi, daladala ya posta ikaja!
Dili muhimu kuliko mapenzi?? Nikakwea zangu daladala nikasepa japo shosti alitaka tupande wote ila mwenzie akakataa eti limejaa.
Nipo kwenye daladala ndio nakumbuka (japo sikujuta, wala sijutii), simjui jina lake wala sijachukua namba ya simu, just nakumbuka "tulionana kwenye mwamvuli wake"
Ah mvua hizi zina mambo.
 
nimependa sanauandishi wako duuh!!
hadi raha kusoma, nilitaka uendelee tu
huwa unaandika hadithi JG?
Hongera sana
 
Una kipaji cha kuandika jaribu kutafuta ajira kwa Shigongo hahaha!

haaaaaa,kama vile nime igilizia kwako ati!
Ila kweli bro,wekeza hapo kama hauko tyt sana na masuala mengineyo
 
u mwandishi mzuri sana wa story,
story yako nimeipenda mtiririko wake,
haichoshi kuisoma, bali inavutia kuisoma na kutaka kujua nini mwisho wake,

KIPAJI HIKI KINAWEZA KUKUSAIDIA KUTIMIZA NDOTO ZAKO.......HONGERA SANA.
 
Story yako haiboi, iko constant hadi mwisho. Ingeboa kama ungeanza kuhangaika na kuomba mawasiliano. Story nzuri imenirudishia mudi ya kupiga shule.
TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA.
 
Huyu jamaa domo zege kashindwa tu kuandika kwamba alijilaumu kwa nn hakuchukau namba ya cm,though story ni nzuri.
 
story yako haiboi, iko constant hadi mwisho. Ingeboa kama ungeanza kuhangaika na kuomba mawasiliano. Story nzuri imenirudishia mudi ya kupiga shule.
Tanzania bila ukimwi inawezekana.
ha ha ha,simpaka iwe story????? Mwenzenu alijua mtasema ni true story.
 
Huyu jamaa domo zege kashindwa tu kuandika kwamba alijilaumu kwa nn hakuchukau namba ya cm,though story ni nzuri.

mmh!watu hamkosi la kukandya!!unag'ata na kupuliza..lol
mkuu umetoa thanks 2 tu tangu 2008!!!!
kungekuwa na kitufe cha thanks ningekwambia umpe thanks ila hakuna
basi japo mlike, ee wacha uchoyo
 
Hivi kumbe ni wewe???

tehetehe!!! kumbe ulikuwa wewe lizy!....

alafu mkuu umenifurahisha ni hii statement (Siwezi kumsemea ila kuna namna alikuwa ananiangalia hadi kama nikawa na-blush ) mwenzio niliwahi kudhani wale dada wanaofanya kazi ndani ya ndege wamenizimikia walivokuwa wanasmile.... !! so take it easy easy tiger .. :A S 465:
 
Hapo lazima sinza kumekucha, nice one nimependa story yako. sasa kuna njemba ilimtokea hovo akawa anaenda kituoni hapo kila siku wapi, mwisho akaamua kutengeneza poster kama kumi hivi akabandika kila mahali pale kituoni hadi alimpata
 
Kaka hupo juu kwa stori ipo hot.
 
hadithi nzuri, ila hujui wapi uweke R na wapi uweke L
 
Back
Top Bottom