Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,455
- 5,134
Kuanzia asubuhi ya leo Juni 30, 2026, Wananchi wengi tumekwama kupata huduma ya kununua dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kufuatia mkwamo wa kimfumo uliosababisha hitilafu katika utoaji wa Namba za Malipo za Serikali (Control Numbers).
Hali hiyo imetuumiza wengi kwa kuwa watumishi wa Muhimbili hawataki kupokea malipo cash na hata kwa wale waliojaribu kuomba walipe leo kisha waje baadaye au kesho kuchukua dawa wameambiwa haiwezekani kwa kuwa ikifika kesho yake malipo yao hayatasomeka kwenye mfumo.
Mkwamo huo umetokana na kwamba wanadai leo ni siku ya mwisho ya Mwaka wa Fedha kwa Serikali hivyo mifumo imesumbua.
Wale wachache ambao walikuwa wamelipa fedha zimeenda hazijasoma na hazijarejea kwao, hivyo malipo yamebaki hewani.
Hivi kweli kwa Dunia ya sasa, inamaana Serikali na Muhimbili wenyewe hawakujua kuwa kuna kiu kama hiki kinaweza kutokea? Inamaana watu wakose dawa sababu tu ya mfumo? Kwa nini wasiweke utaratibu wa cash hata kama ni kwa dharura? Inasikitisha sana hii.
Ufafanuzi ~ Muhimbili: Huduma ya kulipia kwa Namba za Malipo ilirejea, halikuwa tatizo la muda mrefu