Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Wakenya wanaongoza kwa kununua bidhaa za Tanzania, lakini ni bidhaa ambazo hazijaongezwa uthamani, malighafi (raw material) na Kenya wanaongoza kwa kuziongeza uthamani bidhaa hizo na kwenda kuziuza Dubai, Ulaya, Marekani na zinazobaki wanazileta tena kutuuzia Watanzania, nafurahi kuwa tumekwenda kwenye mkutano wa Kilimo nchini Marekani kufanikisha mpango wetu wa kuifanya Tanzania kinara wa uwekezaji na ghala la kilimo hapa Africa kupitia mpango unaofadhiliwa na Marekani unaoitwa Feed the Future,lakini kitu cha muhimu zaidi kama Taifa la Tanzania kwenye kilimo, tunahitaji kuongeza mnyororo wa thamani (value chain creation) ambao ni mtiririko wa shughuli zote zinazofanywa katika uzalishaji hadi kumfikia mlaji wa mwisho, kwa mfano;
✓Uzalishaji.
✓Usafirishaji.
✓Usindikaji.
✓Uhifadhi.
✓Upangaji wa madaraja.
✓kufungasha na,
✓masoko.
-Tunahitaji nini Watanzania kwenye mnyororo wa thamani.
Watanzania tunahitaji utekelezwaji wa mradi wa kuongeza mnyororo wa thamani katika bidhaa na malighafi za Tanzania utanufaisha watu wengi hasa wa kipato cha chini ikiwemo misaada ya kifedha (grants) kwa kuwa Tanzania ndio shamba la malighafi za bidhaa zote zinazopatikana Afrika Mashariki, tukiweza hili la kuongeza mnyororo wa thamani, Tanzania tutachukua nafasi kubwa katika biashara na mauzo, kwenye mnyororo mzima wa thamani kwenye kilimo (agricultural value chain) kitengo Cha kurahisisha mahusiano na mawasiliano kwa washikadau (stakeholders) wote ambao wanaingia kwenye sekta hii ya kilimo na ufugaji, taarifa zote muhimu za mkulima ambaye ni mdau muhimu kwenye uzalishaji wa mnyororo wa thamani, uwezeshwaji kama mkulima atataka kupata mafunzo yoyote kutoka kwa taasisi yoyote, mafunzo hayo yanaweza kua, jinsi ya kulima kisasa ( good agricultural practice) mafunzo ya kifedha (financial education) nk, taarifa zote za kimikataba, ikiwa mkulima au wazalishaji watakua na mkataba na mnunuzi wa malighafi au bidhaa, na mwisho taarifa zote za mbegu na mbolea ambazo mkulima alitumia mwanzoni mwa shughuli yake, pia kurekodi taarifa za mavuno mwishoni wakati wa mavuno, baada ya hapo twende kwenye viwanda tukaongeze uthamani wa malighafi zetu ili ziwe bidhaa adimu, tukatae kuwa wachuuzi wa finished goods zilizotokana na malighafi zetu.
Tunapokwenda Marekani kwenye mikutano wa kilimo kipindi hiki cha Noeli,tusiende kupokea zawadi za krismasi,ni muhimu tunapokwenda kwenye mikutano hiyo ya kilimo,kitu cha kwanza lazima tuwe na vipaumbele vyetu kama matatizo ya kutokuwa na mtaji, naamini USA haitoi pesa kupitia Serikali bali kupitia miradi,lakini pia teknolojia, kama tutashindwa kupata pesa ya msaada kwa ajili ya kilimo na mnyororo wake wa thamani basi mtaji utapatikana kupitia resources tulizokuwa nazo kwa kuzisimamia vizuri, na kwa namna ya pekee mtaji utapatikana kwa kubana matumizi na kuepuka matumizi ya hovyo kama za nje ya nchi zisizo na faida, teknolojia tutaipata kwa kutumia wizi kupitia ushushushu wa watu wetu huko kwenye teknolojia kwa kubadilishana na baadhi ya resources zetu, tuige mfano wa China,tunaweza kuipata teknolojia kwa kutumia watu wetu wa TISS vizuri kupata teknolojia mpya na kwa kuhakikisha watu wanakwenda kusomea vitu vyenye tija na kuja kufundisha wengine nini cha kufanyaTukishazalisha lazima dunia ije kununua maana tayari ina mahitaji ya tulichozalisha, dunia ina mahitaji ya dhahabu zetu, dunia inamahitaji ya gesi yetu,dunia inahitaji makaa yetu ya mawe, dunia inahitaji korosho zetu,dunia inahitaji graphite zetu, dunia inahitaji mahindi yetu, dunia inahitaji mchele wetu, nk nk.. vyote hivi thlivyonavyo lazima hao wanaitwa wawekezaji waje, ni sisi tu kutumia akili,
Nimalizie na China tuionayo leo, Hisense ni moja ya kampuni zinazotengeneza electronics ikiwepo television tena kwa kutumia cheap za kichina na inamilikiwa na Serikali ya China, teknolojia iliyoe delezwa kwa ubunifu wa kichina umepelekea China kuwa na licence ya kutengeneza Samsung, iphone na brand nyingine nyingi ndio maana hata kutengeneza Hisense, Mchina hajapata shida sababu technology ya television ameipata kupitia Samsung, sony nk.
Mchina anajitahidi sana kuingia kwenye soka, teknolojia anayoiendeleza kutoka soka la sasa itamfanya aende kuwekeza sana kwenye soka, kwa jinsi China inavyoweza kuendeleza teknolojia kutoka iliyopo sasa, basi China anaweza kwenda kutengeneza league ya kuvutia kama ilivyo ya Uingereza,fikra hii inaonyesha Mchina halali wala hapoi, Mchina anawaza suala la brands zake kuteka soko la dunia,kwa sasa Mchina anaweka low cost of production ikilinganishwa na nchi nyingine ukiacha india, dunia iliyobaki yote imeamua kwenda China kuoutsource manufacturing kutokana na teknolojia iliyoendelezwa, sijui kama wenye dhamana wananielewa, Umasikini tulionao Watanzania ni wa kujitakia na unatengenezwa na watu kwa manufaa yao na sio kwa manufaa ya taifa la Tanzania.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;-
-Assessment on the effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.