TUMELETWA NA MUNGU

TUMELETWA NA MUNGU

Joined
Jul 6, 2024
Posts
97
Reaction score
72
Tumeletwa na Mwenyezi Mungu ili tukemee mauozo ya ubinafsi, uchocho, na roho za korosho; zinyooke, zitenende haki.

Nilisikika katika ulimwengu wa kiroho huko ndotoni nikikemea mauozo. Nakumbuka tarehe 18/10/2021, Mheshimiwa Steave Masato Wasira, ex-waziri, ex-mbunge, na mwenyekiti wa Chuo cha Kivukoni, alisema kwamba kushauri kukosolewa ni sehemu ya maisha ya uongozi wa aina yoyote, sio wa kisiasa tu. Mwisho wa kunukuu. Shekhe Walid Alhad Omar Kawambwa, Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, tarehe 05/10/2024, akiwa msibani mbele ya jeneza la Dida kabla ya kuswaliwa, alisema, "Tuambiane ukweli." Mwisho wa kunukuu.

Maadili yaliyo mema ndani ya nchi yenye ucha Mungu ni kusoma vitabu vitakatifu na kuwasikiliza kwa nidhamu wawakilishi wa Mwenyezi Mungu wanasimamia na kutupatia maelekezo yahusuyo Muumba wetu. Pili ni kutambua kuwa sisi Watanzania tunatoka familia tofauti zenye tabia na mitazamo tofauti. Ili kudumisha maadili ya nchi na kuleta utulivu, tukaweka katiba ya nchi, katiba, kanuni, miongozo, na taratibu za vyama vya siasa. Tukatengeneza sheria itakayosimamia vyama hivyo, na tukatengeneza sheria nyingine nyingi ndani ya nchi, ambazo ili zitekelezeke tukaweka mfumo wa kuwa na viongozi wanaotakiwa kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu na kisha kusimamia haya kwa uadilifu na uaminifu.

Ajabu, walioaminiwa baadhi wamekengeuka kiasi kwamba hata ule uovu wao hauna kificho tena mbele ya jamii yenye shauku ya kuona inatendewa haki kwa mujibu wa viapo vya waongoza njia. Sasa uovu unapozidi, ndipo Mwenyezi Mungu anatutuma sisi ambao tunadharaulika sana kwa ukweli wetu ambao ni kama vichekesho mbele za watu walioamua kukufuru. Hatutachoka kusema kwa sababu hii ndiyo kazi Mungu aliyotuitia kuwaonya wale wote waliopituka mipaka kiasi cha kujiaminisha ya kuwa wao ndiyo Tanzania na walio chini yao ni kama kyanyampwowaaa.

Viongozi wa hovyo ndani ya nchi yetu baadhi hawana hofu kabisa ya kumhofu Mwenyezi Mungu. Mfano, wanakula viapo wakitamka Mwenyezi Mungu huku wakiwa wamepewa jukumu la kuchukua hatua dhidi ya uvunjifu wa mifumo. Ajabu, nyakati tulizomo, viongozi hao kabla hawajachukua hatua huangalia yule wanayetaka kumchukulia hatua ni safu ya mtu gani. Ikiwa ni wa mtu wao, basi viongozi hao hujifanya kama viziwi, kama mabubu, kama vipofu. Ila wakibaini wanayetaka kumchukulia hatua si wa kwao, utasikia kerele vyomboni na kote, na haraka mtu anachukuliwa hatua; na saa nyingine hao wanaochukua hatua wana mapungufu ya kisheria na kikanuni.

Hawa ndiyo wanaovuruga amani na utulivu kisha kusingizia watu wengine wasiohusika na uvunjifu huo. Vitendo vya kuchukua hatua kiubaguzi na kiupendeleo kunajenga chuki na kutowesha upendo ndani ya jamii ambayo kimuonekano inaonekana kama vile bado imelala kumbe zamani ilishaamka, inajielewa na inaona mauza uza yanayoendelea yaliyojazwa unafiki usiofichika. Kwa hali hii, twawezaje kusema kwa mujibu wa ibara 35(1) ya katiba kuwa sisi tunamsaidia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan?

Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika hafla ya kufunga tamasha la utamaduni la kitaifa huko Songea, nakumbuka tarehe 23/09/2024, alisema, "Tuwakatae wote wanaotaka kutugawa kwa sababu za kisiasa au tofauti za kiitikadi. Watanzania ni wamoja, Tanzania ni moja, sisi ni mtu mmoja." Mwisho wa kunukuu. Sisi tumeisha wakataa baadhi ya viongozi na kuonyesha kasoro na disari zisizovumilika ndani ya jamii ila bado wanalindwa. Sasa tufanyeje?

Wakili Msomi na Jasiri Edson Kilatu, akiwa maeneo ya mahakamani tarehe 24/09/2024, alisema, “Kuna kitabu kinaitwa cha wanyama - Animal Farm. Ambapo wanyama walisema wapo sawa lakini ikaonekana kuna wanyama wako juu ya wanyama wengine.” Mwisho wa kunukuu.

Mtume na Nabii Josephati Elias Mwingira wa Kanisa la EFATHA, tarehe 15/10/2018, alisema, “Ninataka Taifa la Tanzania lijiunge katika namna ya haki na sheria ya Mungu itulie ndani yao ili Mungu aweze kuibariki Tanzania.” Mwisho wa kunukuu.

Askofu Dkt. Benson Kalikawe Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, akitoa mahubiri tarehe 13/10/2024, alisema, “Mwenyezi Mungu anajihusisha sana na maisha yetu, na kila wakati akiona mambo yetu hayaendi vizuri, anatuma watu kutushtua.” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Nzabayanga Mpango, Makamu wa Rais, akimuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia katika kufunga kongamano la uhuru wa kidini Bara la Afrika lililofanyika Arusha tarehe 22/09/2024, alisema, “Dini zina mchango mkubwa katika kujenga familia na jamii zenye maadili mema. Familia na jamii zinazozingatia mafundisho ya dini zinazingatia pia maadili mema.” Mwisho wa kunukuu.

Nikashtuka katika kongamano la ulimwengu wa kiroho huko ndotoni nikiwa kimya.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Mathias Mugerwa Kahinga
 
Back
Top Bottom