Tumelogwa

Tumelogwa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
TUMELOGWA.

Na Thadei Ole Mushi

PhD Holder Harrison Mwakyembe amewataka watanzania waichangie timu ya taifa ili wapate motisha wa kucheza mpira. Hii ndio Tanzania na watanzania wenyewe ndio sisi tuna Tabia kama ya patasi hatuendi wenyewe mpaka tugongwe kwa nyuma.

Sikia....

AFCON 2019 ina wadhamini lukiki ambao wanahakikisha timu zote pale misri zinapata mahitaji yao yote, haya ndio mashindano ya juu kabisa kwa ngazi ya mataifa kwa bara la Africa. Kwa kutambua hivyo makampuni makubwa yamejitokeza na yamemimina fedha ya kutosha kuendesha mashindano. Makampuni rasmi ni kampuni la mafuta la TOTAL, Kampuni la Digital payments la VISA, Kampuni la Magari YAMAHA, Kampuni la Simu la ORANGE, Kampuni la matairi la CONTINENTAL, Kampuni la madawa la GILEAD, na Kampuni la vyakula la TEMMY`S. Hawa ndio official sponsors kila kitu kipo under Control.

Si hivyo tu.....

Timu zote zilizopo Misri zina vyama vyao vya mpira toka nyumbani. Vyama hivi vimejiandaa na timu zao toka na hata kabla ya kufuzu kwa timu zao. Hapa kwetu tuna TFF ambayo ilipata gawio la FIFA na Gawio la match zote (Gate Collection) kwa ligi zote nchini.

Si hivyo tu Bali.....

Timu zote katika nchi zao zina wizara ambazo zinashughulikia michezo huko nako wamejipanga toka timu zao zilivyofuzu. Fifa nao wametoa gawio kwa CAF ili kuendesha Haya mashindano.

Kubwa kuliko.....

Timu yetu ina sponsor wake ambaye ni Serengeti lager naye anamimina mamilioni kwa vijana......

Kupitia hayo yote sioni sababu ya watanzania kuchangishwa tena kwa ajili ya kusapoti timu.

Hoja ya MOTISHA.

Wachezaji wote waliopo pale misri mentality zao ni kunyakua kikombe hii ni motisha ya kwanza. Yaani kama kuna mchezaji anasubiri fedha zichangwe ndio acheze hatutafika mbali. Nani hataki kuweka historia kuwa alichukua Afcon 2019? Wachezaji wote pale Misri nia yao ni kucheza final na kuvaa medal za dhahabu.

Pili ni kitita cha fedha watakachoondoka nacho, bingwa anaondoka na $4.2 milioni ambazo ni sawa na bilioni karibia kumi (9,659,580,000). Unataka wapewe motisha gani nyingine?

Sisi waalimu tunajua utaratibu wa motisha kuwa ni kuimarisha Tabia Flani iliyotokea au kukomesha tabia flan isijirudie. Sasa taifa Stars haijacheza match hata moja tumeanza kuwachangia. Jukumu lao la pili ni kuwinda hizo dola za mshindi wa kwanza.

Hata hivyo wafahamu kuwa kuanzia robo final kuna kitita cha fedha watapata. Kwa nn wasiwaze hizi fedha?

Motisha ya tatu ni mchezaji kujiuza yeye binafsi, pale alipo Samata wala hawazi fedha anachowaza ni kuchukua ubingwa ili aandike historia yake binafsi na ajiuze zaidi kimataifa. Wachezaji wote pale Misri kichwani mwao hilo lipo, kwao hii ni motisha tosha.

Kuhusu hamasa!!!

Tumewekeza mno mbwembwe nje ya uwanja badala ya vitu technically, timu tumeshaimilikisha kina Makonda tumeitoa kwa wananchi sasa hivi wanakimbia nayo wanaoitwa kamati ya kuhamasisha timu ishinde. Maajabu kama haya unaweza kuyaona tu Tanzania. Kilichotokea watanzania wamekaa pembeni wamewaachia kamati ifanye mambo yao.

Sioni impact ya hiyo kamati ikibadilisha matokeo ndani ya uwanja. Kwamba tukishavaa hayo madera yaliyoshonwa kwa bebdera za Taifa ndio tutapata matokeo? Hivi ni vituko vya aina yake.

Nasikia TBC hawataonyesha Haya mashindano, yaani timu ya taifa inashiriki jambo kubwa hivi halafu Chanel ya Taifa wala haina habari inakimbizana na Chereko Chereko. Wanajua ni shilingi ngapi wanapoteza hapa za matangazo?

Je kwa watanzania ambao hawana kingamuzi cha Azam wataenda vibanda umiza kila Siku? Je wale ambao hawana uwezo wa kulipia vingamuzi vyao hawataona?

Dr Mwakyembe unafeli wapi mheshimiwa mbona nilikuwa nakuamini sana? Master planner wa wizara ni nani kwa sasa ni wewe au katibu mkuu au Mh Makonda? Maana kila mahali nakuona naye....naona mmeshampa na cheti cha kutambua mchango wake Haya mngeyafanya mwisho wa mashindano haraka ya nn?....

Tumelogwa

Ole Mushi
0712702602
1130483
 
Siiombei Taifa stars mabaya ila tutachakazwa sana..

Maximo alikuwa kocha mzuri na kikosi hakikuwa haba, ila tulichakazwa na Senegal bao 5 kama sikosei miaka ya 2006
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Vituko vya awamu hii ni funga kazi...

Badala ya kuimarisha timu wao wanafanya mambo ya kijinga sana...
[emoji23][emoji23][emoji23] ni amri kutoka juu
 
TUMELOGWA.

Na Thadei Ole Mushi

PhD Holder Harrison Mwakyembe amewataka watanzania waichangie timu ya taifa ili wapate motisha wa kucheza mpira. Hii ndio Tanzania na watanzania wenyewe ndio sisi tuna Tabia kama ya patasi hatuendi wenyewe mpaka tugongwe kwa nyuma.

Sikia....

AFCON 2019 ina wadhamini lukiki ambao wanahakikisha timu zote pale misri zinapata mahitaji yao yote, haya ndio mashindano ya juu kabisa kwa ngazi ya mataifa kwa bara la Africa. Kwa kutambua hivyo makampuni makubwa yamejitokeza na yamemimina fedha ya kutosha kuendesha mashindano. Makampuni rasmi ni kampuni la mafuta la TOTAL, Kampuni la Digital payments la VISA, Kampuni la Magari YAMAHA, Kampuni la Simu la ORANGE, Kampuni la matairi la CONTINENTAL, Kampuni la madawa la GILEAD, na Kampuni la vyakula la TEMMY`S. Hawa ndio official sponsors kila kitu kipo under Control.

Si hivyo tu.....

Timu zote zilizopo Misri zina vyama vyao vya mpira toka nyumbani. Vyama hivi vimejiandaa na timu zao toka na hata kabla ya kufuzu kwa timu zao. Hapa kwetu tuna TFF ambayo ilipata gawio la FIFA na Gawio la match zote (Gate Collection) kwa ligi zote nchini.

Si hivyo tu Bali.....

Timu zote katika nchi zao zina wizara ambazo zinashughulikia michezo huko nako wamejipanga toka timu zao zilivyofuzu. Fifa nao wametoa gawio kwa CAF ili kuendesha Haya mashindano.

Kubwa kuliko.....

Timu yetu ina sponsor wake ambaye ni Serengeti lager naye anamimina mamilioni kwa vijana......

Kupitia hayo yote sioni sababu ya watanzania kuchangishwa tena kwa ajili ya kusapoti timu.

Hoja ya MOTISHA.

Wachezaji wote waliopo pale misri mentality zao ni kunyakua kikombe hii ni motisha ya kwanza. Yaani kama kuna mchezaji anasubiri fedha zichangwe ndio acheze hatutafika mbali. Nani hataki kuweka historia kuwa alichukua Afcon 2019? Wachezaji wote pale Misri nia yao ni kucheza final na kuvaa medal za dhahabu.

Pili ni kitita cha fedha watakachoondoka nacho, bingwa anaondoka na $4.2 milioni ambazo ni sawa na bilioni karibia kumi (9,659,580,000). Unataka wapewe motisha gani nyingine?

Sisi waalimu tunajua utaratibu wa motisha kuwa ni kuimarisha Tabia Flani iliyotokea au kukomesha tabia flan isijirudie. Sasa taifa Stars haijacheza match hata moja tumeanza kuwachangia. Jukumu lao la pili ni kuwinda hizo dola za mshindi wa kwanza.

Hata hivyo wafahamu kuwa kuanzia robo final kuna kitita cha fedha watapata. Kwa nn wasiwaze hizi fedha?

Motisha ya tatu ni mchezaji kujiuza yeye binafsi, pale alipo Samata wala hawazi fedha anachowaza ni kuchukua ubingwa ili aandike historia yake binafsi na ajiuze zaidi kimataifa. Wachezaji wote pale Misri kichwani mwao hilo lipo, kwao hii ni motisha tosha.

Kuhusu hamasa!!!

Tumewekeza mno mbwembwe nje ya uwanja badala ya vitu technically, timu tumeshaimilikisha kina Makonda tumeitoa kwa wananchi sasa hivi wanakimbia nayo wanaoitwa kamati ya kuhamasisha timu ishinde. Maajabu kama haya unaweza kuyaona tu Tanzania. Kilichotokea watanzania wamekaa pembeni wamewaachia kamati ifanye mambo yao.

Sioni impact ya hiyo kamati ikibadilisha matokeo ndani ya uwanja. Kwamba tukishavaa hayo madera yaliyoshonwa kwa bebdera za Taifa ndio tutapata matokeo? Hivi ni vituko vya aina yake.

Nasikia TBC hawataonyesha Haya mashindano, yaani timu ya taifa inashiriki jambo kubwa hivi halafu Chanel ya Taifa wala haina habari inakimbizana na Chereko Chereko. Wanajua ni shilingi ngapi wanapoteza hapa za matangazo?

Je kwa watanzania ambao hawana kingamuzi cha Azam wataenda vibanda umiza kila Siku? Je wale ambao hawana uwezo wa kulipia vingamuzi vyao hawataona?

Dr Mwakyembe unafeli wapi mheshimiwa mbona nilikuwa nakuamini sana? Master planner wa wizara ni nani kwa sasa ni wewe au katibu mkuu au Mh Makonda? Maana kila mahali nakuona naye....naona mmeshampa na cheti cha kutambua mchango wake Haya mngeyafanya mwisho wa mashindano haraka ya nn?....

Tumelogwa

Ole Mushi
0712702602
View attachment 1130483
Hii ni aibu ya karne.

Nchi nyingine wana budget kwa ajili ya AFCON in billions of shillings.

We can do better than this. Mwisho wataenda kuomba msaada kwa "mabeberu" wale wale.
 
Hapana nakataa, hakuna kulogwa hapa

Hii ndio hali halisi...Wajinga wanawaongoza wasomi...Akili za Jalalani hizi....
 
Unapoanza kuweka pembeni au inapojiweka pembeni Taasisi Rasmi ya kusimamia Mpira wa Miguu (TFF) na kuanzisha Taasisi nyingine isiyo rasmi kwa jina la Kamati ya Ushindi, asili itakuja kutueleza mbeleni kuwa tulishakosea huko nyuma..
Kama Rais wa TFF anataka siasa, atupishe aende kwenye Siasa..
Watanzania kwa sasa wako pembeni wanaangalia mbwembwe za Kamati ya Ushindi..
Bado tuna safari ndefu.. tunaleta Utani kwenye Mambo ya Msingi..🙁🙁
Zaidi ya hapo kwa kutengeneza hayo mavazi yanayofanana na Bendera ya Taifa bila ruhusa wamevunja Sheria namba 15 ya 'National Flag and Coat of Arms' ya 1971 na adhabu yake ni faini au kifungo kisichozidi miaka miwili..
 
Back
Top Bottom