Maana ya kumpoteza ni kuwa muendapo nyinyi mwenzenu hapaoni, hawezi kupaona na kwa hiyo hawezi kuja mlipo, nanyi japo mwamuona hamna aina ya sauti anayoweza kuisikia, hamna namna na aina ya maneno kumwambia aamke kinyume chake atafukiwa.
Unaweza ukampoteza mtu kama vile kwa kumpa ushauri usiofaa, kumuonyesha njia tofauti na ile itakayomfikisha anakotaka, au kumfundisha tabia chafu..hapo kuna mchango wako katika kumpoteza
Lakini unaweza ukampoteza mtu kwa maana kwamba amefariki kwa hiyo uwepo wake umepotea na mliobaki hai mnabaki bila yeye (aliyekufa)..hapo hakuna ulichochangia katika kufa au "kupotea"' kwake ila mnabaki na hali ile ya kumpoteza tu
Hiyo ni tafsiri sahihi kabisa., kwani lengo hasa la kutumia maneno kama tumepoteza., ameaga dunia., hatunae tena.,, lengo hasa hapa ni kupunguza ukali wa maneno (tafsida) na kuonesha ushirikiano kwa lengo la kumfariji mfiwa ama kufarijiana