Tumempoteza mpendwa wetu

Tumempoteza mpendwa wetu

Ok9

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Posts
4,549
Reaction score
4,133
Mara zote msiba ukitokea tunatumia kauli ya "TUMEMPOTEZA" hii ina maana ya kwamba na nyie mlichangia kwenye kifo chake....

Wadau wa lugha mnasemaje hapa
 
Nafikiri ni sahihi kabisa,kwani wkt wa uhai wake mlishindwa kumnusuru na kifo,mkampoteza!
 
Maana ya kumpoteza ni kuwa muendapo nyinyi mwenzenu hapaoni, hawezi kupaona na kwa hiyo hawezi kuja mlipo, nanyi japo mwamuona hamna aina ya sauti anayoweza kuisikia, hamna namna na aina ya maneno kumwambia aamke kinyume chake atafukiwa.

Ndio maana tunasema "tumempoteza mwenzetu"
 
Mara zote msiba ukitokea tunatumia kauli ya "TUMEMPOTEZA" hii ina maana ya kwamba na nyie mlichangia kwenye kifo chake....

Wadau wa lugha mnasemaje hapa

Kumpoteza mtu kunaweza kukawa na maana kama mbili

Unaweza ukampoteza mtu kama vile kwa kumpa ushauri usiofaa, kumuonyesha njia tofauti na ile itakayomfikisha anakotaka, au kumfundisha tabia chafu..hapo kuna mchango wako katika kumpoteza

Lakini unaweza ukampoteza mtu kwa maana kwamba amefariki kwa hiyo uwepo wake umepotea na mliobaki hai mnabaki bila yeye (aliyekufa)..hapo hakuna ulichochangia katika kufa au "kupotea"' kwake ila mnabaki na hali ile ya kumpoteza tu
 
Hiyo ni tafsiri sahihi kabisa., kwani lengo hasa la kutumia maneno kama tumepoteza., ameaga dunia., hatunae tena.,, lengo hasa hapa ni kupunguza ukali wa maneno (tafsida) na kuonesha ushirikiano kwa lengo la kumfariji mfiwa ama kufarijiana
 
Back
Top Bottom