JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Moja kati ya jambo ambalo limekuwa likipigiwa kelele ni kuhusu ubora wa huduma za Watoa huduma katika taasisi na Mamlaka mbalimbali za Serikali, inaonekana ni kama sehemu ambayo Watu wengi hawajali sana kuhusu ‘customer care’.
Nilifika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupatiwa huduma tena nikiwa na mwenzangu tukaelekea upande wa VIP tukiamini tutapata huduma nzuri na kwa haraka licha ya kuwa gharama zitakuwa kubwa.
Tulipofika hapo tukasajiliwa pekee kisha tukajulishwa madaktari hawapo tunatakiwa kuwasubiri, hiyo ilikuwa ni asubuhi mapema tu muda wa kazi.
Mgojwa ambaye nilikuwa naye hakuwa katika hali nzuri, tulilazimka kumfikisha hapo akiwa katika kiti cha kusukuma wagonjwa, ajabu tukaambiwa tunatakiwa kusubiri Daktari kwa masaa mawili.
Wahudumu tuliowakuta wa VIP wanahuduma Watu kwa mazoea sana, majibu mabaya, hata unapojaribu kuwaambia wakupe maelekezo kwa usahihi wanajibu kama vile tunaomba msaada.
Hali ya mgonjwa wetu ikawa inazidi kuwa mbaya tukiwa palepwale, tukawa tunajiuliza kama sisi VIP tunapata huduma ya aina hiyo, wale wanaolipa kawaida hali ipoje?
Alipofika Daktari na kuona hali ya mgonjwa ilivyo akasangaa kwanini hatujapata huduma wakati wazi Mgonjwa anaonekana yuko vibaya, ikabidi Daktari aanze kulazimisha vitu viende kwa haraka na kutusaidia kuhakikisha tunapata huduma ikiwemo vipimo.
Kibaya zaidi wakati sisi tunafika kuna wagonjwa wengine tuliwakuta hapo wanasubiri, hivyo mpaka Daktari anafika tayari walikuwa wamekaa kwa muda wa Saa tatu wakisubiri huduma.
Huduma zinatolewa kimafungu, ni kama vile watu wanapewa huduma kwa kujuana, na ukumbuke kuwa hapo ni VIP, inavyoonekana yaani kama hujiongezi wewe mwenyewe hupati huduma kwa wakati.
Kiufupi hakuna mawasiliano mazuri kati ya Wahudumu wa hapa na wagonjwa, wahudumu wanahudumia kwa mazoea au watu maarufu, wasio na connection ni tatizo.
Yaani ni tatizo kubwa sana sana, na huruma pia. Kuna mama nilimuona anajigeuza tu yupo hoi, nilipomuuliza akasema ameambiwa Daktari yupo kwenye kikao, awe na Subira, hivi for 3 hours kweli? Kikaoni tu wakati afya za watu zipo tete?
Kingine kibaya, tulipofika hapo upande wa VIP kulikuwa na mhudumu mmoja ambaye muda mwingi yuko bize na mambo yake, kule kwenye registration walikuwepo wawili.
Tulichobaini kuwa kuna ubaguzi ni kuwa kuna Wagonjwa ambao wanapewa Nurse kabisa wa kushughulikia kila kitu then wengine wanajishughulikia wenyewe kushuka chini kuuliza wapi niende na vitu vingine.
Pia Wahudumu wa JKCI tuliowakuta wako too defensive, yaani hawataki wagonjwa wahoji au kuuliza, ukiwauliza wanakuwa wakali na kukuona wewe ni mkorofi.
Ufafanuzi wa JKCI huu hapa ~ JKCI yatoa ufafanuzi madai ya baadhi ya Watumishi wao kutoa huduma kwa kujuana