KERO Tumepata huduma mbovu JKCI upande wa VIP, baadhi ya Watumishi wanahudumia Watu kwa kujuana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mimi veterani wa miaka mitano hapo sasa nikumegee.
Tangu mheshimiwa sana Peter Kisenge akabidhiwe kitengo huduma zimezorota kiasi cha kutisha.
Unafika saa kumi ya usiku Toka nje ya Jiji kutamani update matibabu haraka uwahi usafiri wa kurudi utakaa sii chini ya saa nne kumaliza registration,kumuona Daktari na saa mbili zingine kutoka pharmacy ambapo kwenye computer zao wanacheza games, na Mungu akusaidiwe usiwe na vipimo au kubadilishiwa Daktari
Peter Kisenge mara yupo Zambia mara Comorro,au Kawe siku hayupo kwenye camps alizobuni mikoani kupima BP kitu local docs wanachoweza.
Sasa siku hizi katangaza Wasanii watatibiwa BURE 😡
 
Shida ni nyomi, unafika saa 10 alfajir unakuta we ni mtu wa 70. Hii ya kujiandikisha inasaidia kupunguza upendeleo kwenye kupata huduma.


Hii ya kwenda mikoani imekaa kisiasa zaidi mkuu ama kujitangaza
 
Kabisa vitu vingine vinauma sana. Mtu kang'atwa na joka, sumu inasambaa mwilini kwanini husimpe huduma kwanza halafu mkawadai.
Hizo taaluma wamezipataje? Wanamatumizi mazuri ya ubongo kweli?? Utu huko wapi???
Kama ni hospital ya serikali,dawa na vifaa tiba siyo vyako,unaogopa hasara gani?!
 
Muhimbili yote hilo tatizo lioo sana haswa watu wa dini fulani wanapenda sana hio michongo mchongo anaonaga wanavyo kuwa busy kuhudumiana haswa wakija wale wenye rangi kidogo
Ni kama unaisema Agha khan...Yan akija wa upande wao...anapitiliza moja kwa moja kwa Dr...we utashinda hata siku nzima
 
Ni kama unaisema Agha khan...Yan akija wa upande wao...anapitiliza moja kwa moja kwa Dr...we utashinda hata siku nzima
Nimeona sana pia. Nilienda kwa Dr. Jumaa kutairi mtoto, alikuja mmama muhindi wa kariakoo eti wamempitisha Dr alimuuliza Namba akaanza kujibebisha, Dr. Alimtoa ndani na mwanae wakasubirie zamu yao
 
Nimeona sana pia. Nilienda kwa Dr. Jumaa kutairi mtoto, alikuja mmama muhindi wa kariakoo eti wamempitisha Dr alimuuliza Namba akaanza kujibebisha, Dr. Alimtia nadhani na mwanae wakasubirie zamu yao
Kuna haja kubwa sanaa somo la customer care likawa sehem ya mtaala wetu...Kenya wanatupigia gap hapa kwa huduma zao...wabongo tunaendekeza sanaa tamaa na kukosa weledi kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…