Tumepeleka wapi vichwa vyetu? Hivi ni kweli mchakato wa kuwafukuza uanachama Halima Mdee na wenzake ulikamilika kwa vigezo vyote vya kikatiba?

Ulishajibiwa:Ikiwa umehukumiwa kufungwa na kuna fursa ya kukata rufaa unaachilwa huru au unatumikia adhabu wakati process ya rufaa inaendelea?
Unakuwa umeshahukumiwa- utaratibu ungekuwa sawa unakuwa huru
 
Chambua hiyo katiba ya Chadema na katiba ya nchi inayosema mchakato haujakamilika. Nape sio mjinga hadi aongee vile.Anawanasheria na mtandao wa watu wa kila eneo.

Suala hili alishalimalizaga Mzee Pius Msekwa.
Katiba ndio sheria mama ya nchi lazima ifuatwe
Watu wanaapa kwa kutumia katiba halafu wanaivunja maksudi kwa maslai ya kisiasa
 
Mie sioni tatizo liko wapi- kwa nini hawasikilizwi rufaa yao?
 
Mie sioni tatizo liko wapi- kwa nini hawasikilizwi rufaa yao?
Hujui lolote umejaza ujinga kichwani wewe. Chadema wana utaratibu wao wa kuitisha kikao cha baraza . Hata ccm pia ndo maana mkutano wa ccm ukaitishwa tarehe 30 mwezi huu mbona haujaitishwa baada ya kufa yule mpuuzi JPM?
Huo uharaka unaotaka wewe ni kwa utashi wako wewe.
Je mfungwa akikata rufaa mahakama ya juu huwa anaachiliwa huku rufaa yake ikiwa inasikilizwa?
 
Mkuu inawezekana ila nakushauri usilazimishe mambo na kama unauwezo kawatoe bungeni

 
Maoni ya Mh. Nape juu ya uhalali wa wabunge wa vitu maalumu CHADEMA umenishangaza kidogo kwa sababu mchakato wa kuwafukuza uanachama haujakamilika kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, JMT na Natural law.
Ukifukuzwa sehemu (whether kwa mchakato sahihi au usio sahihi) inabidi uondoke na kama utaona hukutendewa haki unaweza kukata rufaa kwa ngazi ya juu. Huu ndio utaratibu kila sehemu, hata kazini. Hata mahakamani, hukumu ikitolewa, ambayo mhusika ataona siyo ya haki, hatagoma kuitumikia, bali wakati anatumikia hiyo hukumu, atakata rufaa kwa ngazi husika. Sasa hata kwa akina Halima Mdee kama wanaona makosa yalifanyika kwa upande wa chama kwa wao kuapishwa kinyume cha utaratibu wa chama na chama kikachukua hatua, inabidi uamuzi wa chama uheshimiwe na walalamikaji wakate rufaa 'to rectify the wrong and set the records straight'. Full stop!
 
Wewe ndiyo unalazimisha mambo japo sijui una elimu gani inayokufanya kuwa na akili ndogo hivyo? Kwamba kila anayetetea katina wewe kwako ni chadema!
Kwamba pesa za umma inaweza kulipa watu wasiostahili kwa mujibu wa katiba wewe unashangilia ukifikiri unamkomoa mbowe?
Kama nilienda shule basi itakuwa ulikuwa unagelezea kwa wenzio wewe.
Haiwezekani logic ndogo kama hii usielewe!
Mwaka juzi kulikuwa na uchaguzi wa serikali.za mitaa hapa. Watu waliondolewa kwa mambo ya kipuuzi kabisa . Chukulia mfano kungekuwa na wagombea wenye sifa za kina halima na wenzake! Wangeruhusiwa kugombea wakati ule ati KISA rufaa hazijakamilika au wangeenguliwa?
 
Mkuu soma hii halafu uendelee kupinga kwa sababu wewe u mfuasi wa bwana yule

Katiba ya Chadema

Ibara ya 5.4.3 ya katiba ya Chadema inaelezea mchakato wa kukoma uanachama na nafasi ya kukata rufaa kwamba hutokana na “kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya chama kwa mujibu wa katiba, kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo usioendana na itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za chama.

“Mwanachama atakuwa na haki ya kukata rufaa kwa ngazi za juu kama hakuridhika na adhabu hiyo.”

Kwa kuwa wabunge hao walifutiwa uanachama wao na Kamati Kuu, wanatakiwa kukata rufaa Baraza Kuu ambalo kwa mujibu wa ibara ya 7.7.3 (e) ya katiba ya Chadema lina jukumu la “kusikiliza na kutoa uamuzi juu ya rufaa za uchaguzi na kinidhamu kutoka ngazi za chini.”

Endapo Baraza litashikilia msimamo wa Kamati Kuu, akina Mdee bado watakuwa na nafasi ya kukata rufaa katika Mkutano Mkuu ambao kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ibara ya 7.7.10 (f), kazi yake ni pamoja na “kuzingatia na kutoa uamuzi juu ya rufaa na masuala ya kinidhamu yanayowasilishwa na Baraza Kuu.”

Endapo Mkutano Mkuu nao utashikilia uamuzi huo, wabunge hao wanaweza kwenda mahakamani wakitaka.
 
Mkuu achana na Msekwa na Nape- malizeni kwa kuamua rufaa yao ili kieleweke mbona ni rahisi tu.
Ndio maana nikakwambia ubatili ni ubatili tu. Kuna tofauti kubwa kati ya legality na legitimacy. Taratibu guilty conscious inaanza kuwatafuna.

Ukweli ni kwamba temperature imeshaanza kupanda, na hata mwaka 1 hawajamaliza.
Hawata-survive miaka 5 hawa, it's a matter of time tu.
 
Mkuu ebu tuweke kumbukumbu sawa - kule gerezani kuna wafungwa na mahabusu unaelewa tofauti yake?
 
Mkuu napenda nikuhakikishie- mlisema haya haya huko nyuma- watabaki bungeni mpaka pale mtakapo kamilisha mchakato wa kufukuzwa kwao.
 
Mkuu ebu tuweke kumbukumbu sawa - kule gerezani kuna wafungwa na mahabusu unaelewa tofauti yake?
Nenda kwenye point. Achana na wafungwa na mahabusu tutapoteza muda bure.
 
Unakataje Rufaa Kama hujafukuzwa you mutuziii
Kama katiba yao inaruhusu rufani inamaana mchakato bado haujakamilika, na maamuzi ya mwisho hayajafanyika.

Hivyo mpaka hapo Chadema watakapowasikiliza rufani yao na kutoa maamuzi ndipo tutakapojua kuwa wamefukuzwa Rasmi.

Hata hivyo bado wanazo avenues nyingine pia wakiona hawakutendewa haki (refer kesi ya Zito, alibakia mbunge wa mahakama)

Sofar, kinachoendelea ni porojo tu ambazo mwisho wa siku yanayopaswa kufanyika yatafanyika.
 
Nenda kwenye point. Achana na wafungwa na mahabusu tutapoteza muda bure.
Mkuu uko sawa na kwa usawa wako hoja kuu ni kwamba mpaka hapo mchakakto wa kuwafukuza uanachama utakapohitimishwa wale wanawali 19 ni wabunge halali
 
Ulichoingia kukitetea hutaweza
sina cha kutetea - Halima na wenzake wako bungeni watabaki bungeni hadi hapo mtakapohitimisha mchakato wa kuwafukuza. Na wewe na mabawana wale hamna uwezo wa kuwatoa humo bungeni. Mnakerekaje.
 
Mkuu uko sawa na kwa usawa wako hoja kuu ni kwamba mpaka hapo mchakakto wa kuwafukuza uanachama utakapohitimishwa wale wanawali 19 ni wabunge halali
Unapotokea mgogoro juu ya jambo fulani - kunakuwa na mashaka juu ya uhalali au la na ili ijulikane kama ni halali au la inatakiwa wahusika wakate rufaa dhidi ya uamuzi wa chama. Chadema wanadai hao wanachama wao 19 hawakufuata utaratibu wa uteuzi (walijiteua) na inaonekana pia wanaonyesha walishajulisha ofisi ya Spika baada ya kuwa wameapishwa kwamba uwepo wao bungeni hautokani na ridhaa ya chama chao. Na kwa vile na wao wanadai walipitishwa na chama, sisi tunaosikia pande zote mbili tunakuwa na mashaka: 1) ama chama chao kiko sahihi kwa yale kilichofanya au 2) wao wako sahihi kwa kile walichofanya. Kwa vile, kuna upande wa chama na upande wa wale waliofukuzwa na chama, kujua uhalali wa nani yuko sahihi mpaka rufaa yao isikilizwe na uamuzi utolewe na kama upande fulani utaona bado haujaridhika utakata rufaa...hivyo hivyo mpaka uamuzi wa mwisho utakapotolewa.

1) Sasa ni nani yuko sahihi: wale 19 au Chadema? Jibu lake ni hatujui? 2) Je, Chadema kuwafuta uanachama kiko sahihi kwa sababu zilizotolewa? Ndiyo na hapana. Ni ndiyo kama walijiteua na ni hapana kama chama ndicho kilichowateua. 3) Je, chama kuwafuta uanachama umeathiri uanachama ndani ya chama na ndani ya bunge? Ndiyo, kwa sababu chama kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (kama ilivyorekebishwa hadi 2005) inavyosema:

71.-(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake
katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo (NB: mambo mengine sikuyataja hapa) -
(e) ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.

Chadema kuwafukuza uanachama (kimejiondoa kwenye udhamini wao), hivyo wanakosa sifa za kuendelea kuwa wabunge kwa sababu si wanachama wa chocote cha siasa. Na Tanzania hadi siku ya leo hairuhusu mgombea binafsi maana ungeweza kusema wanajidhamini wenyewe. Hapa ndipo penye mzizi wa fitina!
 
Mkuu umeeleza na umeeleza vizuri kabisa. Hapa hoja ni kama mchakato wa kufukuzwa ulihitimishwa inavyotakiwa kikatiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…