Tumepigwa; Hii temporary camp ni sawa kugharimu Tsh milioni 7?

Tumepigwa; Hii temporary camp ni sawa kugharimu Tsh milioni 7?

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
901
Reaction score
1,742
Hivi watendaji wa Awamu hii wanatuonaje Watanzania ? Kuanzia report ya CAG ni Wizi kweupe kabisa hata kama mama sio mkali jamani huu upigaji unapitiliza sanaa
 
Ndiyo inawezekana kwa Engineering ya Tanzania, kwasababu huwa tunajumlisha na Finger Engineering.
 
Hiyo camp ni ya kazi gani, ni site ya ujenzi?

Ila sishangai, hapo ni porini , usafiri peke yake hadi kufika huko mbugani unaweza kuta milioni imeenda, mabati na mbao labda milioni 1 nyingine, ufundi milioni 1, milioni 4 faida ya mkandarasi
 
Hiyo camp ni ya kazi gani, ni site ya ujenzi?

Ila sishangai, hapo ni porini , usafiri peke yake hadi kufika huko mbugani unaweza kuta milioni imeenda, mabati na mbao labda milioni 1 nyingine, ufundi milioni 1, milioni 4 faida ya mkandarasi
Zee la michanganuo
 
Camp ni ya nini kwanza ?

Kabla hata sijaongelea gharama za hio camp kwanza ningependa kujua umuhimu na ulazima wa hio camp ambayo ni temporary.., na utemporary huo ni wa muda gani ?
 
Si maneno yangu "Kila mbuzi ale KWA urefu wa kamba yake"
 
Yule jamaa Ni Kama vile anawachongea wenzio ndio maana hakuwa na hakuogopa alivyo kuwa anatamka Kuna kitu kimefanyika
 
Wote wajinga kuanzia waziri

Hapo paliandaliwa mpango wa ujenzi ambao baadae mshauri atakuja kupima kilichopo site na cha kwenye karatasi kisha pesa inaondolewa ama kupunguzwa kulingana na kilichofanyika

Nchi hii kila waziri anajua na kuhoji
 
Watu hawajui tu, engineering projects sio ungwini.

Watu wakisikia gharama ya kitu wanawaka utadhani hawajaenda shule.

Ingekuwa mchina hapo wangeandika 100m na wasingehoji, mchina angejenga kama Darasa, baadae anawaachia wanakijiji inakuwa ofisi ya kijiji.

Guys temporary office ina mambo mengi sana. Hapo panatakiwa viti, Meza, yaani kila kitu kinachotakiwa ofisini.

Huyo waziri anashangaa wakati posho yake ya kwenda kukagua site, kwa saa moja tu ni mshahara wa mtu mwezi mzima.
Bongo wanafiki ni wengi sana
 
Afadhali sasa hivi wakati wa mama inaonekana kwa uwazi hata kutangazwa. Wakati wa Jiwe matrillion na matrillion hazina zilipigwa ukithubutu kuanika kama hivi unauwawa. Kwa iyo mleta mada unasifia ukali wa Jiwe kunyamazisha watu akiiba matrillion yeye na genge lake?
 
Huyu mtoa taarifa ameshajua anaongea na mtu stupid ndio maana anaongea huo ujinga.
Stupidity is knowing the truth, seeing the truth but still believing the lie.
 
Back
Top Bottom