MpendaNchi1
Member
- Sep 25, 2021
- 7
- 4
Dkt. Samia Suluhu Hassan anaungana na waasisi wa fikra za Uafrika wa bara hili – akina Mwalimu Julius K. Nyerere, Kwame Nkrumah, Kenneth Kaunda, Nelson Mandela na wengine – kwa kuchora taswira ya uzalendo na mshikamano kwa mtazamo mpya unaozingatia mazingira ya sasa. Anaamini katika mikakati ya kibiashara na kidiplomasia inayolenga leo na kesho, huku akisisitiza kuwa kila mmoja, hata adui, anaweza kushirikiana naye kwa manufaa ya taifa, lakini kwa tahadhari na busara.
Hata hivyo, anakosoa wale wanaodai "misingi ya waasisi" bila hata kueleza ni ipi hasa. Historia inatuonyesha kuwa waasisi hawa walikuwa wakijibadilisha kulingana na mazingira ya wakati, lakini daima waliongozwa na misingi ya utu, mshikamano na maendeleo. Mwalimu Nyerere aliwahi kusisitiza: “Utu wa mtu ni msingi wa maendeleo. Hatuwezi kuendeleza vitu bila kuendeleza utu wa watu wetu.”
Misingi ya Uafrika: Utu, Umoja, Kazi na Kujitegemea na Maadili
Kwame Nkrumah aliwahi kusema: “Uhuru wa Ghana hauna maana yoyote endapo hautaunganishwa na ukombozi wa jumla wa Afrika.” Kauli hii inaonesha mshikamano na ushirikiano wa Waafrika wote. Kenneth Kaunda naye alisema: “Ubuntu ndio msingi wa ubinadamu wa Kiafrika. Sisi ni binadamu tu kupitia ubinadamu wa wanadamu wengine.” Nelson Mandela akasisitiza: “Kuwa huru si tu kuvua minyororo yako, bali ni kuishi kwa namna inayoheshimu na kuimarisha uhuru wa wengine.”
Kwa mtazamo huu, Dkt. Samia anasisitiza maendeleo ya Watanzania kwa msingi wa utu, mshikamano na ushirikiano. Hii ndiyo tafsiri halisi ya misingi ya waasisi, siyo mitazamo ya wahafidhina wanaotumia historia kwa maslahi binafsi.
Mfano wa G55 na Busara za Mwalimu
Harakati za kundi la G55 za kutaka kurejesha Tanganyika zilipingwa vikali na Mwalimu Nyerere, kwa sababu nyuma ya hoja hizo kulijificha chuki za kikabila na udini. Kama Mwalimu angekaa kimya, taifa lingeingia katika mgawanyiko hatari usioweza kudhibitika.
Historia ya G55 inatufundisha wazi kuwa udini na ukabila ni sumu kwa mshikamano wa taifa. Nyerere alisimama imara akilinda umoja wa Watanzania bila kujali dini au kabila, na kwa kufanya hivyo aliweka msingi wa ushirikiano wa kitaifa. Huo ndio msingi anaouendeleza Dkt. Samia leo – kuhakikisha taifa linaongozwa kwa mshikamano, ushirikiano na haki kwa wote, kwa kuwa hakuna Muislamu mwenye haki zaidi ya kuongoza kuliko Mkristo, na hakuna Mkristo mwenye haki zaidi ya kuongoza kuliko Muislamu. Mstahiki ni yule mwenye nia ya dhati, uzalendo na mipango thabiti ya maendeleo.
Ukweli Kuhusu Misingi ya Azimio la Arusha
Baadhi ya wahafidhina wanajificha nyuma ya Azimio la Arusha la 1967, wakidai misingi yake imetelekezwa. Lakini ukweli ni kwamba msingi mkuu wa Azimio hilo ulikuwa utu na heshima ya mwanadamu – ambayo ndiyo kauli mbiu ya Dkt. Samia leo. Kujitegemea hakuishii kwenye maneno, bali ni juhudi endelevu za kuandaa miradi mikubwa ya maendeleo, kuwekeza kwenye elimu, afya na miundombinu, huku akihakikisha Watanzania wanashiriki katika uchumi wao. Aidha, kubwa zaidi hatuwezi kujitegemea bila kuwa na vyombo vya ulinzi na usalama vyenye weledi na vya kisasa, kwa kuzingatia hili Dkt. Samia ameviboresha vyombo vyote vya ulinzi na usalama ili kuvitoa kwenye uzamani na kuvifanya viwe vya kisasa vinavyoendana na mabadiliko ya sasa ya ulimwengu.
Mwaka 1992 Watanzania walirejesha mfumo wa vyama vingi licha ya asilimia 80 kuukataa na asilimia 20 tu kuubali. Wazee wa Dar es salaam waliandamana kuunga mkono chama kimoja, lakini Nyerere, kwa busara yake, aliona mazingira ya dunia yamebadilika. Akiwa Mwenyekiti wa CCM, alihakikisha mfumo wa vyama vingi unaanza, na hata kuhimiza kuanzishwa kwa chama pinzani (NCCR Mageuzi) ili kuwatoa wananchi hofu.
Hakulaumiwa kwa kuvunja misingi, bali alihesabiwa busara kwa kusoma nyakati. Hii inadhihirisha kuwa misingi ya waasisi ilikuwa hai na inayoweza kubadilika kwa maslahi ya taifa, si maandiko yaliyogandishwa.
Katika moja ya hotuba zake, Mwalimu alisimulia hadithi ya msafara uliotahadharishwa kutoangalia nyuma.
Aliwaonya: “Mkishaamua jambo lenye maslahi kwa taifa, msigeuke nyuma. Ukigeuka, unakuwa jiwe.” Dkt. Samia analichukua fundisho hili kama msingi wa uongozi wake – hatageuka nyuma kwa kelele za wanaotaka kugawa taifa kwa misingi ya dini na ukabila, wala hatakatishwa tamaa na maneno ya wanaotamani kuona taifa likirudi nyuma.
Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka 1964, chini ya mazungumzo ya Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume. Leo tuna Tanzania moja – Mtanzania Bara ni Mtanzania, Mzanzibari ni Mtanzania, Muislamu ni Mtanzania, Mkristo ni Mtanzania. Hakuna mwenye haki ya kipekee ya kuongoza taifa hili. Wala si M'bara zaidi anayestahiki kuongoza Jamhuri ya Muungano, kuliko Mzanzibari. Waasisi waliunganisha nchi njema ya Umoja, utu na mshikamano wa Utaifa, si upande mmoja kujiona una haki zaidi ya kuongoza katika Muungano huo.Kigezo pekee kinachohitajika ni uzalendo, uadilifu, na nia ya dhati ya kuliletea taifa maendeleo ya watu na vitu.
Wazee wahafidhina wasijaribu kulaghai vizazi vipya kwa kueneza hofu na udanganyifu. Historia inaonyesha kuwa kila kiongozi aliyechukua madaraka alibadilisha mwelekeo kulingana na mazingira ya nyakati. Mwalimu hakusimama kama sanamu; alibadilika kadri dunia ilivyobadilika. Hali kadhalika, Dkt. Samia Suluhu Hassan anasimama juu ya misingi hiyo, lakini kwa tafsiri ya karne hii ya ishirini na moja.
Kwa maneno ya Mandela: “Historia itatuhukumu kwa tofauti tunayoiweka katika maisha ya kila siku ya Watoto.” Historia itamhukumu Dkt. Samia kwa kazi anayofanya leo kuboresha maisha ya Watanzania, na kwa hakika wengi wanamuelewa.
Wale wachache wanaokerwa na mafanikio yake walidhani angesalimu amri, lakini wameshuhudia nguvu na ujasiri wake.Dkt Samia, amebadilisha historia za hekaya zilizoonyesha majirani wako juu kiuchumi na maendeleo, sasa Tanzania imeshika usukani Afrika Mashariki na kutabiriwa kupaa zaidi kimaendeleo na kiuchumi. Na hilo ndilo hitajio la Watanzania.
Dkt. Samia shikilia hapo hapo – usigeuke jiwe. Umeandika ukurasa mpya katika historia ya Taifa.