TUMERUDI PALE PALE HAKUNA MABADILIKO, BARRICK KIBOKO

TUMERUDI PALE PALE HAKUNA MABADILIKO, BARRICK KIBOKO

Labda tulisikia vibaya kile ambacho TRA walisema, haikuwa 400 BILLIONI kweli!?? Bahati mbaya TRA hawako 'verified' hapa kama TCRA, TPA, DAWASCO nk. Wangekuwepo tungewuliza wakatupa mrejesho labda!

Mimi kwa Trillion 400 nilikuwa nasubiri mazungumzo yaishe nipate Noah yangu sasa sielewi hii 600 billion kama tutaambulia japo baiskeli ya Swala!

Hakyanani kama mambo yakiwa hivi naenda mahakamani kuyashitaki magazeti na TRA yaliyotuaminisha umiliki wa Noah, sasa nimeshaingia gharama kutengeneza kibarabara cha kuelekea kwetu alafu uniambie 600b pesa isiyofikia hata mishahara ya mwezi kwa watumishi wa umma!!

TRA cheap politician
 
Pesa walioitoa ni kuonyesha uaminifu wao, mazungumzo upande huo wa ukwepaji kodi yalikua magumu Sana, ukizingatia matukio yamefanyika kwa miaka 17.
Watanzania tuache unafiki, cha msingi tumewagusa na sheria na mashariti mapya wameyakubali, hilo ndo muhimu na Rais Magufuli anastahili pongezi kwenye eneo hili.
Mengine ni unaa tu wa wale wapendao Magufuli ashindwe, dua hizo hazitafanikiwa hata Kidogo kwani yupo na Watanzania wengi sambamba nae
 
Hao waliopita awamu nyingine mbona walikuwa wazuri sana wa hiyo lugha na ndo wakatuingiza kwenye huu mkwamo wa sasa? huyu hata kama hajui angalau tumepata hapo bilioni 700 na kuanzia sasa kitakachopatikana ni mara dufu ya kilichokuwa kinafichwa kutokana na sheria mbovu.. kubalini basi hata kwa kidogo kinachofanyika..
 
Hao waliopita awamu nyingine mbona walikuwa wazuri sana wa hiyo lugha na ndo wakatuingiza kwenye huu mkwamo wa sasa? huyu hata kama hajui angalau tumepata hapo bilioni 700 na kuanzia sasa kitakachopatikana ni mara dufu ya kilichokuwa kinafichwa kutokana na sheria mbovu.. kubalini basi hata kwa kidogo kinachofanyika..

sawa, tumetumia bei gani kufika hapo. madhara gani ya direct na indirect tunapata? sorry nielimishe
 
Tunapowalazimisha kugawana faida 50%, wakisema tumepata hasara mwaka huu, na hiyo hasara nayo tutagawana 50% ?

Au tunataka kugawana faida tu?
 
sawa, tumetumia bei gani kufika hapo. madhara gani ya direct na indirect tunapata? sorry nielimishe
Sidhani kama ni sahihi kuangalia bei tuliyoitumia kufika hapo... hata wao wamekaa miezi mitatu hotelini wakifanya haya mazungumzo.. unaongelea biashara itakayoendelea nchini kwa miaka mingi ijayo,hata mzee wa Msoga alisema ukitaka kula lazma uliwe
 
wakifanya hivyo naenda kuchukua kadi ya ccm, ntatoka huku kwetu natembea kwa mguu hadi dar kumpongeza rais
Wewe tembea kwa miguu na kachukue kadi, hakutakua na tofauti na nilichokwambia, na Kumbuka majadiliano yanaendelea, cha kwao ni dhahabu tu, madini mengine yote ni ya kwetu.
 
Njia zipo nyingi kituo kimoja wamebadili Njia upigaji pale pale hawawezi kukubali hasara wao na hiyo 50 50 michanga ya macho tu haiwezekani
 
Napingana na wooote wanaobeza jitihada za Rais kwa milengo ya kisiasa.Tunashukuru hata hizo m700,,,wanafiki hawajui hata hizo zilikua zinapotea.Asante baba
 
50/50 si lolote si chochote kwenye kampuni ambayo iko listed as public company.
Jambo la kwanza linalozingatiwa ni kugawa dividends kwa wana hisa...kwa Acacia wapo wengi ...wadogo wadogo na wakubwa
Baada ya kugawana dividend inabaki amount ambayo inakatwa kodi na then itayo baki ndiohio 50/50
Na hapa pia tutarajie loss , yaani hasara hivo sijui fomula tutagawana hasara ama vipo.
Tusubiri Acacia watoe statement yao
 
Back
Top Bottom