Watumishi Halmashauri ya Wilaya Korogwe Vijijini tunagomewa kupewa vibali vya Uhamisho na Mkurugenzi ilihali tumefika vigezo vya zaidi ya miaka mitatu kazini, wengine tuna hadi vyeti vya ndoa.
Wanaoweza kuongea nao vzuri wanapewa datasheet ila wengine hawapatiwi taarifa za datasheet ila wahame.
Yaani ni kama wanachaguana kwa kujuana kama mtu hawakuelewi hawakusainii wanakwambia baki kituoni kwako.