NGULI
JF-Expert Member
- Mar 31, 2008
- 4,801
- 643
Tumetoka mbali hasa tulianza shule miaka ya 1970s!
Enzi zetu barua kama hii ilikuwa ukishaiandika, unatafuta nafasi ya umdhamiliae awe peke yake ili uweze kumkabidhi, kwa hiyo waweza kukaa nayo kwenye mfuko wa madaftari hata week nzima.
Na je utampatiaje hiyo barua?
Akishakuwa peke unachokifanya ni kumrushia usoni, halafu huyoo unatimua mbio. Ukifika mbele kidogo unachungulia kama anaisoma.
Utajuaje kama amekukubali?
Ukiona anasoma halafu anatabasamu, ujue tayari .
Zawadi gani dada zetu walipendelea zaidi?
Ni kumnunulia mafuta ya Lady Gay au Yolanda (kama uko safi) au kandambili , hapo atakuona kweli unamjali.
Na je akionekana kutokukubalia?
Hapa sasa haangalii kama kuna wanafunzi gani, atakuporomoshea mitusi hiyo, utazomewa na shule hutahudhuria kwa week nzima.