kennyshuaka
New Member
- Jul 28, 2023
- 2
- 2
Nimekuwa nikijiuliza haya maswali muda mrefu mimi kama Mtanzania nisiweze kuyapatia majibu thabiti kutokana na kuona jinsi hali ya mazingira yaliyotuzunguka yalivyo ni kutokana na ongezeko kubwa la watanzania waliokata tamaa na kuona maisha magumu na kuchukuia maisha na kuona pengine hawapo katika ardhi sahihi iliyowapasa kuwepo, mpaka wengine kuacha kuacha kutengeneza hapa na kwenda kutengeneza ugaibuni kwasababu ya fikra ya kutokuthamini ardhi.
Lakini tukipasahau tulipotoka tutafikaje tunako kwenda?
Ubinafsi na kujipendelea mwenyewe na kusahau umuhimu wa mwananchi mwenzako au umuhimu wa jirani yako au umuhimu wa mwananchi wako kwa kushindwa kujiuliza mbona aliyenipa mimi Uhai kampa na huyu au yule hivi imetuondolea utu kabisa na nchi kubaki yenye amani lakini wananchi wasio na amani thabiti mioyoni mwao ila kila mmoja wetu akiambatana na utu tutajenga daraja la amani thabiti kati ya mwananchi na mwananchi pia tutajenga daraja la amani thabiti baina ya kiongozi na mwananchi kwasababu kiongozi akiwa na utu ataongoza kwa haki na atatekeleza aliyoahidi kwa moyo mnyoofu hivyo maendeleo yatabadilika kwa kasi kwa kuwa kiongozi atathamini familia ya mnyonge kama anavyothamini yake hivyo mabadiliko yatakuwepo kwasababu kiongozi hatofanya yale ambayo asingependa kufanyanyiwa yeye kama angekuwa mwananchi.
Lakini kiongozi akikosa utu atafanya maovu na kujipendelea kutafuatia ndivyo itakavyo kuwa hata baina ya anaowaongoza yani wananchi na kupelekea wananchi kufanyiana maovu vivyo hivyo kujitenga na kujipendelea kunafuatia halafu tunakosa jamii komavu inayoweza kupambana na changamoto zinazotuzunguka hivyo kumbe kiongozi asipofanya maovu na kuongoza kwa utu kutapelekea wananchi pia kuishi bila ya kutokea kwa maovu na watu kuishi kwa kufurahia kuwa wananchi na pamoja kuheshimiana patakuwa sehemu ya matendo yetu ya kila siku na hii itatupelekea kufahamu sisi ni wakina nani na kufahamu asilia yetu na kushikamana kwa pamoja.
Hivyo kumbe inatupasa kuheshimiana baina ya mwananchi na mwananchi pia baina ya kiongozi na mwananchi lakini sio utu kiongozi kumuheshimu mwananchi kwa kuangalia cheo, thamani aliyonayo au kutokana na utajiri alionao bali amuheshimu kwa jinsi alivyo kwasababu sisi wote ni wa tanzania.
Tupo kwenye ardhi Mwenyezi Mungu aliyotubariki kwa kila ya aina ya uzuri hivyo matarajio yake ni kila anaeishi hapa aweze kufaidi utajiri huu tuliopewa na Mwenyezi Mungu na sio utajiri huu tuliobarikiwa uwe mtamu na wenye manufaa kwa wachache wakati kwa wale wengi Umekua mchungu na mzigo mkubwa. Ubinafsi umekuwa utamaduni wetu na hii inaonesha ni kwakiasi gani umeota mizizi katika mioyo yetu.
Ubinafsi umepelekea wale wachache kujibinafsisha utajiri huu tuliobarikiwa wote na Mwenyezi Mungu mpaka sehemu hii kubaki jina la utajiri ila waishio ni maskini.
Ubinafsi unazaa chuki ndipo kuchukia wengine na kujipendelea mwenyewe kuna kuja ndipo kujiona mkuu na mwenye thamani kushinda wengine ndipo akili ya kufanya uovu inakujaa na kuanza kuishi kwa fahari kupitia jasho la wengine.
Hapa ndipo tulipo Swali ni kwamba je hapa tulipo ndipo tunapostahili kuwepo? Au ndipo tulipo staili kufika wakati misingi ya nchi hii inawekwa? Jibu ni Hapana kwasababu hatujui thamani ya hapa tulipo ndio maana hatuipi aridhi hii thamani inayostahili.
Hapa ndipo tulipo ubinafsi na kujipendelea mwenyewe umetufanikisha kuweza kuwatengeneza ndugu na rafiki wa karibu mazingira rafiki yanayowasaidia kukamilisha ndoto zao kiurahisi na kusahau kutengeneza mazingira rakifi kwa kila anaeishi kwenye ardhi na wengine kubaki wakiteseka na kuyakatia tamaa maisha.
Hapa ndipo tulipo uwezekano wa kila familia kuwa tajiri na kutokuwa na familia itakayo lala njaa upo na wote kuweza kufurahia huu utajiri tuliopewa na Mwenyezi Mungu. Lakini kutokujua na kushindwa kuthamini hapa tulipo na kusahau tulipo toka ni vigumu sana kufika tunako kwenda.
Tutafikaje tunakokwenda wakati maisha ya kila mwananchi yanaendeshwa na historia na hadithi tulizoaminishwa na wale wakoloni ili waweze kutawala maisha yetu yote mpaka kutuminisha juu ya kuona mafanikio ni magumu na kuona tulivyo navyo havina thamani ila kwao vinathamani mpaka wakaweza kutuaminisha asili yetu ni sokwe mbona hakuna sokwe mweupe ila yote ni kutaka kututawala kifikra ili tuone hatuna thamani na wamefanikisha kutawala fikra zetu mpaka sasa.
Nakuona hatuwezi kuendesha maisha yetu bila usaidizi wao ila yote walituandaa kwanzia mwanzo lakini utajuaje ukweli wa mawazo ya mtu kama usipotafakari kama yeye? Fikiria wewe ni mmoja ya walioketi katika meza moja kule Berlin mkigawana bara la Africa kuwa mali yenu na huku siyo yenu ungefanikishaje kuja kuichukua afrika ya mashariki kuwa mali yako kumbuka na huku siyo yako ungeandaa mipango gani mpaka mali ambayo siyo yako kuwa yako na sisi tukubali ututawale fikiria tu.
Ila kwa maoni yangu lazima unge tubadilishia uhalisia wa mambo kwanzia kwenye historia zetu na kutuficha ukweli na uhalisia wa maisha ili tusiweze kujitambua ili tukuogope tukuabudu ili uwe mtu wa mwisho kututolea maamuzi namna ya kuishi ili tuishi kulingana na matakwa yako katika maisha yetu yote hata kama sisi hatuitaji kuishi kama unavyo hitaji.
Hivyo ndivyo mipango yako itakavyo kuwa kwetu. Mpaka sasa tunakubali na kuhisi unatusaidia kwa upendo tu na wewe umetuaminisha toka kitambo unatusaidia kwa upendo. Kumbe tupo kwenye usingizi wa giza totoro tulilo tengenezewa na wale wakoloni waliotutawala andiko hili liwashe mwanga katika fikra zetu na kupanda mbegu ya uzalendo na utambuzi wa thamani yetu kama watanzania tukitambua thamani yetu tutaweza kutambua thamani za kila Mtanzania mwenzetu ndipo tutajua thamani ya hapa tulipo na tunapokwenda nakufahamu thamani ya tulipo toka ndipo tutapata maana ya maisha yetu na umuhimu wake.ila hatufiki tunapokwenda kwasababu tumejiona tunathamani kuzidi wengine mpaka kuzalisha chuki, ubinafsi na matabaka.
Pia atufiki tunapokwenda kwasabu hatujui thamani ya tulivyonavyo na kuvipa thamani vitu vingine ambavyo vinaharibu na kupoteza thamani ya hapa tulipo hadi kuonekana kama sehemu yenye idadi kubwa ya matukio maovu na wingi wa mateso kwa wanyonge na umaskini kuongezeka. Tutafikaje tunapokwenda wakati hatujui thamani ya hapa na hatuambiwi zaidi ya kujifunza mambo ya nje ambayo hayasaidi katika kuleta maendeleo ya mazingira yaliyo tuzunguka.
Wananchi tunahitaji kuishi hapa na kujisikia tuko nyumbani na kuhisi tunahitajika katika ujenzi wa nchi yetu wote lakini ukijeruhi jicho machozi yatatoka pia ukijeruhi moyo utaondoa urafiki na ukiwatupia ndege jiwe utawafukuza na ukimkaripia rafiki atavunja urafiki.
0768785385

Upvote
1