Tumeunda kikundi cha biashara lakini watu wengine hawatoi support

trigger468

New Member
Joined
Apr 28, 2018
Posts
2
Reaction score
1
Ni muda mrefu sasa tukiwa wanne ndani ya hit kazi....mtu mmoja tu ndiye anayeshughulika na mambo yote. Wengine wanakaa wakisubiri mambo yakae vizuri bila kuchangia kivyovyote na kusema bado ni wanachama wa kikundi hichi. Mimi naona kama hawapo serious na hawana malengo na hasira kama niliyonayo mimi. Nimeamua kuachana nao japo walikuwa ni rafiki zangu sana kabla ya kufanya kazi hii.

Naomba mawazo menu jamani...
 
Ni mara chache sana kuanza kitu kwa kikundi mkatoboa sababu ya uasili wa binadamu
 
Kama wewe ndiye uliyekuwa unafanya yote hayo na wao kukaa tu kusubiri matokeo then una haki na unaweza kuendeleza biashara yako bila wao kuwepo.

Wabongo wengi ni wavivu na huwa wanasubiri pale utakapoteleza kidogo waanze kukutuhumu,majungu tu na hakika kama mtu umeweza kumbeba ktk kikundi na akashindikana huyo siyo wa kuendelea kuwa naye kibiashara atakuja siku akutie loss
 
ukiendelea kuwavuta kwa kutumia ushawishi wako Ndo unavyokarbisha zaidi kukunjana mashati na kupotea kwa uhusiano zaidi!! unacho kiwaza wewe sicho wanachowaza wenzio!! Ndo maana wanakua wazito kutoa support
Ushauri :Fanya kile Nafsi yako inakusukuma kufanya Jambo Hilo ukiwa Kama wewe
kufanikiwa kwa jambo Hilo ndo yatakua Majibu kwao!!
 
Ni kwel kabisaaaa[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Vikundi wanaweza Sana Kenya. Kule wana SACCOS kwa kiwango cha juuu kabisa na zina mitaji kuliko hata baadhi ya Benki zetu huku.

Watanzania wewe waambie kikundi cha kukutana kupiga story za Mipira ya Ulaya hapo utawaona kwa wingi.

Kwenye Vikundi vya Uzalishaji huwezi waona.

Na hii inasababishwa sana na watu wengi kuwa na Plan B.

Mtu anajua mwisho wa mwezi account itasoma so ya nini nihangaike?

Ila amini wasingekuwa na hizo Backup wange toa sapoti
 
Ni ngumu kufanikisha kama mnatoka location tofauti ,, labda kama wote mpo eneo moja yaani wewe upo DAR mwingine kigoma afu unataka muunde kikundi au mkutane kwa kikao itawezekanaje!
 
Kwani kikundi chenu kinajishughulisha na nini na wote mko mkoa mmoja?
 
Kweli kabisa akili zetu tunazijua wenyewe wa tz
Tunachosahau kuna baadhi ya vitu huwezi Fanya ukiwa peke yako

Tuendelee kuwaelimisha wanajamii kwamba mafanikio y'a mtu yanaanzia kwenye kujali muda, hapa kijijini ninapoishi watu wanaamka saa Moja asubuhi wanaenda Kwenye vijiwe vya kahawa wanapiga story Za uongo na kweli had saa Tatu wanatoka na kwenda shambani saa tano wanarudi nyumbani. Inasikitisha Sana nimeamua kuanza kuwaambia ukweli kwamba kuepuka umaskini ni ndoto Kwa mtindo huu.Natamani kuiona Tanzania iliyobadilika
 
Utagombana na watu mkuu! [emoji13]
 
Mkuu labda hawaoni future ya kikundi hicho tena. hamkujipamga vzr.
 
Ni muhimu kuwa na makubaliano na kuspecify rights na duties kabla kikundi hakijaanzishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…