Tumeuza uhai tunazawadiwa wafu

Tumeuza uhai tunazawadiwa wafu

Na bado, siku hizi CHAWA wanasifia hadi ushuzi wa mama
20241025_032350.jpg
 
Mfano wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mchonga meno bado unaishi.. Ni ule mfano wa kugawa madini ya thamani ya Almasi na kubadilishana na kipande cha chupa na kujiona mjanja sana
Post isiwe ndefu sana
Tunagawa maliasili zetu kwa wageni kwa bei ya kutupa
Tunagawa bandari zetu zote
Tunagawa miundombinu getu yote
Tunagawa madini getu yote
Tunagawa ardhi yetu
Tunagawa sehemu za bahari
mito na maziwa
Tunagawa vitalu na vyanzo vya gesi nknk
Hawa wote tunaowagaia wana tabasamu pana usoni lakini rohoni ni wanyama wa kutisha

Hivi vyote tunavyogawa kwa bei chee ni sawa na kugawa uhai wetu.. Achilia mbali uhuru.. Uhai una thamani kubwa.. Na uhai haushuki bei
Maliasili zote, vitalu vyote na kila nilichotaja hakuna kinachoshuka thamani hata siku MOJA na vyote vimebeba uhai endelevu
Sasa hawa tuliowagaia wanatupa nini!? Tunapewa
Vitu vitu visivyo na uhai tupu...! Misaada mfu.. Zawadi mfu.. Vitu ambavyo haviongezeki thamani bali vinashuka thamani tangu siku ya kwanza..
Tunadhani tunapendwa sana.. Tunadhani ni ukwasi.. Kumbe tunachekwa na kuzomewa kwa nyuma
Tunajaziwa machuma yaliyopakwa rangi na kutiwa nakshi mbalimbali
Tunabandikiwa picha zetu mpaka kwenye matambara.. Kila kitu, kila tukio, kila kusanyiko ni mapambio ya picha zetu na majina

Badala ya kuwa raha sasa ni karaha
Badala ya kuwa shangwe sasa ni chukizo
Badala ya kuwa pambo sasa ni uchafu

Mnyange anayejiamini huwa na mapambo machache.. Mnyange asiyejiamini hujipodoa mpaka anachukiza na kutisha...
Tumeuza uhai... Tukazawadiwa wafu..!
Mfano wa Mchonga bado unaishi...View attachment 3131709

Tanganyika...!
Acha kuliza watu mkuu.
Huku watu wameangua vilio walipojua tayari uhai wao upo mikononi mwa wageni.
 
Hivi vyote tunavyogawa kwa bei chee ni sawa na kugawa uhai wetu.. Achilia mbali uhuru.. Uhai una thamani kubwa.. Na uhai haushuki bei
[/QUOT]
Nimejaribu sana kulielezea hili mara kadhaa humu JF, kwa lugha tofauti bila ya mafanikio yoyote.
Ngoja nione kama lugha yako hii itakuwa na mafanikio juu ya kuwaelewesha watu anayo fanya sasa hivi Samia.

Nita yaazima maneno haya mahsusi: "kugawa uhai wetu; uhuru, uhai". "Uhai haushuki bei."
 
Acha kuliza watu mkuu.
Huku watu wameangua vilio walipojua tayari uhai wao upo mikononi mwa wageni.
Unasema kweli mkuu 'NGOSWE2'?
Wapi huko "watu walipo angua vilio walipojua tayari uhai wao upo mikononi mwa wageni."?
Nami ninge penda kwenda huko kuungana na hao waTanzania wenzangu katika maombolezo ya hali ya nchi yetu.
 
Unasema kweli mkuu 'NGOSWE2'?
Wapi huko "watu walipo angua vilio walipojua tayari uhai wao upo mikononi mwa wageni."?
Nami ninge penda kwenda huko kuungana na hao waTanzania wenzangu katika maombolezo ya hali ya nchi yetu.
Acha mkuu! Ni msiba mzito, 😭😭😭
 
CCM: Wamehonga migodi na misitu kwa Wachina.
Wachina: Wamerejesha fadhila kwa maccm kwa kuwatolea mindula ya kampeni.

Wananchi: Njaa kali.!
IMG_0235.jpeg
 
Tunapofunga vituo vya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Taifa limeendelea kushuhudia tena ubaradhuli wa wazi na wa aibu toka kwa mamlaka zote za Serikali kushirikiana kuipatia CCM na wagombea wake ushindi wa aibu hata kwa gharama za maisha ya Watanzania.

Tunalaani mauaji na kujeruhiwa kwa wagombea, viongozi na wanachama wetu mbalimbali wakiwemo:

1) Steven Chalamila wa Jimbo la Tunduma aliyevamiwa na kukatwakatwa mapanga kikatili hadi umauti kumkuta.
2) Modestus Timbisimilwa, Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Serikali ya Mtaa wa Ulongoni A, Kata ya Gongolamboto, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam aliyeuwawa na askari kwa kupigwa risasi wakati wa purukushani za kuzuia kura bandia na batili kuingizwa kituo cha kupiga kura.
3)George Juma Mohammed wa Kitongoji cha Stand Kata ya Mkwese Jimbo la Manyoni Mkoani Singida aliyevamiwa nyumbani kwake na watu waliofahamika kuwa askari na kumpiga risasi iliyomsababishia umauti.

Aidha, tuna taarifa kadhaa za kujeruhiwa na kukamatwa na Polisi viongozi, wagombea, wanachama na wapenzi wetu maeneo mbalimbali ya nchi walipokuwa wakijitahidi kukamata na kuzuia kuingizwa vituoni kura bandia na batili zilizopigwa tayari kuwabeba wagombea wa CCM.

Tunataka watu wetu hawa waachiwe haraka na bila masharti yeyote.

Tunaendelea kuwasiliana na Chama kitatoa tamko rasmi zoezi hili likikamilika.

Tunaamini kinachofanyika kina maagizo na baraka zote za @SuluhuSamia na Serikali yake na au nchi iko kwenye "autopilot" na yeyote katika eneo lake ana mamlaka ya kunajisi uchaguzi anavyotaka kwani tayari wamepewa kinga na Kanuni ya 49 ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa inayosema, nanukuu:

"Msimamizi wa Uchaguzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Msimamizi wa Kituo, Wajumbe wa Kamati ya Rufani au mtumishi yeyote wa Umma aliyehusika na usimamizi wa uchaguzi hatowajibika kwa Jinai au Madai au kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu au za kiutawala kwa jambo lolote alilolifanya au kuacha kulifanya kwa nia njema wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Kanuni hizi". Mwisho wa kunukuu.

Hakika Taifa lina Msiba mwingine!!
 
Back
Top Bottom