Tumewachoka kwa wizi wenu wa hila

Tumewachoka kwa wizi wenu wa hila

Joined
Jul 6, 2024
Posts
97
Reaction score
72
Diwani aliyepata cheo kwa kuziendea kinyume ilani, katiba, kanuni, miongozo na taratibu, nataka atoke hadharani akanushe. Naomba machawa mwambieni.

Diwani feki feki atoke hadharani, ahimize watu kufuata sheria, kisha nimpatie vidonge stahiki vya kumeza.

Diwani, toka hadharani ukanushe wewe na madiwani wengine wengi walio kinyume na sheria, wenye kutumia uelewa mdogo wa mtu mweusi kumdhulumu kama mkoloni alivyofanya. Watoke wakanushe hadharani, au kama vipi, warudishe mafao waliyolipwa yatokanayo na kodi za mafukara walio wengi, washinda na njaa ambao wamewakosesha uwakilishi wa kihalali kwa tamaa zao za kula mihela wakiwa wamevaa ngozi ya mwanakondoo huku wakiwa na roho za mbwa mwitu.

Tumewachoka kwa wizi wenu wa hila, msiosoma mapato na matumizi. Wezi mvaao vizuri, mkiitwa waheshimiwa huku mkiwa hamstahili kuitwa waheshimiwa.

Nikashtuka katika ulimwengu wa kiroho, huko ndotoni, nikiwa kimya.
 
Back
Top Bottom