Tumewekeza kwenye Arts (Sanaa) tukasahau Sayansi

Tumewekeza kwenye Arts (Sanaa) tukasahau Sayansi

Shytown

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2025
Posts
1,196
Reaction score
2,236
Maendeleo ya Nchi yoyote duniani huletwa na uwekezaji kwenye Hesabu na Sayansi.

kwa sababu zisizo eleweka, Nchii hii imewekeza vikubwa kwenye Arts badala ya sayansi; na hii ni kwa takriban miaka 30 hivyo kizazi kilichojaa mtaani kwa kiasi kikubwa ni cha arts.

Kimsingi mtu hawezi kufanya biashara vizuri na kulipa kodi bila shida, kurejesha mikopo, vikoba nk wakati hesabu ya darasa la saba ya Kujumlisha, kutoa na Asilimia, kapata sifuri.

Bila maboresho makubwa kwenye Hesabu na Sayansi kwa kuanza na kuajiri waalimu wa kutosha kuanzia shule za MSINGI na kuendelea; mabadiliko yoyote kwenye Mfumo wa Elimu, hayataweza kuleta tija iliyokusudiwa.

Nilisoma mahala kuwa, kwa Nchi kama Iran inayofanya vizuri sana kwenye uchumi na Sayansi; mfumo wao wa Elimu ni "STEM" yaani; Science, Technology, Engineering & Mathematics.
 
Back
Top Bottom