Tumeyashinda mabepari, tumeyashinda mabeberu, tumewashinda vibaraka wao Tundu Lissu, Zitto Kabwe na Robert Amstaderm

Hawa mabeberu ndiyo walitupatua nchi mwaka 1961... Na bado tunaendelea kupata misaada kutoka kwao... Walijenga reli ya kati, bandari ya Daslamu, Tanga, n.k....

Na bado tutaendelea kuwahitaji hawa watu....
 
Ujinga umekuzidi.
 
Uzuri ni kwamba umeweka namba ya simu. Who knows pengine ukaonwa!!
 
Tumia akili, kukaribisha mila na desturi za nje zisizo kua za kwetu zinaitwa demokrasia nibkujichimbia kaburi

Kigezo cha demokrasia ndicho kilicho iharibu Libya na leo hii wanajuta kisha yule aliyewahubiria neno demokrasia kakaa pembeni anawatazama wakizama kwenye bahari wakiwa wanakimbia aridhi yao kuwafuata wao huko ulaya

CCM na mapungufu yake kadhaa lakini ndiyo bado ni chama chenye watu wanaoweza kuongoza nchi kwa weredi mkubwa na kusababisha amani kwa wananchi

Tundu Lisu alitumwa na sasa amerudi kulipwa mshahara wa walicho mtuma huku wakimsuka tena kwa baadae kama watafanikiwa,wao wana pesa nyingi zisizo na kazi watamuweka na kumlea kwa malengo na hata wakimsaidia akachukua nchi siku moja kama alivyokua Ghadafi baada ya kuona nia yao mbaya aliwageuka na uchungu wa waafrika wenzie ukamuingia akawagomea kuchukua mali za waLibya wakapanga njama za neno demokrasia na wakamuu Ghadafi

Hiyo ndiyo mbinu inayotumika kwa Tundu Lisu na ninaamini WATAKWAMA.
 
Ka nchi masikini kama haka ndo kanaweza kuwashinda mabeberu?

Kuondoka kwa Lissu tu ni ushahidi mwingine kuwa hatuna ubavu wa kuwazuia wanachotaka.
Hama na wewe ondoka utupishe..uko humu kutafuta nini
 
Tumekupata kibaraka wa watawala, hangaikia tu teuzi mkuu maisha magumu sana
 

Ujamaa na Kujitegemea ndani ya Uhuru, Umoja na sasa Haki ndo walioyaona WAASISI wa nchi yetu. Now, bado hatujitegemei na dalili za upuuzi za tawala MBOFUMBOFU bila checks n balances haambiwi KIZIWI atazame!

Yote haya toka enzi zile na sasa dunia hii ilipo. Wengine walijipanga tangu 1492 AD na yatokanayo. Kwetu sisi ukipata nafasi ya usafiri wa MV LIEMBA utabaini vijiji utakavyoviona kando ya ziwa viko vilevile tangu zama zilee. Muendelezo wa noble savagery, poverty? Iko dynamics za maingiliano ya kiutamaduni na ndani yake "inevitables" zimo.

Kwamba TAL ni KIBARAKA na sio vinginevyo basi tupe VIELELEZO na sio simulizi za kina WAMIREMBE.
Kama haujui uzito wa kosa la KIHAINI tafuta maana yake. TAL asingekanyaga TZ bila kukamatwa. High treason?

Mwishoni, nakuuliza wewe ni tangu lini MTAZAMO tofauti na "status quo" ukawa ni KOSA?
 

1. Mabeberu ni wakoloni mamboleo - kwa maana ya kutawala kiuchumi.

2. Wanatumia upinzani kupitia kinachoitwa demokrasia ya vyama vingi kumbe ni kanuni ya "wagawe watawalike" (Divide and Rule principle).

3. Hekima ilitumika kuepusha vurugu zisizo na tija nchini na hata huyo kibaraka kaingia na kurudi alikotoka pasipo kughasiwa.
 
Nashukuru kwa kunijibu ndugu.

1. Hao wakoloni mambo leo ni kikundi cha watu? Ni sekta fulani? Au ni serikali za nchi fulani ambazo zinawawakilishi nchini mwetu, tunaowaita washirika wa maendeleo? Nina jaribu kupata mantiki ya matumizi ya jina hili la mabeberu ukilinganisha na majina kama nchi washirika au marafiki wa maendeleo. Mpaka sasa ninaona jina hili la 'mabeberu' huibuka ikiwa wawakilishi/wananchi wa nchi za Ulaya au Marekani wakitoa ushauri, wakishirikisha vyama vya upinzani, au wakitetea wanaharakati; ilihali hao hao huitwa "wadau wa maendeleo" au "washirika wa maendeleo" wakitoa misaada, mikopo au kupongeza serikali. Hapa ndipo ninapopata mkanganyiko.

2. Kwa hiyo unamaanisha kuwa utawala chini ya chama kimoja ndio bora kuliko vyama vingi? Tumeanza demokrasia ya vyama vingi Tanzania miaka ya '90, na kabla ya hapo tulikuwa na utawala wa chama kimoja. Kwa nini tulibadili Katiba kuruhusu demokrasia ya vyama vingi ikiwa chama kimoja kinatosha? Najaribu kuelewa wanatumiaje "wapinzani" kugawa nchi. Kivipi? Kwamba wapinzani wakiongea watu watagoma kutoa kodi? Kwamba miundo mbinu haitajengwa? Au watu wakitoa mawazo mbadala serikali haitaweza kuendesha nchi na hivyo "mabeberu watafaidika"?

3. Ni vizuri kama Serikali inatumia hekima ila kama kuna ushahidi kuwa Lissu ana uraia wa nchi nyingine, kwa nini huu ushahidi usiwekwe wazi? Unaposema kuwa hakughasiwa tangu aliporudi, mpaka alipoondoka una maanisha kuna namna nyingine alitakiwa afanyiwe? Maana inatakiwa iwe kawida kuwa mtanzania akirudi nchini kwake aendelee na shughuli zake bila kughasiwa kwa mujibu wa sheria. Ikiwa amevunja sheria basi afikishwe kwenye vyombo vya sheria kwa mujibu wa sheria. Nadhani pia hata kukamatwa nje ya Umoja House haikuwa kughasiwa.

Muhimu kujiuliza ni kuwa ikiwa kiatu kikivaliwa mguu mwingine, kitaenea kwa namna ile ile?
 
Ushindi mkubwa, mzuri sana na wa kishido kikuuu uliokosa mawakala wa vyama washindani, hakika ni ushindi mwema na wa aina yake aka kihistoria tangu Tanaganyika iwepo. Viva my democratic TZ
 
Shetani huja kwa sura mbalimbali za wanadamu. Tuliishamsikia MAMA s akitamba kuhusu umahili wa wauwaji wao.
 
Umejazwa kasumba umepumbazwa,mara mabeberu mara wadau wa maendeleo!Nilichoona labda unaweza kukariri kama mtoto ametumwa dukani,anaimba njiani,''unga robo na chenji irudi!''
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…