Tumia chumvi kufanya scrub na kuboresha ngozi yako

Tumia chumvi kufanya scrub na kuboresha ngozi yako

InnovatorTz

Member
Joined
Jul 1, 2016
Posts
23
Reaction score
23
Habari,

Leo katika urembo tunakuletea namna ya kufanya scrub kwa kutumia chumvi na maji ya baridi na kuonekana wa kisasa zaidi.

Utumiaji huu ni wa salama zaidi na watumiaji wamethibitisha swala hilo kwa asilimia 100%.

Chumvi ni kiungo muhimu kwa kila mlo pia inaumuhimu mkubwa katika urembo. je una fahamu kwamba chumvi unaweza kuitumia kama scurb na kukuacha ukiwa na ngozi ya kuvutia na nyororo?

Matatizo ya chunusi , ukavu katika ngozi, mafuta usoni na hata ngozi iliyokufa usoni ni miongoni mwa mambo yanayowakera warembo wengi na hatimaye kuwafanya watumie vipodozi ambavyo si salama kwa ngozi zao.

Kwa kulitambua hilo wataalamu wa urembo wa asili wamegundua kuwa chumvi ni scrub yenye gharama nafuu ambayo kila mtu anaweza kutumia tofauti na urembo mwingine wa ngozi. Matumizi ya chumvi yamekuwa na matokeo mazuri katika matatizo mbalimbali ya ngozi japo kuwa si wengi wanalolifahamu hili unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha chumvi haiingii machoni pindi unapotumia.

MAHITAJI

Chumvi ya unga kijiko kimoja cha chakula

Jinsi ya kufanya

Nawa uso wako kwa maji safi ya kawaida kisha chukua kitambaa laini na safi chovya kwenye chumvi kisha sugua kwenye uso taratibu pia unaweza kutumia hata mwilini.

Baada ya kujipaka katika uso weka pembeni kitambaa kisha anza kujisungua kwa kutumia viganja vya mikono yako fanya hivyo hadi utakapoona taka zinatoka kisha kaa kama dakika 2/5 ukisha maliza osha kwa maji ya baridi.

Ni muhimu kufanya zoezi hili kwa wiki mara mbili kwani linasaidia kuondoa mikunjo na husafisha ngozi kabisa.
 
Mimi nilipakwa scrub ya chumvi imechanganywa na ukwaju. Matokeo ni poa sana ila inauma. Upo hapo kui?
 
  • Thanks
Reactions: kui
Wewe lazima utakuwa ni Mkongoman,vipi una kibali cha kuishi Tanzania.Kwa taarifa yako tukimaliza zoezi la kuhakiki vyeti vya taaluma tunahamika kuhakiki uraia.

Wewe ndio wale wanaume wana vipele kwenye ndevu kama nungunungu halafu umekomaa hutaki tiba. Na kwapa jeusi utafikiri umeweka bandeji hahahaha!!!

Staarabika bwana Ngongo misimamo mingine ni ushamba tu
 
Wewe ndio wale wanaume wana vipele kwenye ndevu kama nungunungu halafu umekomaa hutaki tiba. Na kwapa jeusi utafikiri umeweka bandeji hahahaha!!!

Staarabika bwana Ngongo misimamo mingine ni ushamba tu

Haijalishi lakini suala la kuhakiki uraia lipo pale pale haaa haaa.Ngoja tukukute unawaka waka kama binti halafu utuambie ni kabila gani hapa Tanzania wanaume wanajikwatua usoni.
 
Haijalishi lakini suala la kuhakiki uraia lipo pale pale haaa haaa.Ngoja tukukute unawaka waka kama binti halafu utuambie ni kabila gani hapa Tanzania wanaume wanajikwatua usoni.

Sasa ona unavyojidhalilisha mkuu, tangu lini chumvi na ukwaju vikabadilisha rangi ya ngozi?

Watu kama wewe mnakuwa na ngozi fulani hata mamba ana nafuu mnawatesa wapenzi zenu jamani. I used to respect you Mr. Ngongo I didn't know you were so uncivilized
 
Wewe ndio wale wanaume wana vipele kwenye ndevu kama nungunungu halafu umekomaa hutaki tiba. Na kwapa jeusi utafikiri umeweka bandeji hahahaha!!!

Staarabika bwana Ngongo misimamo mingine ni ushamba tu
Halafu akiwaona akina chriss brown wanang'ara anajua walizaliwa vile vile,kila kitu matunzo joo
 
Tuliambiwa tukichezea chumvi kwenye ngozi tutapata ndutu.
 
Je asali je wanajamvi inasaidiaje ngozi kwa wale wanaojipata hasa usoni?
 
Mwanamitindo Heaven Sent

Njoo uone hii scrub ya ukwaju na chumvi ya Lusajo.
Itabidi tufanye hii kabla ya party, lakini tukifika huko sura zitakuwa zimetuparama zinatuwaka moto...lol
Hahaha mbona kama naogopa? Ila kama hadi lusajo kaikubali, aisee ntaijaribu. Shoga angu tutang'aaaa
 
Back
Top Bottom