MSONGA The Consultant
Member
- Feb 5, 2022
- 38
- 60
Bao la Mantiki (Logic Framework) ni jedwali ambalo huonyesha uhusiano kati ya Lengo Kubwa la Mradi (Project Overall Objective), Malengo Mahsusi ya Mradi (Project Specific Objectives), Matokeo ya Mradi (Project Outputs) na Shughuli za Mradi (Project Activities) ili kuleta mtiririko wenye mantiki.
Bao la Mantiki ni miongoni mwa njia zitumikazo katika uandaaji wa Andiko Bora la Mradi. Wafadhili wengi wamekuwa wakihitaji Bao la Mantiki pindi unapowasilisha Andiko la Mradi kwa ajili ya kuomba ruzuku. Kwa mfano Umoja wa Ulaya (EU) wanalazimisha uwasilishaji wa Bao la Mantiki pindi uombapo ruzuku kwao. Kwa sababu hiyo, ni vyema wewe kama mtendaji wa Taasisi/mwandishi wa Mradi ukafahamu namna ya kuandaa jedwali hili ili kujiwekea mazingira mazuri ya mradi wako kukubalika.
Kitaalamu, ninapenda kushauri kwamba, uandaaji wa Bao la Mantiki ufanyike katika hatua za awali kabla ya kuanza kujaza fomu ya mradi (ikiwa utahitajika kuwasilisha Andiko la Mradi kupitia fomu maalum)
MUUNDO WA BAO LA MANTIKI
Jedwali la Bao la Mantiki linatengenezwa kwa mistari minne ya kusimama (columns) na minne yenye kulala (rows). Mistari yenye kusimama (columbs) hubeba taarifa zifuatazo;
- Msatari wa Kwanza (First Column); huonyesha mpangilio au uhusiano uliopo baina ya Lengo Kubwa la Mradi (Overall Project Goal/Objective), Dhumuni la Mradi (Project Purpose), kwa lugha nyingine huweza kutambulika kama (Specific Objective), Matokeo ya Mradi (Expected Results) na mwisho kabisa ni Shughuli za Mradi (Project Activities)
- Mstari wa Pili (Second Column); huonyesha viashiria vinavyotumika kupima mafanikio/matokeo ya Mradi ( verifiable indicators of achievement). Viashiria huweza kuwa idadi ya watu waliopatiwa mafunzo (ikiwa mradi ni wa kuwajengea watu uwezo), idadi ya vyoo vilivyojengwa (kwa mradi wa ujenzi wa vyoo)
- Mstari wa Tatu (Third Column); huonyesha vyanzo vya uthibitisho wa mafanikio ya mradi. Vyanzo hivi huweza kuwa Taarifa ya shughuli za Mradi (Activity Report), Tathmini ya Mradi (Evaluation Report) n.k
- Mstari wa Nne (Fourth Column); huonyesha dhana ambazo hupelekea mafanikio ya Mradi. Dhana huweza kutofautiana kati ya Mradi na Mradi. Mfano wa dhana inaweza kuwa; ushiriki mzuri wa walengwa, ushirikiano mzuri kutoka Mamlaka za Utawala, Upatikanaji wa fedha n.k
- IKIWA rasilimali (resources) zitapatikana tena kwa wakati; basi shughuli za Mradi zitafanyika kikamilifu
- Na IKIWA shughuli za mradi zitafanyika kikamilifu; basi matokeo ya mradi yatatokea
- Na IKIWA matokeo ya mradi yatatokea; basi dhumuni la mradi litatimia
- Na ikiwa mradi utatimiza dhumuni lake; basi mradi utaweza kuchangia utimilifu (contribute) katika lengo kuu
Taasisi nyingi pindi zinapoandaa Bao la Mantiki, hufanya makosa yafuatayo;
- Kuanza na hatua/kipengele cha shughuli za mradi (project activities) badala ya lengo kuu la mradi (Overall Objective)
- Kudhani kwamba viashiria vya mafanikio ya mradi (verifiable indicators) ni sawa na lengo (target)
AHSANTE
OMAR MSONGA (BA. PPM & CD)
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
Call: +255 719 518 367
Email: omarmsonga8@gmail.com
Dar es Salaam
Tanzania