Tumia Pesa ya mkopo kwa nidhamu ya hali ya juu

Tumia Pesa ya mkopo kwa nidhamu ya hali ya juu

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Ni ukweli ulio wazi kwamba maisha yana kupanda na kushuka, wakati mwingine inatokea mambo yanakuwa magumu kama vile biashara kuyumba nk,

Kwa mfanya biashara ukichukua mkopo ili ku boost biashara yako pale ukwamapo siyo mbaya,

Niwape kisa kimoja
Kuna rafiki yangu alichukua mkopo kama ML 15 akanunua gari aina ya Ist kwa ajili ya kutembelea, aliuziwa na mtu kwa Tsh M 8, kwa kifupi gari yenyewe kumbe alishikishwa, ilikuwa kimeo, baada ya miezi miwili akauza kwa hasara Ml 4.5.

Jamaa amebaki kulalamika kazini anapokea nusu mshahara, ana watoto wanasoma, mambo hayaendi.

Sijaanzisha huu uzi ili kukupangia matumizi ya pesa zako, , ila nakushauri tumia kwa busara mikopo inaumiza mno.

Nb .Majuto ni mjukuu.
 
Kuna mwalimu mmoja anaitwa A. Sagomba yeye kuchukua mkopo wa milion 7 then taizi la kwanza akanunua suti ya laki 2 muda wa mkopo ni miaka 5 .....Namlilia malebo
 
Ndugu zangu ukitaka kununua gari, achaneni na used za bongo tena ikiwa ndio gari yako ya kwanza acha.
 
Back
Top Bottom