JamiiCheck
JF-Expert Member
- Nov 3, 2023
- 245
- 267
Utafiti ni mojawapo ya vyanzo muhimu vya taarifa, lakini si kila utafiti unaochapishwa ni sahihi au unawakilisha ukweli. Kabla ya kuamini hitimisho la utafiti wowote, hakikisha umetathminiwa kwa kina.
Mfano mzuri ni utafiti uliochapishwa mwaka 1998 katika jarida la The Lancet uliodai kuwa chanjo ya surua (MMR) husababisha usonji. Mwaka 2010, utafiti huo ulifutwa rasmi baada ya kubainika kuwa ulikuwa na udanganyifu wa data, ukiukaji wa maadili ya utafiti na mwandishi wake mkuu alikuwa ameficha maslahi ya kifedha. Tangu wakati huo, tafiti nyingi zenye ubora wa juu zimeonyesha kuwa hakuna uhusiano kati ya chanjo ya MMR na usonji.
Unapotumia utafiti kama chanzo cha taarifa, hakikisha:
Umetathminiwa na wataalamu wa fani husika (peer review).
Umechapishwa katika jarida linaloaminika.
Hakuna migongano ya maslahi kutoka kwa wafadhili au taasisi zilizohusika.
Hitimisho lake linaungwa mkono na tafiti nyingine huru.
Kumbuka: Utafiti mmoja pekee hauwezi kuthibitisha ukweli. Ushahidi unaotokana na tafiti nyingi zinazofikia hitimisho linalofanana ndio msingi imara wa kufanya maamuzi na kuamini taarifa.