Tumia vizuri mfungo huu utoke jumla kwenye miasha dhambi

Tumia vizuri mfungo huu utoke jumla kwenye miasha dhambi

MNEKI

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2014
Posts
992
Reaction score
1,311
Huu Mfungo ukiutumia vizuri,
Ni muda Muafaka wa kushinda jumla matamaa-tamaa yako ya kifala!!
Usione mwanamke mzuri tayari unamtaka , Kama umerogwa.!!

Ushokijua ni kadiri unanyoendekeza tamaa ndivyo unadhoofisha hatima yako kubwa ambayo Mungu kakupangia.

Dhamilia kuacha ujinga Mfungo huu,,
Baada ya hapo fanya maisha ya mifungo na ibada kama tabia yako.
Unatenga angalau Siku mbili za kufunga ndani ya wiki na ibada zako za Kila siku,, maisha yanakuwa mepesi .
Hupotezi muda, zaidi unawekeza kwenye kesho yako ambayo ni Mungu pekee ndiye anaijua.
Sio kuvizia kwaresma na Ramadhani !!

Inahitaji akili ya wehu kuamini mwezi mmoja utakusanya Nguvu ya kushinda dhambi kwa mwaka mzima wenye Miezi kumi na mbili.
Sio kwa shetani huyu.
 
Back
Top Bottom