Tumieni Hesabu za Seti Katika Kutafuta Idadi ya Serikali (Katiba Mpya)

Tumieni Hesabu za Seti Katika Kutafuta Idadi ya Serikali (Katiba Mpya)

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
495
Reaction score
379
Tume ya mabadiliko ya katiba Imetoa mapendekezo ya serikali tatu, mengi yamesemwa na yatasemwa, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndo ulizaa Tanzania, yaan ilikuwa hivi, Tanganyika+Zanzibar: Herufi za Kwanza za neno Tanganyika yaan TAN ndizo zilizoanza kuchukuliwa ili kuunda neno Tanzania, baadae ikafuatia herufi ZA ya Zanzibar, baadae ndo kila herufi zilizokuwa pande zote yaan n, i, a zikachukuliwa na kuzaa neno TANZANIA.

Kwa bahati mbaya au kwa makusudi Tanganyika ikapotea na Zanzibar ikaendelea kutukuzwa na hadi leo ipo, kabla ya muungano Nchi ya Tanganyika ilikuwepo lakini baada ya Muungano nchi ya Tanganyika ikapotea je, Nani aliruhusu ipotee? kwa nini ilipotea?

Jambo la dhahiri ni kuwa hadi sasa hatujui makubaliano ya Marais wawili waliowezesha Muungano upatikane, je walikubaliana kuwa baada ya kuungana majina Tanganyika na Zanzibar yasitumike tena, ila iwe Tanzania bara na Tanzania visiwani?

Kwa nini Tanganyika haitaki kuiachia Zanzibar iwe huru? je ni sababu za kiusalama zaidi au? je zanzibar itaweza kujiendesha bila Usaidizi wa Tanganyika? je Zanzibar itapoteza nini ikiwa tutajitenga?

Nimesikitika kuona watu wakitumia hasabu ya 1+1 = 2, halafu hawakujua kwamba 2 ni Tanganyika na Zanzibar.

Hamujui hesabu za seti. Union ina sehemu tatu, ina non union areas 2 na union area 1, yaani jula ni sehemu tatu

1 Zanzibar (Non inter sectional are)
2 Tanganyika (non inter sectional area)
3 Tanzania (inter-sectional area)

Tatizo nape na ccm wote hawajui hesabu ipi inatumila wapi?

Kawaulizeni watoto wa drasa la kwanza, watwaambia ni moja au tatu. Hakuna mbili.

attachment.php
 
Sijui watakula wapi tukianza kutoza kodi hizi tani lukuki za vyakula vinavyopakiwa kwenye boti kuelekea Unguja kila siku.
 
Nchi yenye ukubwa wa kata moja ya Ubungo, eti iungane na Nchi kubwa kama Tanganyika na kutuletea vimanenomaneno. Vunjilia mbali muungano wa kizushi.
 
Kunatofatuti kati ya KUJUMLISHA na KUUNGANISHA

Nimeipenda hoja yako. Kimsingi mantiki ya kuunganisha katika mahesabu ilipashwa kuwa siyo 1 + 1 bali ni 1 x 1. Kwa mantiki ya hesabu ya kujumulisha hapo hujaunganisha nchi bali ulikuwa na nchi moja ukaogeza nyingine ukawa na nchi mbili, kinyume na dhana ya kuunganisha nchi mbili ukawa na nchi moja.

Sasa haya yanayoelekea kutokea sasa hivi kama rasimu ya katiba hii ikipita wameyataka wenzetu walioumbwa wanung'unike tu na kutufanya sisi hatuna akili. Wanadai "full sovereignty" na hako kanchi kao ndani ya Muungano na sisi tumechoka kuubeba muungno usio na mantiki. Pendekezo la serikali tatu mantiki yake kwa kweli ni kutuingiza katika mazingira ya mpito (transition) ya kuufisha muungangano maana hakuna njia nyingine. Serikali tatu siyo dawa ya kuuponya muungano bali mashine ya kupumulia wakati huu mgonjwa anaposubiri huruma ya Mungu, maana juhudi wa waganga zimefika kikomo. LET ZANZIBAR GO!
 
Hakuna haja ya kubembelezana kwani Muungano unaopiiwa debe na hawa magamba ahuna tija yoyote kwa sasa.Namwomba sana Mungu Chadema ishike dola 2015 ili iunde tume bora ya kutengeneza katiba bora itakayowasaidia watanganyika kupata maendeleo ya ukweli sio huu usanii wa magamba waliotuletea sasa hivi.
 
Sijui watakula wapi tukianza kutoza kodi hizi tani lukuki za vyakula vinavyopakiwa kwenye boti kuelekea Unguja kila siku.

KUH TAARIFA Chakula kikuu zanzibar ni mchele, ngano na sukari na zaidi asilimia 90 ya bidhaa hizo zinatoka pakistan, india na thailand, bidhaa zinazotoka zinazotoka kwetu huku TG ni ghali kuliko zile za nje mfano mchele wa TG unauzwa kilo moja tsh 2000 ule wa nje sh 1100, sukari nyekundu inayozalishwa huku kwetu kule haitumiki sana wao wanatumia sukari nyeupe. Tukiweka kodi bidhaa zetu tutakula wenyewe kwa sababu watashindwa kununua kwetu, wewe si una elimu kidogo? na unajua gharama za uzalishaji wa bidhaa kwetu ni kubwa kuliko nchi nyengine.
 
1+1=3 na au1+1=1
kamwe moja +moja huwezi pata mbili(2)
Utapata mbili kama vitu vinavyojumlishwa vinafanana kwa kabisa kwa asilimia 100
Je ni sahihi kusema Tembo mmoja+Swala mmoja= Tembo mmoja?
Mwanamume mmojo +mwanamke mmoja= Mtoto mmoja au ni sawa na Watu Watatu
Chungwa moja +Chungwa moja=Machungwa mawili(2)
Chungwa moja +Limau moja= Tatu yaani
1-Ladha ya chungwa peke yake
2-Ladha ya Limau peke yake
3-Ladha ya Mchanganyiko wa Limau na Chunwa
Kupanga ni Kuchagua
Hakuna Demokrasi isiyokuwa na gharama:yield:
 
Hamujui hesabu za seti. Union ina sehemu tatu, ina non union areas 2 na union area 1, yaani jula ni sehemu tatu

1 Zanzibar (Non union are)
2 Tanganyika (non union area)
3 Tanzania (inter-sectional area)

Tatizo nape na ccm wote hawajui hesabu ipi inatumila wapi?
 
Nchi yenye ukubwa wa kata moja ya Ubungo, eti iungane na Nchi kubwa kama Tanganyika na kutuletea vimanenomaneno. Vunjilia mbali muungano wa kizushi.

Mbona hatuoni jitihada za kuungana na kenya au malawi?
 
Hamujui hesabu za seti. Union ina sehemu tatu, ina non union areas 2 na union area 1, yaani jula ni sehemu tatu

1 Zanzibar (Non union are)
2 Tanganyika (non union area)
3 Tanzania (inter-sectional area)

Tatizo nape na ccm wote hawajui hesabu ipi inatumila wapi?

Kuanzia kwa Mwenyekiti wa nyinyiemu hadi balozi wa nyumba kumi kumi hakuna anayejua hesabu ndo maana hata kwenye kura za urais aliyekuwa na kura kidogo ndo alitangazwa eti ndo mshindi.
 
Sijui watakula wapi tukianza kutoza kodi hizi tani lukuki za vyakula vinavyopakiwa kwenye boti kuelekea Unguja kila siku.

Kwani wale wanaochimba almasi na dhahabu na kuzisafirisha wanalipa kodi?
 
Wape wenye maslahi ktk huu muungano na si bure
 
Hivi kwanini watanganyika hawawezi kuungana na nchi nyengine zaidi ya zanzibar?
 
Mke mmoja znz +mke wa pili bara= mume mmoja popote hesabu ya muungano ndo hiyo je Jibu utapata nyumba ngapi?
 
Nimesikitika kuona watu wakitumia hasabu ya 1+1 = 2, halafu hawakujua kwamba 2 ni Tanganyika na Zanzibar.

Hamujui hesabu za seti. Union ina sehemu tatu, ina non union areas 2 na union area 1, yaani jula ni sehemu tatu

1 Zanzibar (Non inter sectional are)
2 Tanganyika (non inter sectional area)
3 Tanzania (inter-sectional area)

Tatizo nape na ccm wote hawajui hesabu ipi inatumila wapi?

Kawaulizeni watoto wa drasa la kwanza, watwaambia ni moja au tatu. Hakuna mbili.

attachment.php
 
Attachments

  • Tanzania Union.jpg
    Tanzania Union.jpg
    7.5 KB · Views: 746
Dawa ya huu muungano ni moja tu, iitishwe kura ya maoni kwa pande zote za muungano watu waseme NDIYO ama HAPANA kuhusu muungano halafu mambo mengine ikiwamo aina na mfumo wa muungano yafuate thereafter.
 
Back
Top Bottom