Tumjadili Hashim Dogo na Ufalme wake wa Hip - Hop

Kama alishindwa kwenda mainstream enzi hizo hakuna ushindani mkubwa n' hakuna ubanaji wa Hiphop redioni basi hawezi kuwa mkali huyo
 
 
Pengine tutamkumbuka tu kwa kuwa ni moja kati ya wale walionza huu mziki zamani kidogo kipindi una anza anza, sio rahisi kumkumbuka kama mfalme. maana watoto waliozaliwa miaka ishirini iliyopita asilimia 98 hawamfahamu Hashimu Dogo Hata humu jukwaani tu ukiuliza ni wangapi wanamfahamu Hashimu dogo nadhani asilimia 80 hawafiki. sasa hapa tunaanzaje kumwita mfalme??
 
 
 
Tupo dunia tofauti hatuwezi kuelewana. Unaonekana mshikaji una mapenzi makubwa sana na Fm radios, sisi wengine haya mambo tumeanza kuyafatilia kabla ya ujio wa Fm.

Wakina 2 Proud,Balozi mbona tuliwafaham kabla ya FM kuanza kuwa hot,yeye alikuwa wapi?
 

Kwanini hata kitukuu chako kitamwita Pele mfalme wakati hata Messi hakijamshuhudia? .......kuna watu wamezaliwa na vitu ambavyo ni ngumu kuvipata kwa mwingine yeyote ......Hashim Dogo ni mfalme kwa tuliomsikia kipindi hicho na hata sasa tunasikiliza mziki .............
 
 
Ni kigezo gani mnampa hasheem ufalme? ...nimegundua wengi humu hawakuwa hata wanaudhuria matamasha that time. ....nashukuru nilikuwa mmoja wa waandaji wa matamasha kipindi hicho. .....hasheem alikuwa mzuri kwenye kiingereza lakini sio kwa freestyle (kumbuka wengi walikuwa wana freestyle mistari waliokuwa tyr wameshaitunga, ndio maana ngwear anabaki kuwa king of freestyle wa bongo).
Hashim kilichokuwa kinambeba ni sauti yake nzito yenye punch na style yake ambayo maneno yalikuwa yanasikika, tofauti na wengi kipindi hicho walikuwa wana rap kwa speed na wanafanya tongue twist.......na isitoshe Hashim wengi wamemjua kupitia fm radio kwa wimbo wake aliofanya na unique sisters pamoja na huu dark of. ..... , kwenye matamasha mengi alikuwa si muudhuriaji, inakuwaje leo umpe taji la ufalme?
 
Waliopanda wameshuka, wanatetemeka hawana pakushika itafahamikaa (ney wa mitego )
Hili game gumu, so take care aliimba niki mbishi nini huyo dogo hashimu
 

Hashim dogo hakuwa mzuri kwenye freestyle? .....unajua wengi kwenye "shadow of a dark destiny" tulipenda Zaidi mistari ya Kiswahili? Tafadhali mkuu .....huyu legend kipindi kile na mazingira ya muziki hasa Hip hop ilikuwa bado haipewi nafasi lakini akafanikiwa kuifanya kwa kiwango ambacho flow yake hata sasa ni ngumu kuipata pamoja na technology iliyopo Bongo.
 
Alkua tu mwandishi mzuri, kuusu ufalme iyo hapana aise, lakini rhymin jamaa kweli ALIKUA anaweza, sasa kwanin siku izi hayupo? nnavyojua mtu kuitwa mfalme ina maana we ni kiongozi wa teritory mpaka kufa, sasa hatuwezi kumuita mfalme akati hayupo tena, ha-exist.. tumuiteni best lyrcist au best rhymer au best freestyler, au sijui nini kingine, kuhusu ufalme hapana
 

Kiongozi unachanganya sana mambo mpaka nashindwa kukupata kama tupo kurasa moja kwenye jambo tunalolizungumzia mbele yetu.
 
Na mimi nimeshangaa.
 

Ku freestyle wengi walikuwa wanachanganya na verse walizokuwa wametunga zamani. ...mmojawapo ni hasheem, nakumbuka ilikuwa lang'ata walishindanishwa Hashim na solothang kisha taji liundi akawauliza fans wachague nani mshindi, wakasema solooooo
Hashim amefahamika wkt Sugu tayari ana album moja na hard blasters wana album moja na walikuwa wanapendwa ile mbaya na sos b alikuwa yupo juu that time(walikuwa kundi moja black houndz)
Hivyo kusema jamaa ni mfalme hamumtendei haki.
 

Tunamwita mfalme sababu ni package iliyokamilika ya hiphop, wenzake wengi wanafanya vizuri lakini wakosa baadhi ya vitu muhimu kwenye utamaduni wa hiphop. Kwa mfano Kwanza Unit ni wachanaji wazuri lakini hawakuwa na ujuzi wa kufreestyle kitu ambacho pia anakikosa Fid Q.

Kuhusu uhandishi wake pia ni baabkubwa ndio maana ukimsikia anavyochana ni ana tiririka sababu anaandika hatungi kupata punchline kali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…