Tumjibu Askofu Gwajima Kisayansi na si Kisiasa, tuache kumshambulia na kumtishia. No research no right to speak


G/morning

Indeed it will be just amazing to ask the rationale of stats, as of believing that the developed COVID-19 vaccines have the potency while the recipients still can contract/spread the disease.

Gwajima hana ulazima wa kuthibitisha madai yake. Kisheria anayepaswa kuthibitisha ubora na usalama wa chanjo katika muda mfupi, kati na mrefu, ni mtengenezaji wa chanjo, yule anayemtaka mtu achanjwe, na mchanjaji. Kwamba mtengenezaji wa chanjo na mtoa chanjo hausiki na matokeo (hasi/chanya) baada ya mtu kuchanjwa, kunaacha maswali kadhaa ya msingi, ambayo ni madai ya Gwajima.

Gwajima apewe majibu ya kisayansi na si vitisho. Amejitokeza kuwa msemaji wa kondoo wake, kama huyu [emoji116]
 
Mimi mwenyewe nimechanjwa mwezi wa tatu sasa na niko poa tu.
Hongera kwa maamuzi hayo kuhusu afya yako. Natumaini kabla ya kuchanjwa ulipewa nafasi ya kujieleza, kupimwa afya yako na maelekezo kuhusu chanjo (infomed decision).
 
Kabla ya kama atajibiwa au la awajibike kwa insubordination.
Hoja yeyote aliyonayo alitakiwa ajiuzulu kwanza. Hiyo ndio sheria. Tuanzie hapo.
Kuna mengi ambayo nae yanamhusu e.g. vyanzo vya taarifa zake, utalaan ktk fani hiyo na kithibitisha hoja zake kwamba viongozi wamechanjwa kimagumashi kuwazuga watz n.k, lakini kabla ya yote awajibike. Naona mnampa big up sana huyu gwajima chameleon bila kuliangalia hilo.

Kauli nyingine ya kipuuzi ya huyu chameleon ni ile ya kusema potelea mbali ubunge.
Angekuwa hachukui posho angekuwa na hiyo jeuri

Edwin Mtei aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu alipoona Nyerere hataki ushauri wake kwenye masuala ya IMF alijiuzulu kesho yake.

Hapa huyu bw anatakiwa ajiuzulu kwamza wote mnaompigia debe hamlioni hilo haijalishi kama chanjo ni sawa au sio sawa.

Kama hajali sana Ubunge mbona anakomba hizo m11 na ushee kila mwezi.
 
Unateseka ukiwa wapi?unawaabisha sana wazazi wako....umaskini wako unakuletea hasira....😂😂😂😂
Masikini yule mbwa aliyekuwa akitamani kupora hela za watu, masikini yule alikuwa ni zaidi ya shetani.
 
Anachotukera ni kutangaza hadharani msimamo wake wa kutochanja.... hapa anapingana na serikali yake ya CCM waziwazi kitua ambacho hakina uhai kwa chama chetu.

Kama ana hamu ya kuungana na CDM kudai katiba mpya aseme mapema - mambo ya chokochoko sisi hatutaki.
 
Jamaa kaeleza kisayansi San na kaeleweka naunga mkono hoja
 
Hata kimya ni jibu pia,je unalifahamu hilo na je analifahamu hilo?
 
N
Habari za mungu ni pamoja na kuwaokoa watu wasiuwawe na machanjo ya ajabu ajabu!
Sawa kabisa lakini Mungu muumba Mbingu na nchi hapendi mtu anaefanya kwichikwichi kujificha nyuma ya JINA lake

Hata fl. Mbxxsha inaekea alimtafuna pia, inaelekea alijiongeza kwa yule bro mambo yakaisha, ila ile clip angeenda kumshitaki aliye ipost, baadala yake amezuga halafu anajidai mtu wa Mungu.
Yaani anawapumbaza mnasahau kabisa habari zake za uzinzi.

Inabidi nikubali " the guy is really smart upstairs"

Amewatoa kwenye reli sasa amakubalika kama mtu wa Mungu mmesahau kila kitu cha zamani

Hatudanganyiki wote mkuu.

Huyu Gwajiboy namjua toka anaanza kanisa pale Ubungo juu. Ile bar ya Hunters Club, enzu hizo ndio alifanya kanisa. Hapo kufufua misukule ilikuwa bado sana.

Alikuwa hamna kitu anakuja kwenye cafe yetu palepale jirani kupata internet karibu kila siku.

Unajua scandal zake na longolongo zake au unafuata mkumbo tu ?

Hajasomea hayo mambo kabisa. Anapata ubuyu toka kwa jopo lale halafu kichwa anaenda live.

Hata 5G yeye bingwa pia katoa mada kibao, na kikika kingine utakuta nacho anatoa mada.

Ana Shahada za Juu za Theolojia basi. Ila bingwa wa kuropoka.

Kuna watu wanadhani Gwajiboy anahoja ni tofauti kubwabwaja kanisani na kuitwa kwenye jopo la mabingwa wa fani hizo.
Mambo anayozungumza yote yapo kwenye mtandao.

Ahubiri Biblia tu na akiweka mkazo amri ya 6 basi inatosha.
Kama hataki kuchanja ajiuzulu.
 
Analysis nzuri Sana.
Katika vitu Mimi nami Nina maswali kuliko majibu.
1. Watu waliopona baada ya kuugua Corona ni wengi Sana kwa mbali kuliko waiokufa.

Kwanini nguvu isielekezwe kwenye kuwajulisha watu kuwa wengi wanapona, na kwa dawa gani wamepona,ili watumie hizo?

Badala yake kutiwa hofu kana kwamba ukipata Corona lazima ufe tu.
Kazi ya wataalamu wa afya ni kuwapa matumaini wagonjwa siyo kuwatisha.

2.Katika watu zaidi ya 4m. Waliokufa bara la Afrika hawafiki hata laki nne.
Kwanini viongozi wanataka tuogope Sana kuliko hata kule ugonjwa umeweka makao?

Wao barakoa Sasa si lazima,sisi tunalazimishwa kwanini? Kwa ugonjwa ambao si kitisho kwa Afrika?
Maana Afrika inayo magonjwa mengine tu yanayoua Sana kuliko Corona mfano Malaria.
Je inaingia akilini kuwalazimisha wazungu kuogopa Malaria kwao inayoua watu wachache?

3. Kwa vile uamuzi wa kuchanjwa umetokana na ushauri wa tume ya Corona.
Kwanini hiyo tume isitolee ufafanuzi wa hoja ambazo Gwajima na wananchi wanauliza? Kuliko kukimbilia kumtishia Gwajima?
 

Kwenye kesi yoyote ‘mshtaki’ ndio anaanza kwa kuthibisha uhalali wa mashtaka yake, na sio upande wa ‘utetezi’ unaanza kwa kujibu.

Wewe kama mfuasi wa Bishop Gwajima chukulia hii ni fursa adimu serikali imempa kupeleka ushahidi wa madai yake na kama maelezo yake yanajitosheleza mbele ya sheria ajibiwe.

Vinginevyo unataka serikali ipoteze muda kujibizana na kila mtu atakaekuwa anajitungia mambo tu.
 


Sayansi iko wazi lakini anapotosha makusudi kwasababu ya kupata sifa tu na sadaka. Huyu ndiyo mtu anadanganya watu kuwa ana fufua watu leo unataka eti science !
 

Tatizo jopo la madaktari limeshakaa wakisema pelekeni maswali mnasema hamna kwasababu hamtaki kujua ukweli bali kuweka drama mitandaoni na kupotosha watanzania. Ndugu zangu wote wamechanja na hakuna tatizo lolote . Watu wanakufa nyie mnaona hii ni drama show!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…