Tumkumbuke Luteni Rajab A. Mlima

Tumkumbuke Luteni Rajab A. Mlima

Saguda47

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
11,258
Reaction score
20,386
Kwa ufupi.

Lt. Rajab Ahmed Mlima alizaliwa 30 Agosti 1977 na alifariki 27 Oktoba 2013.

Luteni Rajab Ahmed Mlima alikuwa askari katika jeshi la wananchi JWTZ, alikuwa Komandoo katika kikosi maalum cha JWTZ chenye makao yake makuu mkoani Morogoro eneo la Ngerengere- Sangasanga (92 kj). inaelezwa kipindi cha uhai wake Lt. Rajab A Mlima alikuwa mwenye kupenda elimu na mwenye kujituma awapo katika majukumu yake ya kijeshi na nje ya jeshi.

Mauti yalimkuta akiwa katika majukumu ya kulinda amani huko Congo DRC Mashariki mwa Goma ambapo yeye na wenzake kutoka Tanzania alikuwa akiwalinda raia dhidi ya waasi wa M23 ndipo waliposhambuliwa kwa mabomu toka kwa waasi wa M23 wenzake baadhi walijeruhiwa na yeye kupoteza maisha.

Baadhi ya picha enzi za uhai wake.

commando ahmed mlima.JPG3.JPG

moja ya picha akiwa kwenye mafunzo ya ukomandoo
commando ahmed mlima.JPG

Akipokea nembo maalum ya ukomandoo (wing seal special force) baada ya kuhitimu mafunzo hayo hatarishi na magumu.
commando ahmed mlima.JPG 2.JPG

Akiwa kwenye pozi katika uwanja wa ndege huko Goma- Congo DRC
commando ahmed mlima.JPG 5.JPG

Akiwa msituni mashariki mwa Congo DRC.
commandoo tz.jpg

1935083_540703196136763_4383791638258077260_n.jpg

Yes it's a Tanzanian Special Forces unit Logo. 92KJ COMMANDO.​

TUTAKUKUMBUKA KOMANDO WETU Lt. Rajab A
 
Why huyu na ni luteni tu? Roho yake si sawa na askari wengine wanaofariki kusimamia taifa
 
Why huyu na ni luteni tu? Roho yake si sawa na askari wengine wanaofariki kusimamia taifa
kabla hujaandika hivyo ni vyema ungefaham tu hata robo ya kadhia na magum ya kupata medani ya ukomandoo, na ndipo ungekuja kulinganisha thamani ya hii nguvu kazi moja (komando rajabu) na maafisa wengine (wasio makomando).
nmeandika nikiwa na uzoefu katika kupata medani hii ngumu na adimu( not every soldier can become a commando, but all commandos are soldiers)
 
Kuna yule mmoja aliye mrestisha mtu bar maeneo ya Tandika pale my love wake alipotongozwa na mlevi,sijui kesi yake iliishaje yule komando!!!
Cdo hawezi kuachishwa majukum kihivyo kwanza mauaji yalitokea eneo la baa ambapo jamaa (cdo) alikuwa kapachika maji,
 
kabla hujaandika hivyo ni vyema ungefaham tu hata robo ya kadhia na magum ya kupata medani ya ukomandoo, na ndipo ungekuja kulinganisha thamani ya hii nguvu kazi moja (komando rajabu) na maafisa wengine (wasio makomando).
nmeandika nikiwa na uzoefu katika kupata medani hii ngumu na adimu( not every soldier can become a commando, but all commandos are soldiers)
Mkuu achana nao hao watoto ambao uwezo wa uelewa ni mdogo na pia vichwa vyao havipo tayari kueleweshwa.
 
R.I.P shujaa wa taifa,
Uliyekufa ukipigania amani ya waafrika wenzako,
Mungu akupokee na akuweke mahala pema,
Amin.
 
Msibishane na hawa vijana wa digitali kabisa nyie waacheni hawajui gharama za kumuaandaa cdo mmoja tu mpaka afikie hatua ya kuwa full operational. Vijana wao tuwaache na Kelele zao za ccm vs chadema. Inauma sana ila natamani sana vijana waamke wajue hii nchi ni zaidi ya hizo siasa zao
 
Back
Top Bottom