Da Vinci XV
JF-Expert Member
- Dec 7, 2019
- 3,862
- 6,438
- Thread starter
- #101
Siyo kila jambo ni mpango wa Mwenyezi Mungu!
Mipango mingi mibaya ni mipango yetu sisi binadamu.
Usiniambie kuwa matendo yako yote tangu uamkapo hadi ulalapo ni mipango ya Mwenyezi Mungu.
Nitatoa mfano:
Miongo kadhaa iliyopita wakati nikiwa sekondari (maeneo ya kanda ya ziwa), mjukuu wa mama mwenye nyumba alifariki dunia. Msiba ulikuwa pale pale nyumbani tulipokuwa tumepanga mimi na kaka yangu.
Ni wazi kuwa kilichofanya aage dunia kilijulikana pale mtaani. Marehemu (binti) alikuwa mtu wa kujirusha sana na mwisho wake alibeba mimba. Ili kikwepa aibu na mambo mengine aliamua kumeza vidonge ili afanye abortion.
Mauti yalimkuta baada ya kuchukua uamuzi wa kuondoa maisha ya kiumbe kisichokuwa na hatia.
Pale msibani niliona kitu cha ajabu!
Wale wazee wenye kutia ina kwenye ndevu, walifika msibani kwa ajili ya kumpa pole mama mwenye nyumba juu ya msiba wa mjukuu wake. Kauli ya "Pole, hiyo ni kazi ya Mungu", ilitawala pale msibani.
Je ni kweli kuwa ile ilikuwa ni kazi ya Mwenyezi Mungu?
Mwenyezi Mungu ana mipango mizuri kwa wale wamchao - Romans 8:28.
Aisee