Sweya Makungu
JF-Expert Member
- Jun 11, 2023
- 508
- 601
Tumnong'oneze rais kwa sauti ya chini watu wabaya wasisikie..
Ama tuendelee kuwa shamba darasa ama turudie zama za shamba la bibi.
💫💫💫💫💫
©️ Mwl. Makungu m.s
0743781910
Ilikuwa ni lazima Yesu ashitakiwe ili herode na pontio pilato wapatane na kumaliza uadui wao.( Luka 23:12)
Ilikuwa ni lazima Yesu afe ili baraba (mfungwa) apate kuishi na kutoka gerezani. (Luka 23:25)
Ilikuwa ni lazima Afrika nyeusi ife ili izaliwe Afrika nyeupe ambayo wazinifu wanaitwa wapenzi na watembea uchi wanaitwa warembo.
Ilikuwa ni lazima falsafa ya zamani ife izaliwe falsafa mpya ili tupate wadudu wengi..
Ilikuwa ni lazima matete yainame ili upepo mkali unaovuma kwa nguvu upite, yapate kusimama tena..
Ilikuwa ni lazima bwana harusi avue suti , ili wapambe wa bwana harusi wapumzike.
Ilikuwa ni lazima Babeli yenye bustani zinazoelea angani ife ili Iraki inayotia mashaka izaliwe.
Ilikuwa ni lazima wanadamu wavurugwe lugha ili mnara wa Babeli ushindikane kujengwa.
Ilikuwa ni lazima mmasai avae nguo ili mwarabu apewe sifa duniani.
Ilikuwa ni lazima mchanga upate uwezo wa kutembea ili mashine zilizolala ziweze kufanya kazi.
Ilikuwa ni lazima taifa zima lenye maarifa ya uganga wa kienyeji lijifunze uchumi ili iwe rahisi kuwafafanulia kinachoingia na kinachotoka..
Ilikuwa ni lazima kuwatofautisha kwanza aina ya mbuzi , kabla ya kuwaruhusu wale kwenye urefu wa kamba zao.
Siyo mbuzi wote wenye kamba ndefu wanakula zaidi . Bali mbuzi wanaotusumbua ni wale waliokata kamba..
Ilikuwa ni lazima bulb ziungue ili wauza chemli wafanye biashara.
Yesu aliambatana na maskini maisha yake yote lkn alizikwa kwny kaburi la mtu tajiri asiyekuwa na mahusiano naye kabisa.
Ilikuwa ni lazima dada(umbu) yake Musa akae pembeni ya mto
Musa alipotelekezwa , Siyo tu kwaajili ya kujua kitakachompata Musa bali pia kuwa chanzo cha taarifa /maelezo yanayomuhusu Musa kwa binti wa Farao aliyemuokota.
Musa alitelekezwa na mama yake mzazi. Musa akaokotwa na binti wa Farao. Binti wa Farao akamuajiri mwanamke wa kiisrael kumnyonyesha Musa ndani ya ikulu bila kujua ndiyo mama yake mzazi na Musa.
Kwahiyo ilikuwa ni lazima Musa atelekezwe ili mama yake apate kazi ikulu ..
Ukitazama juu utakumbuka kushukuru, lkn ukirudisha macho ukatazama chini unaweza kukufuru .
Fikiria nyuma kwa shukrani, fikiria mbele kwa matumaini, fikiria juu kwa imani..
Mhe. Rais maneno haya nimekunong'oneza wewe tu . Usiwaoneshe watu wabaya.
Kila mstari utakaousoma ukiurudia tena utapata maana tofauti na uliyoipata mwanzo.
Nakusalimia kwa jina la imani , PHILOSOPHY- LOVE OF WISDOM.
Mwl. Makungu m.s
0743781910
14 February 2023