Tumpe heshima Samia Suluhu Hasani, tuchape noti zenye sura yake

Tumpe heshima Samia Suluhu Hasani, tuchape noti zenye sura yake

Wadau napendekeza Mheshimiwa wetu mpendwa Rais Samia Suluhu Hassan, Tuchape noti zenye sura yake kwasabab;-
  1. Ndiyo Rais wa kwanza Mwanamke.
  2. Utendaji wake ni wa kutukuka.
  3. Ana kazi kubwa ya kulikomboa taifa kutoka katika giza nene la chuki, unyanganyi, kupotezana kupigana risasi na ubabe.
Napendekeza hivyo iwe kumbukumbu kwa mama yetu.

Huna akili
 
Yaani unapendekeza tuweke Sura yake kwenye Sarafu/noti zetu ati tu kisa ni
1. Rais wa kwanza Mwanamke?
2. Utendaji ulotukuka (ambao umeupima kwa miezi isozidi mi3)?
4. Na kisa 'ana kazi kubwa ya kulikomboa taifa'?

Well, hata wanywaji wana kazi kubwa ya kuendelea kuongoza kulipa kodi zinazolipa mishahara ya walimu wa watoto wako shuleni, Tuweke na Sura zao kwenye Sarafu??

Nonesense,
Wambie mkuu ,tuna WATU wa hajabu haijawai tokea tz, USA imepata kua na rais kibao je ni wangapi Kati yao wamekua kwenye pesa yao , watz why tunajitoa ufaham kiasi hichi ,tukiitwa wapumbavu twachukia why Afrika
 
Bado ni mapema mno kusema huyu ni Rais bora. Tujipe muda zaidi.

Kwani kuwekwa kwenye pesa ndiyo kuheshimiwa?
 
Wadau napendekeza Mheshimiwa wetu mpendwa Rais Samia Suluhu Hassan, Tuchape noti zenye sura yake kwasabab;-
  1. Ndiyo Rais wa kwanza Mwanamke.
  2. Utendaji wake ni wa kutukuka.
  3. Ana kazi kubwa ya kulikomboa taifa kutoka katika giza nene la chuki, unyanganyi, kupotezana kupigana risasi na ubabe.
Napendekeza hivyo iwe kumbukumbu kwa mama yetu.

Hapana me naona bora tumuongezee muda
 
Naona umesaliti chama cha mbogamboga.
Ulikuwa kwenye team ya praise na worship team ya CCM.
Ila sasa umekuwa msaliti.
AJIRA HAZITOLEWI NA KAZI IENDELEE
Atoe kwanza ajira haraka na pia awashughulikie kwa Sheria waliompiga risasi Lissu
 
Nina imani naye ila sura kwenye noti hapana.
 
Back
Top Bottom