Malick M. Malick
JF-Expert Member
- Apr 2, 2013
- 658
- 312
View: https://youtu.be/Qoag3vwDQrk
Msanii wa UGANDA Jose Chameleon aliimba wimbo unaosema tusisubiri kutoa sifa kwa watu ,wakishaenda, tuwape sifa zao wakiwepo,na ikipendeza wakiwa madarakani ..watanzania tumpe maua yake Rais Samia
Wakati tuelekea mwishoni mwa mwaka 2024 ,ni wakati wa watanzania mmoja mmoja kutambua mchango wa Rais wetu mpendwa MAMA SAMIA SULUHU ,alama ya upendo DUNIANI.
Kiongozi alieziweka 4R katika maisha ya watanzania,Afrika na Dunia.
kila eneo sasa kwenye nchi imekua na baraka ,kisiasa tunaongoza DUNIA ,Tanzania ya SAMIA inaongoza bunge la DUNIA kupitia Dr TULIA,Afya afrika tulimpata DR NDUGULILE[marehemu] kwenye biashara Tumesikia Rais RUTO anasema Tanzania tunaongoza Afrika Mashariki.
Twende kwenye michezo,Timu za Taifa ziko kwenye fainali za mataifa ya afrika morocco 2025,tunaandaa CHAN,na tutaandaa AFCON 2027
Njoo kwenye Elimu kila kata katika nchi hii utakuta madarasa mapya ya kisasa ,shule za mfano za wasichana kila mkoa ,shule kongwe zimekarabatiwa
Twende kwenye uchukuzi ,SGR mtelezo ,viwanja vya ndege vinajengwa ,swala la nishati safi ya kupikia tunaona watanzania walivyolipokea, mitungi kila sehemu kwa kweli tumpe maua yake ,
Hakuna eneo kwenye jamii ambalo mama ajaweka upendo wake ..twendeni tukampe maua yake
Rais wa jamhuri ya muungano wa TANZANIA Mhe Dr Samia Suluhu ameendelea kuwa kiongozi bora mwenye maono ya mbali na yenye maslai kwa watanzania,afrika mashariki,afrika na Dunia kwa ujumla,tunakuombea Rais wetu,watanzania tupu nyuma yako