SoC03 Tumpe maua yake Rais Samia

SoC03 Tumpe maua yake Rais Samia

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
May 9, 2023
Posts
18
Reaction score
14
TUMPE MAUA YAKE MHE. SAMIA
inbound131185818921228781.png


( picha kwa hisani ya Ikulu.go.tz)

UTANGULIZI
Andiko hili limelenga kumpa maua yake mhe. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake jadidi wa nchi yetu ya Tanzania. Naomba kuchukua fursa hiii kumpongeza kwa dhati mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumpa maua yake kwa kuiongoza Tanzania kwa umahiri mkubwa, na kudumisha amani, upendo na utulivu na mshikamano kwa watanzania. Rais Samia anastahili kupewa maua yake kupitia kazi anayoifanya katika nyanja mbalimbali kama vile uimarishwaji wa uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi nyingine, kuimarishwa kwa sekta ya elimu, afya, michezo, utalii, n.k. Ni matarajio yangu kupitia andiko hili mtafurahia kuhusu niliyoyaandika na picha mbalimbali zinazohusu kazi kubwa na nzuri anayoifanya Samia Suluhu Hassan kama ifuatavyo;

Uimarishwaji wa amani, usalama, na utulivu nchini Tanzania; serikali chini ya mhe. Samia kupitia Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi amehakikisha kwamba mamlaka na maslahi mapana ya nchi yetu yanakuwa salama kwakuwa ulinzi na usalama ni tunu muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote duniani ambayo inahitaji kulindwa kwa aina yeyote. Mhe. Samia Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania anaendelea kuhakikisha kwamba kuna uimarishwaji wa umoja, mshikamano, na utulivu nchini Tanzania kupitia kwa Wizara ya Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa amefanikisha kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa weledi na mafanikio hatimaye kuiwezesha nchi kuendelea kuwa na amani na utulivu. Kupita JWTZ imeendelea kushirikiana na Umoja wa Matiafa (UN), Umoja wa Afrika ( AU) na Jumuiya ya maendeleo Kidini mwa Afrika (SADC) katika oparesheni mbalimbali za ulinzi wa amani katika nchi zenye migogoro.

Kuongezeka kwa upatikanaji wa maji; serikali chini ya Mama Samia imeona maji ni hitaji na kimbilio la msingi la kila mtu hapa nchini Tanzania ambapo serikali imeendelea kutekeleza miradi ya maji inayohudumia wananchi wote mjini na vijijini pasipo kujali itikadi au eneo. Mara nyingi Mhe. Samia amenukuliwa akisema anatambua changamoto kwa akina mama katika baadhi ya maeneo wanavyotumia umbali mrefu katika kuhakikisha uwepo wa maji kwa matumizi ya familia. Mfano hadi februari 2023 hali ya upatikanaji wa maji safi na salama maeneo ya mjini imefikia asilimia 86 na miradi 114 inatekelezwa katika maeneo mbalimbali ambapo miradi 40 imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi wapatao 1,978,730 na miradi 74 ipo katika hatua za utekelezaji. Pia serikali inazidi kufanya manunuzi ya mitambo ya kisasa ya maji kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji.


inbound1888984197769772283.jpg
( chanzo .BBC news.)

Sekta ya utalii imezidi kuing'arisha Tanzania kimataifa; takribani asilimia 32.5 ya ardhi yote Tanzania sawa na kilometa za mraba 307, 873 imehifadhiwa chini ya usimamizi wa Wizara ya maliasili na Utalii. Jitihada mahususi za Raisi Samia katika kutangaza Tanzania kimataifa kupitia programu maalum ya Royal Tour zimeifungua Tanzania na kuipa umaarufu zaidi kimataifa. Juhudi hizi za kutangaza utalii zimeingarisha Tanzania kwa kuifanya Hifadhi ya taifa ya Serengeti kubwa hifadhi bora zaidi barani Afrika katika miaka mitatu mfululizo kuanzia 2019-2022.

Utekelezaji wa miradi ya nishati unazidi kushika kasi; sekta ya a nishati imepiga hatua kubwa katika nyanja ya umeme, gesi asilia na mafuta, nishati jadidifu, miradi mikubwa kama mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere wenye megawati 2115 ambao umefikia asilimia 85 kukamilika, bomba la mafuta la Afrika mashariki. Pia serikali kupitia mhe. Samia inazidi kutekeleza miradi ya kimkakati ikiwemo miradi wa utafutaji wa mafuta katika vitalu Eyasi, Wembere, Mnazi Bay Kasikazini, mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia( lique field natural gas) pamoja na mradi wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania ( East African crude oil pipeline-EACOP)

Sekta ya biashara na uwekezaji inazidi kupaa nchini kutokana na ziara za kimataifa . Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan anazidi kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kukubalika na kuheshimika kimataifa kwa kuweka msisitizo katika diplomasia ya uchumi. Mfano kupitia Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na wadau wa diplomasia ya uchumi, nchi marafiki, jumuiya za kikanda na kimataifa imeratibu mikakati mbalimbali ambayo imekuwa na manufaa kwa nchi yetu. Jambo ambalo limeimarisha na kukuza biashara, kusainiwa kwa mikataba ya maendeleo kama vile Raisi Samia ameshuhudia utiaji saini wa zaidi ya mikataba 30 ya biashara na uwekezaji jijini Dubai ambapo alikuwa mgeni rasmi katika kongamano la kimataifa la biashara na uwekezaji.

inbound98095534666293562.jpg


( chanzo cha picha. Jamii forums.com)

Kudumisha kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuondoa vikwazo 11 vya muungano; Raisi Samia amewezesha kufanyika kwa vikao mbalimbali kwa lengo la kujadili masuala ya muungano na kupelekea hoja 11 kupatiwa ufumbuzi kati ya hoja 18 ambazo zimeondolewa kwenye orodha ya hoja za muungano ambapo hati ya makubaliano imeweza kusainiwa mnamo agosti 24, 2021. Miongoni mwa hoja zilizopatiwa ufumbuzi ni moja na uingizaji wa mazimaa kutoka Zanzibar, uvuvi kwenye ukanda wa uchumi wa bahari kuu, ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika taasisi za muungano, mgawanyo wa mapato yatokanayo na misaada kutoka nje ya nchi .n.k. utatuzi wa changamoto hizi unazidi kuimarisha ushirikiano na kuchochea maendeleo.

inbound8755496934639926024.png
( chanzo. EATV news.)

Maslahi ya Watumishi juu, huduma bora kwa Umma; katika sekta za Umma na binafsi wafanyakazi wana mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi na kuongeza pato la taifa. Katika kutambua hilo Mhe. Samia Suluhu Hassan ameweza kuboresha maslahi ya watumishi wa umma ili kuwafanya kutoa huduma bora kwa wananchi. Mfano madai ya watumishi 85,012 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 123.7 yameeleza kulipwa. Pia katika kutekeleza huduma bora kwa umma Raisi Samia serikali yake imetengeneza mifumo mbalimbali ya tehama kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi kama vile mfumo wa sema na waziri wa UTUMISHI, mfumo wa dawati la huduma la OR-MUUB( utumishi call centre).

inbound7326539011633453835.jpg
(chanzo cha picha. Jamii forums.com)

HITIMISHO
Kutokana na andiko kuhitaji maneno yasiyosidi 1000 sina budi kuishia hapa kwa kuyaeleza haya machache kati ya mengi ambayo Mhe. Samia Suluhu Hassan anastahili kupewa maua yake mapema kwa jitihada za dhati za kukuza na kuinua maendeleo ya Tanzania. Tuendelee kumpa mama ushirikiano ili tuijenge Tanzania Bora na Imara. kazi Iendelee.

N.B Naombeni kura zenu kwa yeyote atakayevutiwa na maua haya niliyoamua kumpa mhe. Samia Suluhu Hassan. Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Imeandaliwa na frolian mwesiga Matungwa.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom