Tumpe zawadi iliyo bora Freeman Mbowe

Tumpe zawadi iliyo bora Freeman Mbowe

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
3,197
Reaction score
7,677
Kwanza hongereni sana wale majasiri wote wa CHADEMA wanaofanya kazi takatifu ya kuwapa elimu wananchi juu ya haki yao ya kuwa na katiba bora itakayolenga kulinda haki zao.

Mheshimiwa Mbowe, yupo ndani kwa sababu ya kuongoza mapambano ya kupata katiba mpya. Waliomkamata Mbowe na kumfungia huko, matarajio yao ni kuwa wakimweka ndani huyu kiongozi shujaa, asiyeyumba na asiyerubuniwa, yale mapambano ya kutafuta katiba mpya yatakoma. UlYakikoma, watakiwa wamefanikiwa. Inatakiwa tuhakikishe hawafanikiwi, na kila dalili inaonekana, jitihada za kupata katiba mpya, zitashinda.

Kinachotakiwa sasa, ni wananchi tuidai katiba mpya kwa nguvu zaidi na kwa umoja zaidi. Hiyo ndiyo zawadi kubwa tunayoweza kumpa Mh. Mbowe. Mbowe atakapotoka huko walikomfungia, akikuta moto aliouwasha umekuwa mkali zaidi kuliko hata alivyouacha, atafarijika sana, na itakuwa ni zawadi kubwa kwake kuliko kitu chochote.

Tusilie wala tusihuzunike kwa Mbowe kubambikiwa kesi, bali tufanye kazi. Kubambikia watu kesi kulianza tangu enzi za Yusuf kule utmwani Misri. Bwana wetu Yesu Kristo, alibambikiwa kesi ya uchochezi na wayahudi.

Shetani hajawahi kuacha kufanya kazi. Shetani kama alivyofanya kazi enzi za Yusuf na enzi za Bwana wetu Yesu Masiha, ndivyo anavyofanya kazi sasa. Mh. Mbowe, hastahili kusikitika bali kufurahia kuona kuwa amepita kwenye njia ambayo watu wema waliowahi kubadilisha mataifa na Dunia, walipita.

Timu zile za CHADEMA digital zinafanya kazi iliyotukuka hasa, na kwa kweli, kwenye hili, naiona CHADEMA ikiwa mbele ya vyama vyote vya siasa. CHADEMA digital ipite kila mtaa, kila mji na kila kijiji ili kuwadhihirishia wale mawakala wa shetani kuwa ubaya hauwezi kuushinda wema.
 
Sawa kabisa, zawadi kuu na iliyo bora kwa Mh. Mbowe si sisi sote kuungana kudai KATIBA MPYA, bila katiba mpya yoyote haya tufanyayo ni kazi bure.
 
HII APA AKITOKA APAMBANE

New Microsoft Word Document (3)-1.jpg
 
Hakuwekwa ndani kwa kudai katiba, kudai katiba ni haki ya wananchi ila kwa kufuata sheria na mda mwafaka. Sababu aliyosema Mama ndiyo husika, acha mahakana ifanye kazi yake.
 
Muda mwafaka ni mwaka gani?
Hakuwekwa ndani kwa kudai katiba, kudai katiba ni haki ya wananchi ila kwa kufuata sheria na mda mwafaka. Sababu aliyosema Mama ndiyo husika, acha mahakana ifanye kazi yake.
 
Mpaka marekebisho ya uchumi yamalizike haijalishi ni mwaka gani.
 
Kwanza hongereni sana wale majasiri wote wa CHADEMA wanaofanya kazi takatifu ya kuwapa elimu wananchi juu ya haki yao ya kuwa na katiba bora itakayolenga kulinda haki zao...
Kabisa....tunaunga mkono jitihada za CHADEMA kuleta katiba mpya na kuondoa dhuluma na ukandamizaji wa watawala. CHADEMA DIGITAL tupo pamoja.
 
Jamani yalio ajili mahakani leo shahidi hamna, mtupe uuzi tunataka kufuatlia aibu kubwa ya taifa hili
 
Kwanza hongereni sana wale majasiri wote wa CHADEMA wanaofanya kazi takatifu ya kuwapa elimu wananchi juu ya haki yao ya kuwa na katiba bora itakayolenga kulinda haki zao...
Kazi Nzuri aliyofanya Mwenyekiti hadi anakamatwa imefanikiwa vizuri. Kupitia kesi hii Wananchi wameongeza mwamko wa Katiba Mpya.
 
Hakuwekwa ndani kwa kudai katiba, kudai katiba ni haki ya wananchi ila kwa kufuata sheria na mda mwafaka. Sababu aliyosema Mama ndiyo husika, acha mahakana ifanye kazi yake.
Mbona unaandika kama mpumbavu?
Sheria inasemaje kuhusu kudai katiba?
Muda wa kudai katiba ni upi kwa akili yako?
Mjinga sana wewe,CCM imejaza takataka kwenye chama chao ndiyo maana wapuuzi kama wewe hawaogopi kuandika ujinga bila kufikiri.
Stupid.
 
Back
Top Bottom