Tumpende na kumheshimu Rais wetu Mama Samia

Tumpende na kumheshimu Rais wetu Mama Samia

KITEKSORO

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2012
Posts
346
Reaction score
425
Wapendwa watanzania wenzangu, nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( salamu maalum aliyoiasisi Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan na ambayo kiitikio ni "Kazi iendelee").

Mimi huwa napenda sana jinsi Malkia wa Uingereza (kwa sasa Qween Elizabeth) anavyopendwa na kuheshimiwa sana na watu wake. Ukiangalia hafla mbalimbali anazohudhuria Malkia unaona kabisa ukuu wake unavyojidhihirisha.

Sisi Tanzania kwa mipango yake Mungu mwenyewe tumebahatika kuwa na Rais mwanamke Mh. Mama yetu Samia Suluhu Hassan. Mimi binafsi nafarijika sana nikimuangalia na kumsikiliza Mama Samia. Ni Rais lakini ni Mama kabisa yaani ana upendo wa dhati kabisa wa mama na ana nia ya dhati ya kuiongoza nchi yetu kwa amani na kwa kuzingatia utawala wa sheria.

Ukifuatilia historia ya Mama Samia utaona kabisa ni Mwanamke mpambanaji na amefanikiwa sana katika mambo mengi. Unaweza kuona kabisa kwamba hadi wakati anakuwa Makamu wa Rais na hatimaye Rais wetu, alikuwa anajitosheleza kwa kila kitu kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Mimi naamini Mama hayuko kwenye kile kiti kutafuta chochote (kiuchumi, kijamii na kisiasa) maana vyote amejitosheleza. Hivyo, naamini yuko pale ili kuongoza nchi hii ipate maendeleo zaidi na watanzania tuishi kwa furaha bila hofu.

Nawasihi sana watanzania wenzangu tumpe Rais wetu "treatment" kama ile anayopewa Malkia wa Uingereza. Hebu ona hapa kwa mfano



Vitabu vya dini vinatuambia mamlaka za duniani hutoka kwa Mungu, hivyo tuziheshimu mamlaka hizo. Rais ni alama kuu ya nchi. Tumheshimu sana Rais wetu.

Namuoba Mungu ampe Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan afya njema kimwili, kiakili na kiroho ili aendelee kuiongoza na kuiletea maendeleo Tanzania yetu.

Nawatakia Mapinduzi Day njema wapendwa.
 
Siyo kila mwanamke ni 'MAMA'. Hakuna mwanamke mwenye sifa za kuwa 'MAMA' anayebambikia watu kesi wala kufanya upendeleo. Siyo kila mwanamke ni Mama. Tuna Rais mwanamke aliyekosa sifa ya kuwa mama. Fikiria:

1) Kumbambikia kesi ya ugaidi Mbowe na makomandoo. Kuwabambikia watu kesi, kuruhusu mateso na wengine huenda wameuawa, ni ushetani wa hali ya juu, na Samia amebariki na kuufurahia

2) Kusimamia mgawanyo wa upendeleo wa pesa za mikopo kati ya Tanganyika na Zanzibar, tofauti na kanuni za Muungano, ni upendeleo. Hakuna mama kamili anayefurahia upendeleo na dhuluma

3) Unafiki wa hali ya juu unaotaka kutendwa na serikali na CCM chini ya uongozi wake kwa kile kilichopewa mbadiliko ya katiba kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi, ni uthibitisho mwingine kuwa Serikali na CCM bado ipo chini ya mamlaka ya shetani na kanuni zake, kanuni kuu ikiwa unafiki na ulaghai

4) Mwanamke mwongo anabakia kuwa mwanamke lakini hawezi kuwa 'MAMA'. Wewe hukumsikia huyu mwanamke akisema kwamba Mbowe ni gaidi, alitoroka nchi, na wenzake wamehukumiwa. Haya ni maneno ya kweli? Huyu mtu ni mwongo. Ni kiongozi anayeuma na kupuliza, lakini huwezi kusema ni kiongozi ambaye Taifa lingefurahia kuwa naye.

Ana unafuu kuliko marehemu, lakini siye anayelifaa Taifa. Bado Taifa halijampata kiongozi anayenena haki, anayeiishi haki, anayetembea juu ya haki, anayeilinda na kuitetea haki, siyo kwa unafiki bali kwa dhamira.

Malkia wa Uingereza anaheshimika kwa sababu ya upendo wake wa kweli kwa Taifa lake na wananchi wake. Nani aliwahi kubambikiwa kesi na malkia wa Uingereza?

Samia hana sifa ya kupendwa. Unataka apendwe na watu wanaochukizwa na dhuluma wakati yeye ni miongoni mwa watenda dhuluma?
 
Back
Top Bottom