Tumsaidie Alan Shomari, mchezaji wa zamani wa Yanga

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Hakika inasikitisha sana TFF na Klabu zetu zinapowatelekeza Wachezaji wake walioliletea Taifa na Vilabu zetu wakati wanacheza mpira.Mchezaji Allan Shomari alikuwa Mchezaji mahiri wa Klabu ya Yanga na Timu ya Taifa.Mchezaji huyu amepoteza uwezo wa kuona hali ambayo inamfanya ashindwe kuendesha maisha yake na familia yake.Mchezaji huyo amekuwa akiomba omba misaada ili iweze kumsaidia.Tunaishauri TFF na YANGA viangalie namna ya kumsaidia Mchezaji huyu,kumbukeni alivyoisaidia Timu ya Taifa na Klabu ya Yanga.Mbona hivi karibuni Mh.Rais alimsaidia Mchezaji Peter Tino kwanini na nyie TFF msimsaidie Allan Shomari na wachezaji wengine waliolitumikia Taifa letu?Vivyo hivyo kwa Vilabu vyetu Viwakumbuke japo mara moja Wachezaji waliovichezea miaka ya nyuma kwani walijitoa.
 
Kila mtu na abebe msalaba wake!
 
TFF Wangekua wanafanya Charity fulani hivi hata wangefanya vipindi ktk tv na kuelezea changamoto mbalimbali ziwapatazo wachezaji wetu wa zamani nina hakika wengi tungeguswa na hasa ikianikwa namba halisi ya mchezaji husika tusingeshindwa kurusha M pesa/tigo pesa japo 2000/= 3000/=
 
Hapa TFF au YANGA watasikia au unataka upate platform ya kuonesha na ww kuna kidudu kinazunguka kichwani?
Wakati anacheza hakuwa analipwa? Alikuwa anafanyia nn posho na mahahara wake?
 
Zamani kulikuwa na talents lakini ela ilikuwa sio.
Siku hizi kuna ela lakini talents sio .
Hawa kina alan shomari , tino na wengine waanzishiwe foundation ya kuwatunza kama vile pensheni
 
Yawezekana hii sio taarifa mpya kwa baadhi yetu lakini kwangu kiukweli ndio nimezipata leo.

Kati ya Wachezaji ambao majina yao yalikuwa yananikaa kichwani wakati ule nikiwa Bw Mdogo mmoja wapo ni Alan Shomari. Leo asubuhi kupitia Redio Free Africa nilisikia habari za Mchezaji huyu Alan Shomari, kwa mara ya kwanza leo ndio nimesikia kumbe yupo Arusha na anakabiliwa na tatizo la kutokuona (upofu). Kwa kweli nimeguswa kwani ni kati ya majina ambayo sitayasahau kichwani kwangu ingawa hata sikuwahi kukutana nao achilia mbali kukumbuka sura zao kupitia vyombo vya habari, zaidi ni Magazeti kwa wakati ule.

Ingawa mimi sio Shabiki wa Yanga, lakini jina la Alan Shomari ni kati ya majina kadhaa niliyokuwa navutiwa nayo kupitia kusikiliza matangazo ya Mpira ya RTD. Nilishawahi kuulizia humu walipo baadhi ya Wachezaji maarufu wa enzi hizo, haswa waliochezea Yanga na Simba miaka ya 80's.

Majina kama vile Alan Shomari (Yanga), Lila Shomari, Kiwelu Musa, Daudi Salum a.k.a Bruce Lee, Malota Soma, Zuberi Magoha, Sunday Juma, Makumbi Juma(Yanga), Hamisi Kinye (Yanga), Abdallh Mwinyi Mkuu, Ahmed Amasha(Yanga) n.k. Majina kama Zamoyoni Mogela, Idd Pazi, Moses Mkandawile walau wao nimeshasikia taarifa zao mara kadhaa.

Nami nitaangalia utaratibu wa kumuona Bw Allan na ninamtakia kila la kheri na Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi ndugu yetu tuyu.
 
Yaani huyu mchezaji amesubiri hadi mechi ya hisani ya Namungo na Simba ndio asaidiwe wakati utopolo wamekaa kimya kama sio mchezaji wao
 
Namkumbuka sana ni miongoni mwa mabeki bora kabisa kuwahi kuwepo pale Dar Young African.
 
Hivi Alan Shomari wa Yanga na Lila Shomari wa Simba walikuwa ni ndugu?.
 
KWANI ALIKUA ANACHEZA BURE? HUU NI UZEMBE WAO WA KUANDAA MAISHA YA UZEENI. WANAKULA STAREHE SANA WAKIWA VIJANA. SASA MNAWATAJA TFF KWANI MSHAHARA WAKE ALIKUA ANAKULA NA TFF??
 
KWANI ALIKUA ANACHEZA BURE? HUU NI UZEMBE WAO WA KUANDAA MAISHA YA UZEENI. WANAKULA STAREHE SANA WAKIWA VIJANA. SASA MNAWATAJA TFF KWANI MSHAHARA WAKE ALIKUA ANAKULA NA TFF??
Kaka miaka ya 80 kulikuwa hakuna mpira pesa. Ili kuwa mpira mahaba kwa hiyo comment kistaarabu sana .
Yaani sawa kumwambia mama yako alimpendea nini baba yako kapuku!
 
Hapa TFF au YANGA watasikia au unataka upate platform ya kuonesha na ww kuna kidudu kinazunguka kichwani?
Wakati anacheza hakuwa analipwa? Alikuwa anafanyia nn posho na mahahara wake?
Ukweli ndio huo ila daaah huo uwasilishaji wako sasa, ila pamoja na yote miaka ya nyuma mpira ulikuwa haulipi kama nyakati hizi mkuu
 
Kaka miaka ya 80 kulikuwa hakuna mpira pesa. Ili kuwa mpira mahaba kwa hiyo comment kistaarabu sana .
Yaani sawa kumwambia mama yako alimpendea nini baba yako kapuku!
Jibu zuri sana hasa hii para ya mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…