Tumsaidie huyu dungu yetu

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2011
Posts
1,639
Reaction score
519
Wana JF,
Kuna jamaa yangu mmoja anaomba ushauri wa kiafya na kisaikolojia.
Yeye ni mwanafunzi wa Masters, na analalamika kwamba mwalimu wake anamsumbua sana.
Siku za hivi karibuni anadai amekuwa na wasiasi na uwonga mkubwa sana bila kujua chanzo ni nini.
Akipanda hata lift (elevator), ule mshituko wa kuondoka na kusimama anakuwa anaogopa sana kitu
ambacho hakuwa nacho kabla. Mbaya zaidi mwezi uliopita alipanda denge ambapo tangu kuondoka
mpaka kufika alikuwa na wasiwasi mkubwa kitu ambacho hakuwa nacho kabla.
Sasa amenieleza mimi tatizo lake hilo nikamwambia tutazungumza.
Naombeni msaada wenu wana JF
 

hujaeleweka.
 
Sioni uhusiano wa shule yake na tatizo la woga, hebu funguka vizuri.

Yeye ni she au he?
Bado virgin?
 

haueleweki kabisaa_mara umwingize mwl,mara lift,mara ndege,....ebu tulia halafu uiandike upya hii thread plz.
 
Mwambie akafanye check up, yaweza akawa ananyemelewa na Blood Pressure
 
Dungu au ndugu? Denge au ndege? Hueleweki au ww ni muhindi?
 
nafikiri ana mapepo, achague Lusekelo au Mwingira, naweza kumuombea, tunaweza kuwasiliana kupitia JF.
 
mmeyaona?
Ndo maana hata hysteria mtu anaenda ombewa badala ya kwenda hospital

nafikiri ana mapepo, achague Lusekelo au Mwingira, naweza kumuombea, tunaweza kuwasiliana kupitia JF.
 
Huo woga umeletwa na usumbufu wa mwalimu au? Hujaeleweka manake umechanganya habari hapa.
 
nimependa kiswahili chako kwenye
"dungu" na "denge"

:focus:

nadhani rafiki yako atafute wataalamu wa saikolojia, watamsaidia
 
jipange upya katika maelezo
 
jipange upya katika maelezo
Hii JF kweli! Huelewi nini sasa?

Jamaa anasema kuwa amekuwa akikabiliwa na hali ya wasiwasi mkubwa kwenye matukio madogo tu tofauti na zamani. Mfano, alikuwa apanda lifti ya majengo bila kuwa na hali hiyo, lakini siku hizi akipanda lifti ule mshituko wa lifti wakati wa kuanza kuondoka au kusimama apatwa na huo woga. Kwenye ndege ndo balaa, mwanzao mpaka mwisho wa ndege anomba kufika haraka, na kwenye turbulence ndo balaa zaidi.
Sasa nauliza wataalamu wa JF, je hii hali yaweza kuwa imechangiwa na nini?

J
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…