Tumsaidie Rais Samia kuwaondoa Watendaji Mizigo

Tumsaidie Rais Samia kuwaondoa Watendaji Mizigo

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kama Wananchi tunalo jukumu takatifu la kumsaidia mama Samia kuwaondoa serikalini watendaji mizigo wakiwamo Mawaziri.

Hii ni hata kama jukumu hilo linaweza kuwa chungu, hatari au kuwa na consequences kwetu:

IMG_20210707_084839_278.jpg


Viongozi waongo wakiwamo wasioheshimu haki, wala uhuru wa watu zetu, sheria au wavunja katiba, hawatufai.

Viongozi kama kina katelefoni, pale wizara ya afya au hawa waliotufikisha hapa:

IMG_20210719_193611_569.jpg


kwa hakika wanatakiwa kutupisha tu.

Tunakaza hapo hapo.

Mwigulu must go!
 
Mamlaka yote yapo mikononi mwake mimi nimsaidie vipi? aliamua kuendelea nao kwasababu aliona wanamfaa, kama watendaji wake ni mizigo basi hata naye ni mzigo.
 
Eti tumsaidie, kwani mnapipwa wote? anazinguwa huyo bibi

Kiswahili ni kipana sana jomba.

Kujua namna ya kumfukuza mtu bila kumwambia toka, akaondoka. Hakushushi maana ya kuwa kaondoshwa.

Tatizo la kujua namna ya kukipata kinachohitajika, ni tatizo sugu hasa kwa wajidhaniao kuwa wanajua.

Hilo hubeba sehemu kubwa ya failure.
 
Rais wetu mpendwa alitakiwa kupanga safu itakayoendana naye, hao wa Mwenda awabwage tu.
 
Mamlaka yote yapo mikononi mwake mimi nimsaidie vipi? aliamua kuendelea nao kwasababu aliona wanamfaa, kama watendaji wake ni mizigo basi hata naye ni mzigo.

Kiswahili ni kigumu. Labda haswa pale kinapohusianisha uwezekano wa makabiliano.

Tozo za kizalendo ziko "under review." Kistaarabu tumemsaidia Mama kuamua hizi tozo kuwa "reviewed:"


Mama anapokuwa na watu aina ya kina Mwigulu ambao yeye "be it" angependa kufanya nao kazi hali kwetu hawatufai hatupaswi kukaa kimya.

"Kuwapigia kelele watu kama hao na au kushinikiza waondoshwe, kistaarabu ndiyo kumsaidia Mama kuwaondosha hivyo."

Unadhani hili la miamala wamefurahia hata tulipowafikisha? Hilo ni tatizo lao. Kwani sisi tukiliita tumewasaidia kufikia kuamua badala ya kusema "tumewanyoosha," kwani kuna tatizo gani?

Ama kwa hakika kwa kuendelea kukomaa na hii miamala tutakuwa tumemsaidia Mama kumwondosha Mwigulu.

Mwigulu must go!

Shikamoo - waswahili wabobezi (bila kuwasahau mzee wa Msoga, wazanzibari na wazanzibara wote).
 
Rais wetu mpendwa alitakiwa kupanga safu itakayoendana naye, hao wa Mwenda awabwage tu.

Tunao mchango wa kumfikisha hapo. Awe anataka au hataki, lakini kama tuko strategic.

Uswahilini wanaita kujua namna ya kumsukuma mlevi:

IMG_20210719_223046_853.jpg


Mwigulu must go!
 
Kwa uchumi unaoendeshwa kisiasa mtabadilisha kila siku. Mtafanya rotation mpaka wabunge wote wawe mawaziri wa fedha na hamtafanikiwa. Nchi na uchumi wa tanzania unaendeshwa kisiasa sana.

Tuko katika kudai katiba mpya kuelekea katika kuweka mengi sawa sawa.

Kuna yasiyo na haja ya kusubiri katiba mpya:

Waongo, wakiuka sheria, wakiuka haki, dhulumati, wavunja katiba hao si wa kulea. Kwani haisaidii.
 
VP anaweza tenguliwa? Huyu nae kimeo kabisa.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app

Naunga mkono hoja.

Zile ripoti za CAG BOT na TPA zilizofunikwa funikwa haziwezi kumwacha salama.


Mama auvae ujasiri atuonyeshe nia yake thabiti kuheshimu haki, usawa na demokrasia.

Mbona March - June tulikuwa vizuri?
 
Back
Top Bottom