Tumshauri afanyaje ili aweze kurudia mtihani

Perry

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
10,058
Reaction score
2,195
yeye ni mwanafunz wa mwaka wa kwanza katika chuo flan hapa dar. Alifiwa na mama yake mzazi na akapata taarifa za msiba masaa machache kabla ya kuanza mtihani wake wa kwanza wa kumaliza semister ya pili. Anadai alijkaza akafanya mtihani wa kwanza salama lakini akawa ameomba kutokufanya walau mtihani mmoja ili atulize akili kutokana na msiba wa mzazi wake.

Sasa matokeo yao yametoka na anasema hajafanya vizuri kabisa so anaomba tumpe ushauri wa kama ataweza kuomba chuo kimfutie matokeo yake ya mwanzo ili aweze kufanya mitihani upya kwa kigezo cha kwamba alifanya mitihani ile akiwa kwenye mood mbaya. Mimi binafc nimeshndwa kumshauri coz suala hili liko nje ya uwezo wangu wa kufikiri. Kwa hiyo nikaona niwaletee na nyie wakuu wa humu wenye uwelewa zaidi wa mambo ili muweze kumshauri nin cha kufanya.
 
Miaka yetu ya Nyerere kulikuwa na matatizo ya mawasiliano nikiwa na maana kuwa mawasiliano hayakuwa ya haraka kama sasa. Hii ina maana habari zilifika kwanza kwa administration (Dean, secretariat) au vyama vya wanafunzi. Hapo ina maana kuwa institution ilikuwa na habari tangu mwanzo. Kwa kesi hii uluyoleta, iwapo wahusika walikuwa na habari za kifo tangu mwanzo, kwa ubinadamu wanaweza kumpatia chance ya kurudia mitihani. Ila iwapo anawaeleza sasa habari iliyopita wakati matokeo yameshatoka nafikiri itakuwa vigumu kurekebisha. Nafikiri cha muhimu nijaribu kuomba kurudia mitihani. Nakutakia mafanikio
 
pole zake aiseee. ngoja wenye kujua waje.
 

Hivi ukirudia paper ata kama umescore A kwenye cheti si wanakuandikia C jamani au ni kwa chuo chetu tu?
 
Hivi ukirudia paper ata kama umescore A kwenye cheti si wanakuandikia C jamani au ni kwa chuo chetu tu?

hiyo unayosemea wewe mkuu ni case ya supplementary,yeye anataka kurudia kama special exams ambazo kama itatokea ukipata A unawekewa A yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…