Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Ushindi wa Jihan miss grand international unaendelea kudhihirisha jinsi gani umoja wa rangi/races, makabila na dini ni faida zaidi kwa Tanzania.
Kwa siku za hivi karibuni Tanzania haijawahi kuonekana kinara katika jambo kubwa la kimataifa. Imechukua Mtanzania mwenye asili ya Lebanon kutuweka kwenye ramani ya dunia kwa ushindi wa shindano la urembo.
Kwenye biashara pia bilionea anayetambulika duniani ni Mtanzania mwenye asili ya India, Mo Dewji. Kwenye digital Mtanzania anayetutambulisha duniani pia ni Mtanzania mwenye asili ya India aliyeanzisha kampuni ya Nala. Mtanzania M
muwekezaji mkubwa nje ya nchi ni Rostam Azizi mwenye asili ya Iran.
Hakika Tanzania inazidi kusonga mbele. Tuendelee kudumisha amani, udugu na umoja.