John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Tumshukuru Mungu kwa Kila Jambo
Shukrani ni nini
Shukrani au kushukuru ni kitendo cha kutambua (appreciate) au kujua matendo ya Mungu katika maisha ya kila siku. Ni vema tukatambua kuwa kila kinachopatikana kwenye maisha ya kila siku siyo kwa nguvu zetu wenyewe, bali ni Mungu ndiye anayefanikisha. Shukrani ni ile hali ya kurudisha hisia chanya kwa mema au mabaya yaliyokufikia.
Kwa tafsiri ya kidunia, shukrani inatolewa pale mtu anapopokea mambo mema. Kwa mfano, mtu atarudisha shukrani aidha ya maneno au matendo, pale anapopewa zawadi ya kitu, au anapofanyiwa jambo fulani jema. Mtu hawezi kupokea zawadi na kisha akakaa kimya tu, kwani siyo uungwana, na haioneshi ukaribu kati ya wahusika. Ni lazima mpewa zawadi atasema neno la shukrani, hata kama ni kwa kutabasamu.
Lakini, kibiblia, shukrani inatolewa si tu baada ya kupokea mambo mazuri au mema, bali pia kwa mambo yote, hata kwa yale mabaya. Ndivyo biblia inavyofundisha.
Kitabu cha 1Wathesalonike 5:18, kinasema “shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu”.
Kitabu cha Ayubu 2:10, kimesema, "Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake".
Maana yake ni kuwa ni lazima kumshukuru Mungu hata katika yale mambo ambayo tunaona hayajaenda kama tulivyotarajia. Hii ni pamoja na misiba, na hata tunapopata hasara wakati mwingine. Ni kwa sababu tunajua yote ni mapenzi ya Mungu kwetu, kwani upo ndani ya Kristo.
Moyo wa shukrani ni moyo unaompendeza Mungu, na moyo usio na shukrani huondoa/hukausha mema yote na baraka zote kwetu kutoka kwa Mungu.
Wengine wanajifungia milango yao ya baraka kwa kukaa kimya pale wanapotendewa jambo fulani na Mungu, liwe zuri au liwe baya. Lakini wengine wanaendeleza milango ya baraka baada ya kumshukuru Mungu kwa mambo waliyotendewa.
Shukrani ni jambo linalompendeza Mungu na linaloendeleza baraka juu yetu.
Kitabu cha Luka 17:12-19, kinasema, “Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali, wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.
Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria. Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa”.
Sadaka ya shukrani
Shukrani inayoambatana na sadaka ina nguvu zaidi kuliko ya maneno tu.
Hebu tuangalie mfano wa shukrani kutoka kwa walioponywa ugonjwa wa ukoma (Mathayo 8:2-4).
2 Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.
3 Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika.
4 Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.
Utaona kuwa Yesu mwenyewe ndiye alielekeza kutoa sadaka baada ya uponyaji. Hiyo ilikuwa ni sadaka ya ushuhuda wa uponyaji. Hivyo, sadaka ni sehemu ya shukrani kwa Mungu, kuwa ametenda jambo kwako.
Faida za shukrani kwa Mungu
1. Ni silaha dhidi ya hila za adui
2. Huimarisha imani na unyenyekevu juu ya Mungu
3. Hualika utukufu wa Mungu na uwepo wake na kuendeleza baraka juu yetu
Wakati mzuri wa kumshukuru Mungu
Ni vizuri shukrani zitolewe pale siku inapoanza, na inapoisha. Tunapoamka asubuhi na kuianza siku ni lazima kumshukuru Mungu kwa ulinzi wa usiku kucha, na kwa kukupa siku mpya. Vile vile, unapoimaliza siku ni lazima kumshukuru Mungu kwa kuimaliza salama na kwa ulinzi.
Baadhi ya mistari ya shukrani katika biblia
Zaburi 28:7: “Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru”.
Zaburi 35:18: “Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi”.
Zaburi 71:22: “Nami nitakushukuru kwa kinanda, Na kweli yako, Ee Mungu wangu. Nitakuimbia Wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli”.
Zaburi 118:21: “Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu”.
Zaburi 136:1: "Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele".
Shukrani ni jambo linalompendeza Mungu na linaloendeleza baraka juu yetu. Tukifanikiwa, tumshukuru Mungu ili kuendeleza milango ya baraka. Tusipofanikiwa, tusimkasirikie Mungu, bali tumshukuru Mungu. Kutomshukuru Mungu huondoa au hukausha mema yote na baraka zilizopo kutoka kwa Mungu; pia huziba connection na Mungu.
Hivyo, TUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO.
Sadaka ni sehemu ya shukrani. Kama Yesu Kristo mwenyewe alivyoagiza, tujitahidi kutoa sadaka ya shukrani kwa Mungu, kuwa ametenda jambo kwetu.
Mshukuru Mungu kila siku, pale siku inapoanza, na pale inapoisha, bila kuchoka. Kuchoka au ugonjwa, isiwe ni sababu ya kutomshukuru Mungu kila siku, asubuhi na jioni au usiku.