John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Tumtolee Mungu Vitu Vinavyotugharimu Zaidi
Tumtolee Mungu vitu vinavyotugharimu hata kuhatarisha Maisha.
Mfano wa mashujaa watatu wa Daudi
Hebu tuangalie mfano kuhusu Daudi, kupitia Mfalme wa pili, aya ya 23.
2Samweli 23:15 Daudi akatamani, akasema, laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango!
2Samweli 23:13 “Tena, watatu miongoni mwa wale 30 waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai. 14 Naye Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti wakati ule walikuwako Bethlehemu.
15 Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango! 16 Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; lakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana.
17 Akasema, Hasha, Bwana, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatarisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa”.
Hayo ndiyo waliyoyafanya mashujaa watatu wa Daudi.
Tumeona kuwa kuna wakati Daudi alipokuwa katikati ya vita vikali na Wafilisti, wakati akiwa kule mafichoni katika pango moja lijulikanalo kama pango la Adulamu, alitamani maji ya kisima kilichokuwa Bethlehemu.
Lakini, wakati huo mji wa Bethlehemu, ambao ndio ulikuwa mji wa Daudi, ulikuwa umezungukwa na Wafilisti, maadui zao, na ndipo walipokuwa wameweka kambi zao hapo. Biblia inatuambia, Daudi akiwa kule mabondeni, alitamani sana maji ya kisima cha Bethelehemu, kule maadui zake walipo.
Watatu kati ya wale mashujaa wake 30 aliokuwa nao waliposikia maneno yale ya Daudi, wao wenyewe kwa siri, wakapanga mikakati ya kwenda kumletea Daudi maji ya kisima kile, bila hata ya kumwambia.
Ndipo wakaanza safari kutoka katikati ya kambi ya Daudi, wakaondoka hivyo hivyo bila kujali wanakwenda kuingia katika kambi ya maadui zao. Ili kufikia kisima hicho ilikuwa ni lazima upenye katikati ya Wafilisti.
Lakini wao waliondoka hivyo hivyo, wakadhubutu kuhatarisha maisha yao, kwa hali na mali, ili tu wafikie azma yao ya kuchota maji yale ya kisima kile, na kumletea Daudi.
Halikuwa jambo rahisi. Si jambo rahisi kibinadamu, lakini hawa mashujaa watatu wa juu wa Daudi hawakujali hilo.
Walifanikiwa kweli kupenya katikati ya wale watu kisiri, na kuchota maji yale ya kisima cha Bethlehemu na kumletea Daudi. Lakini, Daudi alipoona maji yale, tunaona mwitikio wake ulikuwa ni kinyume na matarajio yao.
Kama tunavyoona, Daudi hakudhubutu kuyanywa maji yale. Kwa nje yalikuwa yanaonekana ni maji, lakini kwa ndani Daudi aliyaona ni damu.
Na damu siku zote huwa hainywewi, kwa sababu damu inabeba uhai. Na uhai unazungumza.
Daudi aliona maji yale ni dhabihu tosha, ambayo haistahili kutolewa kwake ila kwa Mungu peke yake. Na ndiyo maana alichokifanya ni kuyachukua yale maji na kwenda kuyamwaga mbele za Bwana, kama vile damu inayomwagika kwa ajili ya dhabihu.
Tunaona kuwa, badala ya maji yale kwenda tumboni mwa Daudi, yalikwenda moja kwa moja hadi katika madhabahu ya Mungu mbinguni. Na bila shaka kwa tendo lile, si tu Mungu aliwarehemu wale watu kwa jicho la tofauti, bali pia kuwapa ushindi dhidi ya maadui zao.
Habari hiyo inafunua nini katika agano jipya
Daudi anamfunua Bwana wetu Yesu Kristo. Kumbuka wale mashujaa wa Daudi walikithamini kiu cha Daudi, hawakujali kuwa hata pale kulikuwa na maji mengi tu. Si angekunywa ya pale, kwa nini atafute ya mbali.
Lakini wao hawakujali hilo, hivyo wakawa tayari kuhatarisha maisha yao kwa ajili tu ya kuishibisha kiu yake. Kwa tendo lile, ikamfanya Daudi asiyanywe maji yale, bali kwenda kuyamwaga mbele za Bwana.
Kristo naye alipokuwa msalabani alisema ninaona kiu. Lakini wale askari hawakuithamini kiu yake. Vilevile, hadi sasa, Kristo anasema ninaona kiu, lakini wengi wetu tunaidharau kiu yake. Tunaona kama anataka kutuua huyu, kutufilisi.
Yeye si ana kila kitu, iweje tena atuombe sisi maji. Kwenye Mathayo 25, utaona Yesu anawaambia wale watu aliowafananisha na mbuzi, kuwa alikuwa na kiu, lakini hawakumnywesha (mstari wa 42). Vile vile, na wale wengine ambao aliwafananisha na kondoo, akiwaambia nilikuwa nina kiu na mlininywesha (mstari wa 35).
Ni kweli tunamnywesha kila siku maji kwa matoleo yetu, lakini je, maji hayo tunaweza kuyageuza kuwa damu, kiasi kwamba ashindwe kuyanywa na kuyamwaga mbele za Mungu mbinguni kama dhabihu?
Kristo anatazamia, tumtolee kilicho bora, bila kujali inatugharimu kiasi gani.
Bila kujali tutapoteza nini, au tunapata hasara kiasi gani. Hiyo yote ni kwa faida yetu sisi wenyewe. Anataka tumtolee Mungu vile vinavyotugharimu na tunavyovionea uchungu kuvitoa.
Kwa kufanya hivyo, haitamfikia tena kama maji yakatayo kiu, bali sadaka yako itamfikia kama DAMU, kama uhai wako mwenyewe.
Ukiingia gharama kubwa kumpa Kristo kitu fulani, jambo ambalo mtu wa kawaida hawezi kufanya, mbinguni unahesabika ni kama umemwaga damu yako kwa ajili yake. Haijalishi hicho kitu ni kidogo kiasi gani, kinachojalisha ni gharama uliyoingia, je ni kubwa kiasi gani mbele za Mungu.
YULE MWANAMKE ALIYEKUWA MJANE, ALIINGIA GHARAMA KUBWA KWA KUTOA KILA ALICHOKUWA NACHO, INGAWA KWA NJE ILIKUWA NI SENTI MBILI TU.
Mtu anayefanya hivyo, anapata thawabu kama tu aliyechinjwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu. Hivyo tumtolee Mungu vile vinavyotugharimu zaidi, ili tuvuke si viwango vya baraka tu za kimwili, bali hadi zile za mashahidi wa Yesu.