Amani iwe nanyi,
Kwa kuwa tumemaliza uchaguzi na umepitia katika hali ya kushangaza pale matokeo yalipotangazwa kuona chama tawala kikishinda katika chaguzi zote za uraisi, ubunge na udiwani kwa "kishindo", ni vyema tukajifariji kwa pande zote zilizoshinda na kushindwa kwa haki kwa Kumuomba Mwenyezi Mungu ili atujaaliye amani na upendo katika maisha yetu. Lakini tukumbuke dhulma haina nafasi katika jamii ya wapenda haki na amani.
Uchaguzi huu umeonyesha jinsi gani mfumo wetu wa demokrasia ulivyo na dosari, na dhahiri shahiri hakutakuwa na upinzani wa kweli ndani ya nchi hii, hivyo basi ni bora turudi kwenye mfumo wa chama kimoja ili tuweze kueleweka ni jinsi gani tunataka mfumo wetu wa utawala uwe, hii si dalili nzuri kwa nchi kama yetu ya Tanzania kwani tunaweza tukakaribisha machafuko na uvunjifu wa amani ambayo ni jambo pekee tunalojivunia nalo.
Hivyo basi tuombe sana tena sana, kuliko tulivyo omba wakati wa Corona ili tuepushwe na dhambi hii ya dhulma. Aameen.