hivi hatuwezi kuwa na hospitali 2 au tatu za kimataifa kwa maana madaktari watoke nje [ikiwemo watanzania wanaotibu watu wa mataifa mengine] na kuwepo na vyombo vyote ila vile tu visivyoweza kuzuia mtu kufa tena vya kisasa ili tutoe huduma kwa nchi zote zinazotuzunguka na za mbali hasa zile ambazo kama sisi zinaamini kuna wagonjwa muhimu wa kutibiwa nje ya nchi na wagonjwa wa kawaida ambao hawastahili kutibiwa nje ya nchi.
Suala zima ni biashara tu au mnataka kusema kuwa hali ya hewa ya majuu pia ni sehemu ya tiba ya mgonjwa basi hospitali zijengwe mporoto, mbeya, ilula, iringa au monduli, arusha yaani kule kwenye bardiiii kama ulaya ulaya vile!
Vinginevyo mimi waziri kalala natilia mashaka uwezo wangu na uwezo wako wa kubadili nchi hii na maisha ya walalahoi japo walalahai kadhaa wananufaika na mfumo uliopo tena kwa mapana na marefu.
Sera zinazoweza kutuponya na makali ya utandawazi ni hizi za kuwa na hospitali za kisasa, shule za kisasa, vyuo vya kisasa, mahoteli ya kisasa, miji ya kisasa ambayo kwayo lazima watu wa nje watakuja tu kutumia hela zao hapa wakiwa hai au wamekufa!
Kazi kwenu!