tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Bila kupepesa macho wala kutikisa masikio, naingia kwenye mada moja kwa moja. Katika andiko hili nimebainisha kinagaubaga mambo ambayo yalimuinua na kumdidimiza Magufuli ili mama Samia Suluhu aendeleze yale mambo mazuri na kutupilia mbali yale mabaya. Nitaanza na yale yaliyomdidimiza na kumalizia na yale yaliyompaisha.
1. Mishahara na masilahi ya wafanyakazi
Kama mnavyojua Rais Magufuli hajawahi kuwaongeza mishahara wafanyakazi kwa muda wa miaka 5 iliyopita na alikuwa hazingatii kuwapandisha madaraja kila baada ya miaka 3 kama sheria inavyosema. Katika utawala wake tumeshuhudia watumishi wa umma wakikaa miaka zaidi ya 8 bila kupandishwa madaraja, huku akijua fika kwamba jambo hili linawaumiza sana wafanyakazi pamoja na wategemezi wao. Wafanyakazi na wategemezi wao (idadi yao si haba) wana uchungu sana na uamuzi huu wa kikandamizaji.
Hivyo, namuomba mama Suluhu awapandishe wafanyakazi madaraja, awape nyongeza ya mishahara, na kila mwaka awe anawaongeza mshahara (statutory annual increament) kwa mujibu wa sheria.
2. Kikotoo dhulumishi
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, serikali ya Magufuli, iliamua kufuta fao la kujitoa na kuja na kanuni (kikokotoo) ya ajabu katika kukokotoa mafao ya wafanyakazi. Sababu ya kufanya hivyo iko wazi kwa kila mtanzania mwenye akili timilifu. Serikali imeifilisi mifuko hii kwa kuifanya Shamba la Bibi. Serikali wamekomba fedha zote kwenye mifuko hii na kuifilisi kabisa. Namuomba mama Suluhu afutilie mbali sheria hii kandamizi inayowadhulumu wafanyakazi mafao yao. Inasikitisha athari za ufilisi huu uliosababishwa na serikali ya Magufuli umepelekea wastaafu watarajiwa kuishi kwa kihoro pasipokujua hatima ya jasho lao walilolipigania kwa zaidi ya miaka 40 ya kuitumikia serikali kwa uaminifu.
3. Uhuru wa kujieleza, mahakama na polisi
Hakuna mtu asiyefahamu kwamba serikali ya Magufuli iliminya na kukandamiza demokrasia, uhuru wa kujieleza pamoja na uhuru wa vyombo vya habari kwa muda wote wa miaka 5 aliyokaa madarakani. Pamoja na ukweli kuwa serikali ya CCM imekuwa ikiwatumia polisi kama tawi la CCM kwa muda mrefu, serikali ya Magufuli imekithiri katika matumizi ya polisi kuminya upinzani na kuwakandamiza raia wasiokuwa na hatia.
Namuomba mama Samia Suluhu arejeshe demokrasia, uhuru wa habari pamoja kuacha matumizi ya polisi kuisaidia Serikali yake. Jeshi la polisi linatakiwa kuwa huru na kufanya kazi zake kwa weledi bila kuegemea upande wowote wa kisiasa. Pia tunaomba atokomeze hii tabia ya “watu wasiojulikana” kuteka, kutweza na kupoteza watu.
4. Uhusiano wa kimataifa
Uhusiano wa Tanzania na mataifa mengine ya nje ya Afrika umekufa kifo cha mende. Na jambo hili lilifanywa kwa makusudi na serikali ya Magufuli kwa kuwatukana wazungu kila siku huku akiwabatiza majina ya ajabu ajabu kama vile mabeberu, mashoga, nk. Imefikia hatua hata watalii wanaotamani kutembelea vivutio vya utalii nchini Tanzania baadhi yao wameamua kwenda Kenya na nchi nyingine zinazowathamini utu wao.
Dunia ni moja. Hakuna haja ya kubaguana kwa misingi ya rangi na kubatizana majina ya ajabu ajabu. Namuomba mama Samia Suluhu arejeshe uhusiano na mataifa ya nje na ashirikiane nao bega bega kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo waliyoyakosa kwa muda mrefu. Huwezi kuwatukana watu mabeberu huku ukiwategemea kuchangia zaidi ya 40% ya bajeti ya serikali. Haiwezekani.
5. Ubaguzi wa kijimbo
Tulimsikia Magufuli akitamka hadharani wakati wa kampeni kuwa ikiwa wapiga kura watamchagua mpinzani, hawezi kamwe kuwapelekea maendeleo. Utadhani hayo maendeleo alikuwa anayapeleka kwa fedha zake za mfukoni wakati anatumia kodi za watanzania wote.
Naomba mama Samia aondoe ubaguzi wa aina hii. Ajitahidi kutopendelea wananchi kwa misingi ya kisiasa kwa kuwa maendeleo hayana chama. Ukiwa na rais mbaguzi kama alivyokuwa Magufuli, nchi hii haitakaa ipate maendeleo kamwe.
6. Kuongoza nchi kwa matamko badala ya sheria
Katika utawala wa Magufuli tulishuhudia nchi ikiongozwa kwa matamko na bila kuzingatia sheria za nchi kwa miaka 5 mfululizo. Tumeshuhudia ndege zikinunuliwa na uwanja wa ndege kujengwa Chato bila fedha zake kuidhinishwa na bunge, ambacho ndicho chombo kinachowawakilisha wananchi. Aidha, fedha za umma Tsh Trillion 1.5 zilipotea katika mazingira ya kifisadi na mpaka sasa hazijatolewa maelezo yoyote.
Namuomba mama Samia aongoze kwa kufuata misingi ya sheria kwa kuwa sasa ameishaapishwa kuwa Rais. Na hiki ndicho watanzania wengi wanachokitaka kwa kuwa wamechoshwa kuburuzwa na Jeshi la Mtu Mmoja miaka nenda miaka rudi. Mtu huwezi kuongoza nchi kama vile unaongoza familia yako. Haiwezekani.
Pamoja na kwamba utawala wa Rais Magufuli ulikuwa na mapungufu lukuki, kuna mambo mazuri machache ambayo utawala wake ulifanya. Baadhi ya mambo hayo ni ujenzi wa miundombinu, udhibiti wa matumizi mabaya ya fedha za umma, kupunguza ufisadi na kuleta nidhamu ya kiutumishi serikalini. Sina shaka mama yetu Samia ataendeleza hayo mambo mazuri pale mzee Magufuli apoishia.
Mungu mbariki mama Samia Suluhu, Mungu ibariki Tanzania. Amina.