Tumuombee Mdude Nyagali, hukumu yake ni tarehe 28/6/2021

Tumuombee Mdude Nyagali, hukumu yake ni tarehe 28/6/2021

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mdude Nyagali ambaye ni Mkulima duni wa Jembe la Mkono kutoka Mlowo Mbozi , ameingia kwenye vitabu vya maajabu ya dunia kwa kushitakiwa kwa makosa mazito ya kusafirisha madawa ya Kulevya kutokea Pakistan kuja Tanzania na kuyasambaza bila kuwa na hati ya kusafiria (PASSPORT).

Bado tunaendelea kuchunguza namna binadamu asiye na mabawa na ambaye hakuwahi hata kupanda ndege alivyoweza kufika Pakistan na kubeba Madawa ya kulevya kisha kuyaleta shamba Mlowo ili kuyasambaza. Tunaamini Mahakama italeta ufafanuzi kwenye hilo.

Bali sisi tunaomfahamu Mdude kama mkosoaji mkubwa wa Serikali ya awamu ya 5 tunajua Mdude alitengenezewa kesi hiyo ya uongo ili kumkomesha kutokana na kuikosoa serikali , Ila tunaendelea kumuombea kwa Mungu ambaye ndio Mamlaka Kuu amsaidie na kumuachanisha na kuta za Magereza. Amina.

Joseph_O._Mbilinyi’s_Instagram_photo:_“Tukutane_MAHAKAMANI_kesho_asubuhi_MAKAMANDA_mliopo_MBEY...jpg


UPDATES :
=========

Hilda_Newton_on_Instagram:_“Tayari_Mdude_Nyagali_ameshafika_kwenye_chumba_cha_Mahakama_sasa_an...jpg
chadematz_on_Instagram:_“Kulia_Mratibu_wa_Uhamasishaji_Bavicha_Taifa_Mhe._Twaha_Mwaipaya,_wa_p...jpg

No_Hate_No_Fear_on_Instagram:_“Muda_huu_ndani_ya_Mahakama_kuu_Mbeya_Mdude_Nyagali_tayari_amefi...jpg



UPDATES 2 :
==========

MDUDE NYAGALI AACHIWA HURU
 
Naamini kesho ataachiwa huru, mashtaka dhidi yake yalikuwa ya uongo.
 
Mungu atamjalia wepesi..naamini atakuwa raia huru na ataungana tena na familia yake hiyo tarehe 28, inshallah.
 
Tuache kuombea familia zetu, tuombee wahalifu?

Wewe subiri mahakama ifanye kazi yake, acha munkari wa kichadema!

Akifungwa sijui utasema samia ni dikteta?

Hamjielewi kabisa!
 
Tuache kuombea familia zetu, tuombee wahalifu?

Wewe subiri mahakama ifanye kazi yake, acha munkari wa kichadema!

Akifungwa sijui utasema samia ni dikteta?

Hamjielewi kabisa!
Hukusoma uzi ila umekurupuka kuchangia tu ! umasikini wa akili ni mbaya sana !
 
Back
Top Bottom